Jamboleo na Kagame kuna nini?

Jamboleo na Kagame kuna nini?

Master Legendary

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
579
Reaction score
887
WanaJF,

Nimekuwa nafuatilia muda mrefu ufyukunuku wa hili Gazeti juu ya Kagame, kwa muda sasa limekuwa likiandika front page habari za Kagame zilizojaa fitna, majungu na story za hisiahisia tu.

Nimekuwa nikijiuliza Malengo ya hili Gazeti ni nini juu ya Diplomasia yetu na Rwanda au nani yuko nyuma ya hili Gazeti?

Tumeshuhudia Ikulu wakikerwa na Magazeti ya Rwanda yanayoandika hisiahisia zisizo na ukweli juu ya Rais Kikwete vipi kuhusu JamboLeo?

Masterlegendary na Kituru Nawashukuruni Kwa Kuliona Hilo Kwani Kwa Muda Mrefu Sana Nimekuwa Nikikemea Juu Ya Uandishi wa Gazeti hilo Pamoja na Haya Mawili Mtanzania na Jamhuri ila Nashukuru Yawezekana Ushauri Wangu Ulisaidia Kwani Siku Hizi Mtanzania na Jamhuri Hawaandiki tena Habari za Chuki na Kichochezi baina Yetu na Rwanda.

Kwa Kuwasaidia tu ni Kwamba Kuna Agenda Ya Siri ipo Nyuma Ya Gazeti La Jambo Leo Kila Siku Kuja na Articles mbaya na Za Kichochezi za Kuhusu Tanzania na Rwanda na Usisahau Kuwa Gazeti hilo Linamilikiwa Kwa Asilimia Kubwa Sana na Mwana ( Prince ) ambaye Aliyemleta Duniani ana Bifu, Chuki na Wivu Kwa PK Hivyo Kinachofanyika ni Gazeti La Mtoto Kujibu Mapigo Kwa Maslahi Ya Mdingi na Mama Yake na Naweza Nikakuhakikishia Kuwa Rwanda na Haswa Kupitia Kwa Rais Wao Hawana Chuki au Ubaya Wowote na Tanzania na Nakumbuka Hivi Majuzi tu hata ktk Msiba Wa Uncle Wangu Hayati Patrick S Qorro Nilibahatika Kutambulishwa na Mzazi Wangu Kwa Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania na Nikaona ni Fursa Nzuri sana Kwa Mimi Kuzungumza Nae Haya Yanayoendelea na Kiukweli Mheshimiwa Balozi Alisikitika Mno na Sana Kwa Media za Tanzania haswa Hilo Gazeti Kwa Kuwadanganya Umma Wa Watanzania Kuwa Rwanda Kupitia Rais Wao Wana Chuki na Tanzania.

Kaka Kinachofanyika ni Kwamba ktk Media Kuna Kitu Kinaitwa Agenda Setting Theory ambapo Vyombo au Chombo Fulani cha Habari Kinaanzisha Jambo Fulani Kwa Mlengo wa Chanya au Hasi Kwa Maslahi Ya Mtu au Kundi Fulani. Hili Gazeti linadhani Ni Sifa au Ufahari Kwa Inachofanya na Kama Wahusika Hawatalionya basi Tanzania Inakwenda Kubaya na Tutajishtukia Tunaingia Matatizoni na Kuharibu tena Uchumi Wetu ambao Ulianguka ktk Vita baina Yetu na Nduli Idi Amini Dada.

Kagame hana Shida Ya Vita bali Anajenga Nchi Yake na Anaiheshimu Mno Tanzania Kwani hata Yeye ni Mtoto Wa Tanzania Kupitia Kwa Hayati Baba Wa Taifa Mwalimu Julius Burito Kambarage Nyerere. Hivi Kwanini Gazeti hilo hilo la Jambo Leo Lisiwe Lina Address Matatizo Mengi Yanayoihusu Tanzania Kama Kuibiwa Kwa Twiga Wetu, Uharamia wa Wanyama Kama Tembo na Faru, Umasikini Mkubwa Kwa Watanzania, Mauaji Ya Walemavu wa Ngozi na Vikongwe, Matatizo Ya Vita Vya Ardhi baina Ya Wafugaji na Wakulima na Mengineyo Lukuki?

Naomba Niishie hapa Ila Inachokifanya Jambo Leo Siyo Journalism bali ni Stupidity na Nina Wasiwasi na Elimu na Ueledi wa Wahusika wa Gazeti hilo na Nimemdharau Sana Mhariri Wake Mkuu JP. Hivi Huwa Hawafanyi Post Mortem? Maadili Gani Ya Journalism Yanaruhusu Kila Siku Kuja na Same Story Angle?

Aina Hii Ya Uandishi Ndiyo Inayofanya Fani Ya Wanahabari Kudhaurika na Kupachikwa Majina Ya Kila Aina Kwa Makosa Ya Wajinga Kama Jambo Leo. Naomba sana Radhi Kwa Maneno Yangu Makali na Ya Kuchoma ila Ninaguswa Kwakuwa Kipele Kimempata Mkunaji.

JAMBO LEO MNATIA AIBU na MNA AGENDA GANI NA WATANZANIA WENZENU? Siku Zote Nitaendelea Kuyapenda Magazeti Haya: The Citizen na Mwananchi, The Guardian, Daily News, Raia Mwema, na Majira. Tumewachoka Jambo Leo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
kwa kweli hili gazeti mi mwenyewe huwa najiuliza limeshupalia sana habari za rwanda nafikiri kuna watu wanalitumia kwa maslahi yao naomba lichunguzwe linachochea uhusiano mbaya kati ya rwanda na tanzania
 
WanaJF Nimekuwa nafuatilia muda mrefu ufyukunuku wa hili Gazeti juu ya Kagame,kwa muda sasa limekuwa likiandika front page habari za Kagame zilizojaa fitna,majungu na story za hisiahisia tu,Nimekuwa nikijiuliza Malengo ya hili Gazeti ni nini juu ya Diplomasia yetu na Rwanda au nani yuko nyuma ya hili Gazeti?Tumeshuhudia Ikulu wakikerwa na Magazeti ya Rwanda yanayoandika hisiahisia zisizo na ukweli juu ya Rais Kikwete vipi kuhusu Jambo leo?

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Kwani unaona wanachosema jambo leo ni uongo kuhusu Kagame na serikali yake, au na wewe ni ukoo wa kagame unaoishi Tz ?. Wewe kama una hoja juu ya uongo unaoandikwa na jambo leo kuhusu kagame na serikali yake utuambie, sio kutuletea ukagame type hapa!.
 
WanaJF Nimekuwa nafuatilia muda mrefu ufyukunuku wa hili Gazeti juu ya Kagame,kwa muda sasa limekuwa likiandika front page habari za Kagame zilizojaa fitna,majungu na story za hisiahisia tu,Nimekuwa nikijiuliza Malengo ya hili Gazeti ni nini juu ya Diplomasia yetu na Rwanda au nani yuko nyuma ya hili Gazeti?Tumeshuhudia Ikulu wakikerwa na Magazeti ya Rwanda yanayoandika hisiahisia zisizo na ukweli juu ya Rais Kikwete vipi kuhusu Jambo leo?

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

wakuu sio jambo leo ni mtanzania karibu kila siku lazima liwe na heading ya kagame hadi kero
 
Naamini wengine si watanzania. Anzeni kuhoji kinachoganywa na news of rwanda. Haiwezekani rais wetu na nchi yetu tutukanwe, halafu tukae kimya. Balozi wa rwanda kama kweli ni mkweli, alikemee gazeri lake kwanza. Press ya tanzania inachekwa sana kwa kutomshughulikia pk na wafuasi wake. Nawaunga mkono jambo leo.
 
Master Legendary

LInafanya kazi nzuri kuiibu propaganda za Kagame pamoja na kuwa miimi ni hasimu wa serikali ya Kikwetekwa hli nawaunga mkono Kagame ni mbabe anaejifanya yeye na kanchi kake finyu ni superpower wenye ukanda wetu.

Hatuhitaji Rwanda hata tukiwa bila mahusiano na Rwanda tuko fine. Hongera Jambo Leo
 
Last edited by a moderator:
My Take kama Mh Rais wetu katuma ujumbe kupitia kwa Mh Waziri Prof Mwandosya sioni kwa nini kuendelea na huu uchochezi wa magazeti. Jambo Leo na Mtanzania ni vema waonywe jamani choko choko hizo ndio hizaa vita chonde chonde.
 
mkikemea jamboleo,mkemee na new times rwanda la rwanda pia,nalo limejaa umbea na uzushi tu.ndio itakuwa fair game!
 
waandike tu wao si wameanza, nashauri magazeti mengine yote yaandike habari hizo na achorwe tu huyo PaKa.
 
My Take kama Mh Rais wetu katuma ujumbe kupitia kwa Mh Waziri Prof Mwandosya sioni kwa nini kuendelea na huu uchochezi wa magazeti. Jambo Leo na Mtanzania ni vema waonywe jamani choko choko hizo ndio hizaa vita chonde chonde.

Sisi ndo tunaanza sasa mpaka huyu PaKa familia yake itamchukia.
 
Big up Jambo Leo..... leta mambo nawakubali sana.... Hivi ndivyo inastahili twende, wenyewe waandike ya kwao na sisi kupitia hili gazeti ambalo walau limeoneshwa na kukerwa na propaganda za hawa jirani zetu, na wengine waandike tuuuuu.

Vita yetu iwe ya magazetini tu lakini na sio ile yenyewe sawa eeee
 
Huyu asitupotezee muda wa uzalishaji, tuendelee kupammbana na mambo yetu binafsi akizi aende kuzimu amuulize idd amin habar ya Tz naona alikuwa mtoto enzi hizo.
 
Attachments

  • 1392660601380.jpg
    1392660601380.jpg
    5 KB · Views: 2,508
Kiukweli gazeti linajaribu kujibu propaganda chafu za vyomba vysa habari vya Rwanda dhidi yetu.

Kiukweli huko Malawi na Rwanda vyombo vyao vinafanya propaganda chafu sana na hapa kwetu kimya
 
Back
Top Bottom