Mr_S
Senior Member
- Apr 2, 2022
- 108
- 89
Habari za saa hizi watumiaji wa mtandao wa jamii forums.
Leo nimekuja kuwaelimisha, kuwapa elimu ya bure juu ya suala ambalo limekuwa likipotoshwa sana katika jamii yetu na reflection ya upotoshaji wake unaonekana hapa katika mtandao wa JF.
Nianze kwa kuuliza, kwanini inaonekana kana kwamba kipimo cha wenzi wa ndoa kufanya ngono madhubuti (kuridhishana) ni kufanya kwa muda mrefu ? Au kufanya zaidi ya mzunguko mmoja ? (tumezoea kuita bao).
Ukilitazama hilo jambo kwa undani zaidi utagundua kwamba hilo (ngono ya muda mrefu) halina uhusiano wowote na kuridhishana. Kumridhisha mume/mke wako ni jambo la kihisia zaidi kuliko muda (au wingi wa mabao). Ni rahisi sana kuridhishana ikiwa kuna upendo kati yenu na huenda isichukue zaidi ya dakika 12 kutokana na uwepo wa utayari wa kisaikolojia kwa pande zote mbili.
Ukiona unalazimika kufanya tendo na mwanamke kwa muda mrefu SANA ili kumridhisha basi unapaswa kutambua kwamba kuna mahali kuna tatizo. Yaweza kusababishwa na mambo mengi sana lakini kubwa nililoliona ni kitokuwepo kwa maandalizi mazuri kabla ya tendo lenyewe. Ninapozungumzia maandalizi simaanishi foreplay, namaanisha maelewano/mazungumzo ya kabla ya tendo lenyewe. Hisia miongoni mwa wenzi wa ndoa.
Haiwezekani kwamba siku nzima mnagombana ndani ya nyumba halafu mnataka baadae mkikutana mridhishane, hilo ni jambo gumu sana na litapelekea kufanya kwa muda mrefu sana mkiamini kwamba hilo litasaidia lakini tumeona impact yake ni nini: ku-fake kufika kileleni. Kwahiyo jambo muhimu kabisa ni uwepo wa maelewano na kuzungumza lugha inayofanana ndani ya nyumba ili isipelekee mwenzi wa ndoa kuwa na mawazo hasi wakati wa tendo au kabla ya tendo la ndoa kwa sababu hilo litaathiri kwa kiasi kikubwa kuridhishana miongoni mwa wanandoa.
Ngono madhubuti haina haja ya kuchukua muda mrefu sana ili kila mshiriki aridhike. Kama hisia zipo dakika 15 ni nyingi sana. Tofauti na hapo, jaribu kutafuta tatizo lipo wapi.
Ngono madhubuti inajengwa kisaikolojia kwa uwepo wa mawazo chanya na maelewano miongoni mwa wenzi wa ndoa. Kama hakuna mawazo chanya, hakuna uelekeo wa kufanya tendo la ndoa kwa nia njema.
Naomba niishie hapa maana najaribu kadri niwezavyo nieleze hili jambo kwa ufupi zaidi. Kama utapingana na nnachokieleza basi kuna sehemu hujanielewa ila kama umenielewa naimani itakusaidia kuondoa mawazo potofu kuhusu kuridhika kingono.