Jambo hili nililoshuhudia kwa Wanandoa hawa sijaelewa kama limechagizwa na mapenzi au heshima

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Wasalamu Wanajamvi...

Kweli kaa kwenye nyumba za kupanga uone mengi. Leo kuna jambo nimeliona nikashindwa kuelewa kama limetokea kwa sababu ya heshima au kwasababu ya mapenzi yaliyopo kwa Wapenzi hawa

Majira ya saa moja jioni nikiwa nimerejea kwenye mizunguko yangu ikabidi nikae nje ya nyumba yetu nipunge upepo kidogo kabla ya kuingia ndani. Nyumba yetu tunakaa wapangaji wengi kidogo na tunatumia mabafu ya nje. Katika nyumba hii kuna Wapangaji wapya ambapo ni Mwanaume na Mwanamke (Kwa mujibu wao wameona)

Basi nimekaa nje hapa nikaona Mwanamke ametoka na ndoo ya kisha akachota maji kutoka kwenye bomba la nje na kuyapeleka katika bafuni (bafu hilo la nje) na kisha akarudi ndani. Baada ya kama dakika 10 hiyo Mwanaume akatoka akiwa kavaa taulo na kwenda kuoga. Alipo maliza akatoka na ndoo akaacha nje ya mlango wa bafu, baada ya muda Mwanamke akaja na kuichukua ile ndoo

Sasa hadi muda huu najiuliza Mwanamke alifanya vile kutokana na mapenzi mazito aliyonyo ana ni nini kingine au ni heshima tu ya mila za kwao. Maana ukiangalia bomba alipochota maji lipo njiani ukitoka kwenye chumba chao kwenda bafuni? Lakini cha zaidi Mwanaume aliacha ndoo bafuni na yeye akaja kuifuata

Wakuu nisaidie siku hizi bado wapo Wanawake wa namna hii?
 
Sijui ni nini? Nadhani wao ndiyo wajuao...

Kila mmoja anaweza kutafsiri kivingine ila kama wanayafurahia maisha yao nadhani ni vizuri kwao.

Wapo sema wachache saana. Wengine wanafanya lakini sio kutoka moyoni unakuta kuna jambo analitafuta.

Raha umpate anayefanya bila sababu...anafanya tu maana kajiskia kukufanyia. Ni sawa na wewe kumbeba mkeo unanweka kwenye bath tub na kisha kumrudisha chumbani na kumpaka mafuta.
 
Mimi naona kuna kautemi fulani baina yao. Mwanaume hata kurudi na ndoo ndani kashindwa eti Mwanamke anaifuata.

Hivi kama Mwanamke anafanya kwa moyo Mwanaume hutakiwi hata kujiongeza kidogo?
 
Kabla ya hizi elimu tulikuwa na majukumu yetu kabisa wanaume na wanawake.

Zimekunja zimetuchanganya...tulibaki sio uzungu sio uafrika hakuna mfumo tuufuatao.

Mimi kwangu sio utemi maadamu mwanamke hachukii anakiona anachokifanya ni moja ya jukumu lake...ni kheri.
 
Kama nimekuelewa vema ni kwamba maisha ya zamani ambao elimu ilikuwa hakuna (au ilikuwepo chache) yalikuwa mazuri yaliyooka kabisa

Na kwa namna moja au nyingine Wanawake walifundwa kumtunza Mwanaume kama mfalme
 
Ni kwamba mwanamke huwa anajisikia fahari kumhudumia mume wake...hakuna cha mfumo dume au unyanyasaji,ni upendo tu..

Mie nilipoowa niliendelea kujifulia nguo zangu,nikaendelea kufanya usafi wa ndani na nje ya nyumba hadi chooni....akawa ananizuia ili afanye yeye lakini hakufanikiwa,nilishitakiwa kwa wazee kwamba anakosa fursa ya kunihudumia, ilinibidi nikasimishe madaraka hdi leo mie nina kazi moja tu hapo nyumbani...chumbani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui ni nini? Nadhani wao ndiyo wajuao...

Kila mmoja anaweza kutafsiri kivingine ila kama wanayafurahia maisha yao nadhani ni vizuri kwao.

Wapo sema wachache saana. Wengine wanafanya lakini sio kutoka moyoni unakuta kuna jambo analitafuta.

Raha umpate anayefanya bila sababu...anafanya tu maana kajiskia kukufanyia. Ni sawa na wewe kumbeba mkeo unanweka kwenye bath tub na kisha kumrudisha chumbani na kumpaka mafuta.
Bath tube kwenye nyumba ya kupanga inatoka wapi ?
 
Nadhani hujaoa kwa sababu hukusema unafanyaje kwako. Sasa; chunguza ka huyo mwanamke ni kabila gani na weye uende kuoa huko kwao/kabila hilo. Yapo makabila na mila zao. Mfano; Mkurya usipomtandika kwa mpini wa jembe hadi mkono uvunjike angalao mara moja kabla hamjapata mtoto wa pili kwake anajua una kamchepuko na huna mapenzi naye. Ukifanya mchezo anarudi kwao.
Mpare hata umkune vipi lazima awe na mchepuko tu kwani mafiga matatu ndo ugali husongeka. Mchaga akipata mtoto wa kiume, angalia sana usimuonyeshe mafanikio. Kukuondoa kwake sio shida ili mtoto aje kuzikuta pesa nyumbani. Na mnyaturu hata umfanye nini lazima aende kijijini kwao kupata vijana 2 wa kukusaidia majukumu ya kitandani.
Mchunguze huyu mama, ni kabila gani ukaoe huko ili uwekewe maji bafuni. Swali; wadhani nnani hutandika kitanda chao??
 
Wasalamu Wanajamvi...

Kweli kaa kwenye nyumba za kupanga uone mengi. Leo kuna jambo nimeliona nikashindwa kuelewa kama limetokea kwa sababu ya heshima au kwasababu ya mapenzi yaliyopo kwa Wapenzi hawa

Majira ya saa moja jioni nikiwa nimerejea kwenye mizunguko yangu ikabidi nikae nje ya nyumba yetu nipunge upepo kidogo kabla ya kuingia ndani. Nyumba yetu tunakaa wapangaji wengi kidogo na tunatumia mabafu ya nje. Katika nyumba hii kuna Wapangaji wapya ambapo ni Mwanaume na Mwanamke (Kwa mujibu wao wameona)

Basi nimekaa nje hapa nikaona Mwanamke ametoka na ndoo ya kisha akachota maji kutoka kwenye bomba la nje na kuyapeleka katika bafuni (bafu hilo la nje) na kisha akarudi ndani. Baada ya kama dakika 10 hiyo Mwanaume akatoka akiwa kavaa taulo na kwenda kuoga. Alipo maliza akatoka na ndoo akaacha nje ya mlango wa bafu, baada ya muda Mwanamke akaja na kuichukua ile ndoo

Sasa hadi muda huu najiuliza Mwanamke alifanya vile kutokana na mapenzi mazito aliyonyo ana ni nini kingine au ni heshima tu ya mila za kwao. Maana ukiangalia bomba alipochota maji lipo njiani ukitoka kwenye chumba chao kwenda bafuni? Lakini cha zaidi Mwanaume aliacha ndoo bafuni na yeye akaja kuifuata

Wakuu nisaidie siku hizi bado wapo Wanawake wa namna hii?
We jamaa bhana

Mzee hio ndio maana ya kujenga familia.Kuna wakati inabidi mke wako akuogeshe na kuna wakati inabidi wewe umuogeshi ila jambo la muhimu ni kwamba wanafurahia mapenzi yao,Mume anabembelezwa na mke anadkezwa.Usione wivu.
 
Back
Top Bottom