Jambo hili limeshawahi kutokea shule nyingine?

Jambo hili limeshawahi kutokea shule nyingine?

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Posts
27,972
Reaction score
35,197
Wadau wa elimu poleni na majukumu. Hivi imeshawahi kutokea shule nyingine wanafunzi wamemaliza kidato cha nne, matokeo yametoka halafu wazazi wanaitwa kwenye kikao cha wazazi na wanafunzi waliomaliza shule hiyo?

Huu hapa ni wito wa kikao cha wazazi kutoka Shule ya Alliance Girls Mwanza:

Ndugu mzazi wa mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne mwaka jana 2017 na matokeo kutoka mwaka huu 2018 Alliance Girls wote waliofanya mtihani kwa kituo cha Nganza ns Rock Army tunawatangazia kikao cha wazazi na wanafunzi kwa vituo hivyo kufika tarehe 18/2/2018 Jumapili saa tatu kamili asubuhi, kikao hicho kitafanyikia Alliance Primary, kuna taarifa muhimu sana fika bila kukosa, By Mkuu wa Shule Alliance Girls.

Tushirikishane
 
Huko ni kanda ya ziwa kuna ahueni flani huenda wazazi wanaitiwa ada waende tu.
 
Duuu! Hii mpya sijawah sikia mm ! But kama uko karbu na shule ,fika kawasikilize!
 
Kama mwanao amepata matokeo mazuri wewe nenda, unaweza kujikuta umepata ofa ya kulipiwa ada ya kidato cha tano na sita
 
Mkuu Uzalendo Installer unajua shida ni hali ya "vyuma vilivyokaza" hivi kweli wanamnyanyua mzazi na mwanae kutoka Songea kuja Mwanza kwenye kikao!! kuna gharama za usafiri, hoteli na mengineyo. enewei ushauri wako uko vizuri ndugu yangu
Kama huwezi kwenda, kaa zako nyumbani na usubirie feedback ya kikao.

Watanzania tunapenda sana kulalamika.
 
Huku pia wilaya ya Kilolo, Iringa, baada ya matokeo kutoka yalikuwa mabovu sana wazazi waliitwa. Wakafafanuliwa kwa nini matokeo yamekuwa mabovu, mojawapo ya sababu ni wazazi kupuuzia kuchangia chakula shuleni kwa kisingizio elimu bure.
 
Kama mwanao amepata matokeo mazuri wewe nenda, unaweza kujikuta umepata ofa ya kulipiwa ada ya kidato cha tano na sita
Mkuu duttu.e ni wazazi wote. Halafu hiyo shule wanafunzi wengi walipata Division one na two wanafunzi 2 tu ndio walipata division 3 kwa kituo cha Nganza sasa atawapa offer wote hao!!!
 
Huku pia wilaya ya Kilolo, Iringa, baada ya matokeo kutoka yalikuwa mabovu sana wazazi waliitwa. Wakafafanuliwa kwa nini matokeo yamekuwa mabovu, mojawapo ya sababu ni wazazi kupuuzia kuchangia chakula shuleni kwa kisingizio elimu bure.
Sasa ni kinyume maana hii shule matokeo yalikuwa mazuri sana. ni shule ya binafsi sio ya serikali
 
Mnaitwa ili wakaipigie promo shule yao mbele yenu.
Kuna wale walofanya vizuri zaidi watapewa zawadi huku mkishuhudia. Lengo ni kukuza na kuitangaza shule yao kupitia nyie, hii huwa tunaiita "word of mouth marketing" maana mkitoka hapo bila shaka mtakwenda kuitangaza hiyo shule kwa watu wanaowazunguka.
Ushauri: Kwa kuwa mwanao kasha hitimu na uko mbali si muhimu sana kuhudhuria hicho kikao maana hakutokuwa na jipya zaidi ya kukushawishi upeleke mtoto mwingine hapo kwa kuwa shule imefanya vizuri.
Kama mwanao kawa best zaidi ya wenzie mpe support akahudhurie hicho kikao nakuhakikishia hatorudi bila zawadi kwa kile alichokifanya.
 
Pamoja mkuu
Kama wewe ni mkristu, nikutakie mfungo mwema utakao anza kesho, kama sio mkristu basi nikuombee kila la kheri katika maisha yako yote. Barikiwa mkuu
 
Mnaitwa ili wakaipigie promo shule yao mbele yenu.
Kuna wale walofanya vizuri zaidi watapewa zawadi huku mkishuhudia. Lengo ni kukuza na kuitangaza shule yao kupitia nyie, hii huwa tunaiita "word of mouth marketing" maana mkitoka hapo bila shaka mtakwenda kuitangaza hiyo shule kwa watu wanaowazunguka.
Ushauri: Kwa kuwa mwanao kasha hitimu na uko mbali si muhimu sana kuhudhuria hicho kikao maana hakutokuwa na jipya zaidi ya kukushawishi upeleke mtoto mwingine hapo kwa kuwa shule imefanya vizuri.
Kama mwanao kawa best zaidi ya wenzie mpe support akahudhurie hicho kikao nakuhakikishia hatorudi bila zawadi kwa kile alichokifanya.
Ahsante sana mkuu expedition. Ila sasa kama ni promo wakiwaita wazazi halafu wakajua ilikuwa ni promo tu sio kwamba ndio "watawaudhi"?
 
Back
Top Bottom