Jambo CHADEMA kukataa kuhamia Dodoma

Mimi sijaona galama kwa upande wa chadema bora wangelalamika chama cha cuf , kwasababu cuf wanayo majengo ya ofisi , chadema wao ni wapangaji kuhama ni dakika tu kodi ikiisha wanahama
Cuf wana jengo (Wanalomiliki) la ofisi wapi?
 
..makao makuu ya nchi kuwa Dodoma haimaanishi kuwa kila taasisi ya serekali au binafsi ni lazima zihamie huko.

..tunayo TANZANIA ATOMIC ENERGY COMMISSION ni taasisi ya serekali lakini makao yake makuu yako ARUSHA.
 
Dodoma ni mji mtakatifu kwa Watanzania.Chonde Chonde hatutaki NAJSI
 
Hata kukaa karibu tu na mbaya wako ni gharama kwani hata mwanasheria Mwandamizi wa Chama alipigwa risasi Dodoma...mji Mkuu. Kwa hiyo gharama si lazima fedha wakati wote bali maisha ni gharama kubwa zaidi.
 
Dodoma ni makao ya ccm. Uamuzi wa kuhamia Dodoma ulifanywa na TANU hivyo haukua uamuzi wa Jamhuri ya Muungano kwani wakati huo Zanzibar ilikua chini ya ASP.
Hivo Mji mkuu ni Dar es salaam na Makao ya ccm yapo Dodoma. Nguvu inayo tumika haina tija kwa Muungano
 
Hii ni dunia kijiji, enzi za kidijitali, sio lazima kurundikana pale jangwani Dodoma!
 
Kuhamia dodoma ni suala mtambuka....muda utaamua .....87% mzunguko wa pesa na makusanyo yote yapo Dar....Dodoma aende Rais akajifiche na wizara zake avakize TRA....BoT Wizara Fedha....Mipango wengine waende ......ila uchizi kukomaa Dom uchumi wote unauacha dar
 
Kwani lazima tuhamie Dodoma?
Mfano Act -wazalendo katiba yetu inasema wazi kuwa makao makuu yapo Dar es salam na kuna ofisi ndogo za makao makuu huko Mwanza na Zanzibar .Sasa tuhamie Dodoma ili tuvunje katiba zetu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…