Jambazi ‘kinda’ afunga mtaa

Jambazi ‘kinda’ afunga mtaa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
MTOTO anayesadikiwa kuwa na umri kati ya miaka 15-17 amefunga Mtaa wa Mecco, Kata ya Nyakato wilayani Nyamagana, Mwanza kwa kupiga risasi hewani na kusababisha taharuki kubwa kwa wafanyabiashara na Wananchi.

Tukio la kijana huyo ‘kufunga mtaa’ limetokea usiku wa jana saa 1:45 katika Mtaa wa Mecco stendi, baada ya (kijana) huyo kutaka kupora katika duka moja linalouza mtungi ya gesi na vifaa vingine.

Hata hivyo, katika mapambano ya wawili hao, kijana huyo alianza kupiga kelele zilizosikika, ‘niachieni, niachie’ huku mfannyakazi wa duka hilo akiomba omba msaada kwa watu waliokuwa karibu na duka hilo.

Baada ya watu kufika huku mfanyakazi wa duka hilo, akiita ‘mwizi mwizi,’ watu walifika na kumshika kijana huyo.

Kijana huyo aliwaponyoka na kutoa silaha iliyokuwa kwenye begi na kupiga risasi moja hewani kuwatawanya watu waliokuwa eneo hilo.

Pia baada ya kijana huyo kupiga risasi hiyo, gari ndogo nyeupe ilifika na kumchukua na kutokomea kusikojulikana, kitendo hicho kilisababisha wananchi wa eneo hilo kupigwa butwaa.

Daud Machota, mmoja wa Wananchi wa eneo hilo amesema kuwa, vitendo vya uhalifu katika eneo hilo vimeanza kutishia amani kwani kumesababisha watu wengi kulala mapema.

“Kwanza mimi ninachoshangaa inakuaje mtoto mdogo wa miaka 15 – 17 anashika silaha na kupiga risasi hewani, labda hawa watoto wanaweza wakawa wamefunzwa mafunzo ya kigaidi, haiwezekani kwa umri wake kufanya hivyo,” amesema Machota.

Machota amesema kuwa, kijana huyo alifanikiwa kuchukua kiasi cha Sh. 40, 000 kwenye duka hilo, huku akidai kwamba uhalifu huo unasababishwa na ugumu wa maisha unaonekana kuwagusa watu wengi.

Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza na Naibu Kamishna wa Polisi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akidai kuwa, askari walikuta katika eneo la tukio begi na shati moja.

“Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika uhalifu huo, tunaendelea na uchunguzi kuwakamata watu wanaofanya vitendo hivyo, ilipigwa risasi moja hewani,” amesema Msangi.

Vitendo vya uhalifu wa kutumia silaha za moto katika kipindi cha hivi karibuni, vimeshamiri jijini humo na kusababisha wananchi na wafanyabiashara wa maduka, kuishi kwa hofu.

Tarehe 31 Novemba mwaka huu matukio mawili ya uhalifu wa kutumia silaha za moto yalifanyika kwa wakati tofauti na kusababisha watu wawili kujeruhiwa na kuporwa fedha kiasi cha Sh. 1.2 Milioni katika Mgahawa wa The Dinners.

Kashamiri kwa matukio hayo kumesababisha baadhi ya watu jijini humo kulaumu vyombo vya usalama kwa kushindwa kudhibiti hali hiyo.
 
Wanaume wa Dar naona wamefurahi
Maana wamepata kisingizio.
Kisingizio gan bwana na wakat mtu mmemshika anawaponyoka ..mngemfata bas alipopiga hio risas hewani,
Wanaume wa dar tuko vizuri mumeona tulichofanya uwanja wa taifa mbele ya mkulu...sisi ndo makomandoo bwana
hicho kitoto kingekua kweny himaya yetu tungekapa pigo moja sehem kangelala na kuzindukia polisi
 
Kisingizio gan bwana na wakat mtu mmemshika anawaponyoka ..mngemfata bas alipopiga hio risas hewani,
Wanaume wa dar tuko vizuri mumeona tulichofanya uwanja wa taifa mbele ya mkulu...sisi ndo makomandoo bwana
hicho kitoto kingekua kweny himaya yetu tungekapa pigo moja sehem kangelala na kuzindukia polisi
Sawa komando muogopa panya road.
 
taarifa za kipolisi zina utata sana.

.. walikuta shati na begi moja... na ilipigwa risasi moja...


je waliokota ganda la risasi ? na je bunduki gani ilitumika?

polisi waongeze uchunguzi ktk mifumo ya DNA na alama za vidole, maana kupitia hilo shati na huo mkoba, kwa nchi zilizoendelea ni rahisi kumpata mhalifu
 
Hicho kipaji ni hazina kwa taifa. Nashauri dogo atafutwe ili apewe mafunzo zaidi labda anaweza kuwa kama akina RAMBO baadae
 
Sasa wanaume wa Dar wamepata kisingizio
Hatimaye na Wasukuma wa Mwanza wameonyeshwa kutikiswa na "Panya Road",hiyo mitaa wanakaa Wakurya wengi sana,yaani nao walikimbia?Kweli hiki kizazi cha watu waoga sana hiki

Haya mambo huanza hivihivi;watoto wanamilikishwa silaha na wanaanza kuingia mitaani;na inakuwa ngumu kumkamata na kumshuku,sababu ya utoto wake.

Hata hapo Nyakato ukisoma maelezo,walishindwa kumkamata sbb ya "bumbuwazi";Hii ndio mbinu aliitumia Foday Saybana Sankoh kule Siera Leone,alitanguliza watoto mbele,aliwafunza kupiga na kuuwa bila kutishia.

Ilikuwa mpaka ujue huyu ni mtoto muasi,basi ameshauwa watu kumi au 20.Si jambo la kupuuzia,vyombo vya usalama vianze kuchunguza mazingira ya "mafunzo" ya hawa watoto...Ni hatari sana sana kwa usalama wa nchi.
 
Makamu was Rais kasema tuwe wavumilivu kwa ugumu wa maisha, ni kipindi cha mpito kunyoosha nchi. Changamoto za ujambazi nazo zitaisha tu kunyoosha nchi kukiisha.

KADA
Hivyo vitoto itakuwa ndio vinavyofundishwa ugaidi. Ila mabosi wao wanafaidika na wizi wao, vyenyewe vinaambiwa "tunampigania Allah"sijui Mungu gani anayeshawishi waumini wawe majambazi ili kumlinda huyo Allah! Ni ajabu sana.
 
Back
Top Bottom