Mkuu kwanza pole, pili usipende kuandika kwa kulialia namna hii, unapoonesha dhahili kwamba umefikwa na maji ya shingo unawapa advantage ya kukuchinjia baharini hao unaotaka "wakusaidie"! Kikubwa wewe ni kwamba una biashara zako zitaje ziko wapi na zinaendeleaje ili uvutie mtu kuwekeza kwenye hizo biashara akiwa na hakika kuwa pesa yake itarudi, ukiona mkopeshaji anafurahia kuuza dhamana aliyoweka mteja ujue huyo ni mwizi. Hayo unayopitia ni mapito tu mkuu, komaa. BTW, hiyo kampuni isiyolipa mishahara mpaka wasaini mikataba kwa miezi minne ni kampuni gani?!!! Kuna watu ambao ukiwaona sasa ukaambiwa wamepitia mazito kuliko hivyo vijichangamoto vyako huwezi amini, usilie sana bana, wewe unaaford mpaka kulipia bundle ya kuingia JF!