Jamani watanzania

Jamani watanzania

akukwethi

New Member
Joined
Dec 14, 2012
Posts
1
Reaction score
0
Ni wajibu,jukumu na kazi yetu kuliombea taifa letu amani ya kudumu kwani,amani ndio chombo pekee
kinachoweza kusaidia maendeleo ya taifa letu.Amani tulionayo ni ya kihistoria,lakini tukithubutu
kuipoteza itatuchukua muda sana kuirudisha hasa kwa gharama nyingi pia.Tazama,Egypt,Syria,Libya
Tunisai pia.Lakini pia hii haina maana tusiongee,kukemea na kuwawajibisha viongozi wetu wazembe,
wala rushwa,mafisadi,na wanaojilimbikizia mali wakati watanzania wa kawaida kamma bibi yangu kule
kijijini wanaishi maisha ya matumaini tu.

Rai yangu kwa wasomi.tutumie nafasi yetu ndogo au kubwa tuliyonayo kuwaelimisha na kuwaamsha
watanzania kutambua na kutetea haki zao.Taifa hii ni la kwetu wote,bila kujali chama,rangi na hata
kabila.

mungu ibariki Tanzani.
 
tatizo kubwa la watanzania ni kulalamika hata kama mnajua mchawi wenu ni ccm mwisho mnampa kula za kishindo au mtu baada ya kulalamika anasema ana unga hoja kwa asilimia mia
 
Back
Top Bottom