Jamani wanaume wasomi mna nini?

Jamani wanaume wasomi mna nini?

Queen Horse

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2013
Posts
414
Reaction score
317
Mwidiwee.. Namahorooo wana JF
Bado Niko najiuliza maswali juu ya wanaume wasomi hasa hasa kuanzia level ya masters, PhD hadi kule kwenye ukuta ulioandikwa elimu tena basi kwanini wengi wao wanakuwa wanatabia ya kupenda kuwadharau wake zao hasa ukikuta wamewapita kiwango cha elimu mfano mke ana diploma yake ya ualimu au digrii yake ya course ya kuchechemea.

Naongea hivi kwa experience kwa sababu nimekutana na kesi kama tatu zenye kufanana lakini hii ya nne too much.
Haya yamemkuta shosty wangu mmoja hivi mwenye degree yake ya sociology na GPA ya kuchechemea na mchuchu wake mwenye PHD ya mambo ya planning.

Sikutaka kuchukua details nyingi kwa sababu elimu yake hainisaidii wala kuniletea hela ya ugali
Back to the topic, shosty kipindi kabla hajaolewa mapenzi yamechanua kama maua ya saa nne alikuwa anajisifia kweli na mchuchu wake mara wanaume waliosoma sana waelewa sana, Mara mimi degree holder wenzangu nimpeleke wapi.

Maneno kibao kudharau waume za wenzie na kujifanya wa kwake ndio bora sana kama tunavyojua masikini akipata masaburi hulia mbwata, sie tena wenye vicertificate holder vyetu tukawa tuna zip our mouth shut tunajipa moyo maisha hayapimwi kwa wingi Wa makaratasi ya vyeti.

Basi bwana Shoga yule mwaka juzi kaolewa kwa shangwe na vigelele na sisi mashabiki kama kawa tupo mbele kumpa kampani, ndoa sasa ina miaka mitatu ndo anaona chungu ya ndoa mkaka kawa na dharau kila analoliongea mkewe sharti liwe prove intelectually with high thinking capacity, akikosea kidogo matusi najuta kukuoa kilaza mkubwa wewe degree yenyewe umeipata kwa bahati, mara mimi siwezi kukaa na kujadili maisha na watu ambao sio ma critical thinker, mara sasa utanishauri nini wewe na akili yako ndogo na maneno mengine ya maudhi.

Sasa juzi ndo ilikuwa komesha shoga kaingiza loss katika biashara ya familia ambayo mkaguzi ni Mr.

Alioona junijulai alitukanwa mpaka aliiona ardhi ngumu kuikanyaga kupooza machungu kabaki anatupigia simu mashoga zake kutupa mkasa na maneno ya najuuta kibao nikamwambia shoga vumilia ndo ndoa ilivyo vumilianeni kila mtu ana kasoro zake.

Back to my question: kwani mahusiano yanahitaji akili ya kukariri vitabu?

Kama mnaona vitabu ni mali si mngekaa single mkaendelea kukariri.

Najua wengi mko humu wenye hizo tabia acheni dharau ishini na familia zetu kwa amani, kama mkeo ana weakness mu encourage aweze vile unavyotaka kumnyanyasa kisaikolojia sio vizuri.

Unasababishia makovu moyoni ambayo inawezekana hata we huyajui.
 
kama naona jamaa anavo mkoromea huyo bibie. teh teh teh....
but mchiz anazingua habari hayo sio mapenz definitely
 
kama naona jamaa anavo mkoromea huyo bibie. teh teh teh....
but mchiz anazingua habari hayo sio mapenz definitely

Nakwambia acha bibie mpaka kaloose weight chezea manyanyaso ya kauli wewe.. Anakula vizuri, analala vizuri, usafiri upo ila akimfikiria mumewe nguvu zinaishaa anakosa hata amani ya kumwambia mambo yanayomuhusu
 
sa kama amekosea asiambiwe, umeleta hasara kwenye biashara unataka nikubembeleze tena.... hiyo kitu haipo, tusipokuwa wakali mtatupanda kichwani, lazima upige biti ata kidogo!!! Ilitakiwa ampe na vibao hata viwili kabisa sio maneno matupu
 
Jamaa kakosea sana ila alikosea zaidi na zaidi katika kuoa. Kimisingi huyo bwana anapata tabu sana kuishi na mtu ambaye intellectually yuko chini sana kulinganisha na yeye. Kwa mfano katika hali ya kawaida tu unaweza kuacha kujadiliana na mtu kwa kugundua kwamba uwezo wake wa kuchambua mambo ni mdogo au saa nyingine unaweza kuvumilia na kujaribu kujiweka katika level ya huyo mtu. Sasa fikiria kama unapaswa kufanya hivyo kila siku na mtu huyo huyo!!! Ni wazi baada ya kujitahidi kwa miaka 3 kuna mahali itafika lazima ushindwe.

Hii mara nyingi inatokea kwa sababu mwanzo mwanaume anaweza kugubikwa na mapenzi moto moto na pia wanakuwa hawapati muda wa kukaa pamoja kwa muda mrefu. Zaidi mume anaweza kutegemea mke atakua kiakili na kimaarifa lakini kwa bahati mbaya inaweza isiwe hivyo kwa kuwa watu tunatofautiana uwezo. Kuna wengine hata ufanye vipi hawawezi kufika kiwango anachotamani mume. Sasa ukute mume anataka kujadili kuhusu uchumi wa Uingereza, Marekani, Tanzania na Brazil hapo anakuja na habari za GDP, PPP, per capita, FDI na habari za sekta za dhahabu, wese na wenzao, ukigeuka kidogo anataka kuzungumzia import/export tax, custom duties na visa issues. Hujakaa sawa anataka kuongelea U.S foreign policy in the middle east. Kabla hujajikuna vizuri anakuletea habari za investment and planning ukichanganya na expanding and dreaming big. Sasa kama ndoto zako ni kuishi kwenye nyumba ya vyumba vitatu na gari ya kutembelea lazima mambo yatakuzidi kimo sana. Na ukichanganya na tabia ya watz wengi tulivyo wavivu wa kujifunza mambo mapya ndio kabisa lazima uchemshe. Ndo hapo sasa mume anakuona kilaza bab kubwa. Lazima nyumba uione chungu.

Ila hata hivyo mimi huwa naona watu wanalazimisha mambo. Kuna siku niliwahi kusema maisha yanaweza kuwa magumu sana kama badala ya kutafuta mke unatafuta business partner. Inapofikia mahali huyo mke akashindwa kuwa business partner inakuwa shida kubwa sana.

Inabidi ifike mahali watu kama huyo jamaa inabidi wajue kuwa mke ni mke tu. Kuna majukumu yake kama mke kama anayaweza hayo basi inatosha. Ikitokea akaweza kusimamia na mambo mengine nje ya yale ya msingi na wajibu basi ni vizuri lakini kama hawezi basi si budi kumlazimisha asichokiweza.
 
Ngoja waje wenye Phd kama ya MCHUNGUZI HURU mimi hata darasa la nne sikuvuka kwahiyo mke wangu wala asiwaze saana labda ntasumbua tu aifundishe kuongea kimombo ili tuweze kuitana Bebi, switi, Dalingi, hani na mengineyo mengi ya kidhungu Aahahahhahah lol
 
kuna wakina dada wanabahati mbaya wanakutana na wanaume ambao 'selfish' hiyo ni shida mnao...yaani mtu mimi, mimi, hela zangu, mimi nimesoma, magari yangu, mimi utaniambia nini nimesoma..ukidate na mtu wa mmimi, mimi, mimi,mimi kimbia ufe...
 
"mkaka kawa na dharau kila analoliongea mkewe sharty liwe prove intelectually with high thinking capacity"

Daaaamn!, Hahaaaaa!, nashindwa hata kucheka!, wasomi tunawapenda but mh!, I would tell him to kiss my.....
 
Hii ni tabia binafsi, kama vile mtu kujikweza, kuwa mropokaji nk! Nadhani inaonekana kuwa "common" kwa sababu kwetu huku hii levo ya elimu ina watu wachache, kwa hivyo hujiona kama ni superior sana. Mbaya zaidi upatikanaji wake kwetu huku ni wa shida sana, lazima uaibishwe na kudharauliwa sana na supervisors. Inawafanya hawa ndugu zetu wawe wajinga, na mbaya zaidi ikiwa ni mwenye tabia ya kujikweza hali ndiyo inakuwa kama kilichopostiwa juu. Kwa wenzetu ni kawaida kuintaract na PhD holder bila hata kujua kama ana PhD. Kama ni lecturer anaweza ingia darasani akajitambulisha hata bila kujiita dokta. Huku kwetu, iache hiyo prefix kwenye assignment uone kimbembe chake!!!
Hizi ni tabia za watu tu, na ni aibu sana kumfanyia mwenza. Mke/mume ana heshima yake ambayo ni lazima mwenza ailinde. Katika makosa ni lazima muongee na kuelekezana, lakini si kuonesha dharau. Maisha ya pamoja ni mazuri sana kama kila mmoja anakua na amani na mwenzake.
 
Eti intelectual, unaweza kuta na intelectual yake hata DUDU haisimami, basi hasira zote zinaishia kumtukana binti wa watu. Mwanaume rijali humthamini mke wake na si kuleta darasa Nyumbani! hawa ndo wale wake zao wanadungwa na ma Houseboy sababu ya ujinga wa Mme
 
Umenikumbusha jamaa alikuwa anamrekebisha mkewe anamfokea yani wewe ni mbinafsi sana utasikia watoto wangu mara nyumbani kwangu kwani nini wewe mbinafsi hivyo? Wakati akiongea hivyo mkewe alikuwa anapekuapekuwa kabatini mume akamwambia tena ona mimi naongea wewe upo bizy tu unatafuta nini sasa uko kabatini mke akamjibu mumewe natafuta sidiria zetu ha ha ha ha .
kuna wakina dada wanabahati mbaya wanakutana na wanaume ambao 'selfish' hiyo ni shida mnao...yaani mtu mimi, mimi, hela zangu, mimi nimesoma, magari yangu, mimi utaniambia nini nimesoma..ukidate na mtu wa mmimi, mimi, mimi,mimi kimbia ufe...
 
Umenikumbusha jamaa alikuwa anamrekebisha mkewe anamfokea yani wewe ni mbinafsi sana utasikia watoto wangu mara nyumbani kwangu kwani nini wewe mbinafsi hivyo? Wakati akiongea hivyo mkewe alikuwa anapekuapekuwa kabatini mume akamwambia tena ona mimi naongea wewe upo bizy tu unatafuta nini sasa uko kabatini mke akamjibu mumewe natafuta sidiria zetu ha ha ha ha .
yah mkishakua wawili hamna cha mimi mimi mimi tena ni sisi sisi sisi
 
yaani ameingiza hasara then abembelezwe akuu...hakunaga jamani at the ci mnafisika kisa kuchekeana eti mapenzi wapi wwe even me.
 
Back
Top Bottom