Jamani wafanyakazi wa NSSF Ubungo wanaudhi

Jamani wafanyakazi wa NSSF Ubungo wanaudhi

Jamani, mnataka mwenzenu ajinyonge?

Konnie huu sio wakati wa kutishana, kwani nani asiyejua kuwa ukidinyana na mtu kihasara hasara kuna hatari ya kupata ngwengwe!!
 
Hao ndiyo NSSF, Hakuna uwajibikaji hata kidogo, kote ndiyo hivyohivyo, jeuri wanaipata ngazi ya juu ambayo huhakikisha kuwa watu huajiriwa kwa kauli mbiu "udini kwanza" ni moja ya taasisi ambazo huduma kwa mteja ni duni sana, WAMELEWA madaraka na wanasahau kuwa wanaowaweka hapo ni wanachama wa mfuko ambao wamekubali kuweka pesa zao hapo ili baadae ziwasaidie, NSSF hufikiri kuwa wanachama ni ombaomba ambao hawastahiri kuhudumiwa kwa kiwango cha juu. Huu udhaifu dawa yake ni wanachama kuamka na kukwepa kujiunga na mifuko ya namna hii ambayo huwafanya wanachama kuwa watumwa kwenye mali zao. Walikuwa wameficha Kadi yako ili pengine uwape chochote. Wananchi wawe macho na mfuko huu.

umenena mkuu ni kweli udini umetamalaki nssf.hao mashungi ubungo ni noma yanapenda sana kitu kidogo.hiyo ndo sera ya dau na nssf.vision yao ni kuongeza shungi sana
 
Wadau,
tangu NSSF imeagiza kubadilisha card za zamani kubadilishwa na kuwa smartcard, nimekuwa nafatilia smart card tangu mwezi wa october 2012, nikienda naambiwa nenda kwa mwajiri wako, nikienda kuuliza kwa mwajiri naambiwa haikuletwa.

niliamua kuvalia njuga ufatiliaji hasa baada ya kuacha kazi. Tangu mwezi january 2013 nikienda naambiwa njoo mwezi ujao, imeenda hivo mpaka ilipofika mwezi may nililalamikasaana mpaka wakaamua kuangalia kard imekwama wapi, ndipokuna dada akasema inabidi nipige picha upya nilifanya hivyo may wakaanza tena kunipiga tarehe wiki baada ya wiki, iliyopita alitaka kunirusha nirudi baad ya miezi miwili nilikuja juuu kama mbogo yule dada akapunguza muda akasema nije baada ya wiki ambayo ni ijumaa ya leo, kwa bahati nzuri niliwahi mda wa saa tisa alasiri nilitinga ofisini kwao nikiwa peke yangu hapakuwa na foleni.

Dada aliniangalia kama nyanya iliyooza, nikamuomba samahani "dada nimefata card yangu niliambiwa nije leo" dada bila hata kuniangalia usoni akanipiga tarehe eti " Njoo baada ya miezi miwili," nilikasirika nikamuomba nimuone mkubwa wao, kaka mmoja aliamua kuitafuta kard akaiona kama baada ya dakiki tano tu, akanikabidhi,,, humo ofosini anae fanya kazi kwa moyo ni huyo kaka tuuu wengine wanafanya kwa mood tu.

JAMANI MPAKA MTU ATISHIE KUPELEKA Malalamiko NGAZI ZA JUU NDIPO UHUDUMIWE??? Hiyo ni card tu je, mafao itakuaje???

Nadhani bado kuna wafanyakazi wazuri tu NSSF hata ngazi ya juu. Jaribu kumtafuta Benefits Administration Manager - Bwana Oigo. Ninaamini atakusaidia.
 
Ktk taasisi za uma zenye huduma mbovu NSSF UBUNGO wanaongoza wakifuatiwa na o'bay police then mwananyamala hospital.
 
Back
Top Bottom