Jamani wababa kulikoni?

mataka

JF-Expert Member
Feb 4, 2011
286
61
Hebu wana jf tuliongelee hili, kwa ushuhuda nilionao naona watoto wana mapenzi sana na mama zao kuliko baba. Hebu tuangalie mifano michache, nyimbo nyingi zinazoimbwa dedication ni kwa mama, watu wakipewa nafasi ya kutoa shukrani mara nyingi mama anatajwa tena bila kumuhusisha baba, juzi tuzo za kili wasanii wengi walidedicate tuzo kwa mama, tukiulizana hapa kati ya baba na mama nani unampenda wengi tutajibu ni mama. Mimi najiuliza kwa nini baba mara nyingi hana nafasi mioyoni mwetu? Jamani tatizo liko wapi?
 
Mama anakunyonyesha, anakutunza, anakujali kuliko baba, Lakini si kwamba Baba hapendi kuwa karibu kama Mama hapana anakuwa hana muda wala nafasi hiyo hawezi kukunyonyesha, hawezi kukuogesha, hawezi kukulisha chakula mara kwa mara, inaweza kutokea mara moja moja sana.
 
hii thread imerudiwa???

"Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako." ss anayemuheshimu mama peke yake amri ya 5 inajieleza!!!
 
Hii inatokana na kwamba mara nyingi mama ndie anayekuwa karib zaid na wanae kuliko baba nando maana hata mtoto anakuwa na ujasiri zaid wa kuexpress shida zake kwa mama kuliko baba.(kwa wapenz wa bios nafkiri mtakumbuka ya kwamba ma mjamzito anapojifungua huwa ana release homoni ambayo ina mwifluensi kuwa karib na mwanae)
 
hii thread imerudiwa???

"Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako." ss anayemuheshimu mama peke yake amri ya 5 inajieleza!!!
Ndio wote tunawaheshim ila from childhood kunyonyeshwa na mama kunatengeneza bond isiyovunjika milele
Mtoto akilia akipokewa na mama mtu hunyamaza compared to baba mtu (ukubwani tunafake love na kutumia ubongo ila utotoni ambako ni mahala pazuri pa kuonesha mama zaidi)
 
Mama mama mama mama huyoooooooooooooo!!!!
Mapenzi ya mama kwa mtoto ni makubwa sana, hushangai mama ananaweza akawa anateswa na baba hata kupigwa lkn haondoki kwa sababu ya watoto, anasema watoto wangu watateseka. Mama anavumilia mateso kwa sababu ya watoto wake.

Wakati mwanaume hata mke akifa leo miezi michache tu kashaoa. Dah mama kwa kweli akiwepo hata kama baba hayupo maisha yataenda. Lakini baba akishapata kamtu huko nje nyie hata hawakumbuki tena.

Dah mama mama...........
 
oneza hili wababa huchukia usumbufu/uharibifu wa watoto wakati wamama tunaupenda na watoto wanajua hili.Love us watoto as tunawapenda na kujitolea zaidi ya baba zenu
 
Ukiangalia kwa undani utakuta wote wale waliokuwa wantoa shukurani zao kuzielekeza kwa mama,historia ya maisha yao wamelelewa na mama tu,either baba amefariki au walitengana muda mrefu inaweza ikawa hata tangu ya utoto,kwa hiyo mapenzi waliyokuwa ni ya upande mmoja zaidi
 
Its simple akina mama wako karibu na watoto while sisi wababa ndo kimsingi tunatengeza UKARIBU wa hao akina mama na watoto wetu.
 
Tatizo kubwa la wa baba wengi ni kukwepa majukumu haswa ya kulea na kumwachia mzigo huo mama,pili wababa walio wengi hawatabiriki,na tatu mfumo dume
 
Wengine enzi tupo wadogo kumuona baba ni siku za wikendi tu, anarudi saa 7 usiku na kuondoka saa 11 alfajiri. Muda mwingi tulikuwa na mama!
 
Wengine hatujui hata upendo wa baba unafananaje. Lazima mapenzi yawe kwa mama tu.
 
Ukiangalia kwa undani utakuta wote wale waliokuwa wantoa shukurani zao kuzielekeza kwa mama,historia ya maisha yao wamelelewa na mama tu,either baba amefariki au walitengana muda mrefu inaweza ikawa hata tangu ya utoto,kwa hiyo mapenzi waliyokuwa ni ya upande mmoja zaidi

usikwepe ukweli wamama wanakuwa na mapenzi makubwa kwa watoto kuanzia utotoni mpaka utu uzima,ule ukaribu ni tofauti sana na wababa wavyouonyesha kwa watoto ingawa si kwamba wanaume wanakuwa hawana mapenzi na watoto ila nature inachukua nafasi zaidi,nampenda sana mama nikikumbuka alivyoangaika na sisi napata uchungu pia,lkn nampenda baba pia
 
Ukiangalia kwa undani utakuta wote wale waliokuwa wantoa shukurani zao kuzielekeza kwa mama,historia ya maisha yao wamelelewa na mama tu,either baba amefariki au walitengana muda mrefu inaweza ikawa hata tangu ya utoto,kwa hiyo mapenzi waliyokuwa ni ya upande mmoja zaidi

Na ni ukweli usiopingika kuwa kina baba wengi hawajali familia zao, vurugu, vioja na utovu wa nidhamu uliokithiri; hasa pale inapotokea baba ana nyumba ndogo,
 
Kuna mtoto wa jirani yangu alimwita kijana anaye waletea maziwa asubuhi baba
baba anaondoka nyumbani mtoto amelala anarudi mtoto amelala
Upendo kwa mama lazima
angalia mtetea na vifaranga vyake mvua ikinyesha ndani ya mbawa zake jogoo yuko wapi?
 
Mama anashinda na watoto nyumbani, wakati baba yupo viwanja!
Hivi hata vifaranga vya kuku hawamjui baba!
 
mamaa maaa maaaa uwezo wa kukulipa sina namwomba Mungu akupe baraka mamaa aa.

mara nyingi mama ndio anakuwa karibu na watoto, iwe mvua, masika, baridi au kiangazi, kuanzia mtoto anapotungwa tumboni uwa karibu na mwanae.
 
Hebu wana jf tuliongelee hili, kwa ushuhuda nilionao naona watoto wana mapenzi sana na mama zao kuliko baba. Hebu tuangalie mifano michache, nyimbo nyingi zinazoimbwa dedication ni kwa mama, watu wakipewa nafasi ya kutoa shukrani mara nyingi mama anatajwa tena bila kumuhusisha baba, juzi tuzo za kili wasanii wengi walidedicate tuzo kwa mama, tukiulizana hapa kati ya baba na mama nani unampenda wengi tutajibu ni mama. Mimi najiuliza kwa nini baba mara nyingi hana nafasi mioyoni mwetu? Jamani tatizo liko wapi?

Mama alinipa hifadhi ya kisiasa miezi tisa. Baada ya miezi tisa nikaja duniani. ilikuwa nikifumba macho nikiamka mama ananiangalia, nikilia anajua ninachotaka. Nilimnyima uhuru muda huo na baada ya mimi kutokea, baba ilikuwa anakuja jioni tuu. Love u sweet mama.
 
malizia hapo akiwa amejitwisha furushi la matunda na vyakula mbali na nguo ulizovikwa na chakula ulicholishwa mpaka umekuwa na kuitwa sharobaro! PAMBAF!
 
Hebu wana jf tuliongelee hili, kwa ushuhuda nilionao naona watoto wana mapenzi sana na mama zao kuliko baba. Hebu tuangalie mifano michache, nyimbo nyingi zinazoimbwa dedication ni kwa mama, watu wakipewa nafasi ya kutoa shukrani mara nyingi mama anatajwa tena bila kumuhusisha baba, juzi tuzo za kili wasanii wengi walidedicate tuzo kwa mama, tukiulizana hapa kati ya baba na mama nani unampenda wengi tutajibu ni mama. Mimi najiuliza kwa nini baba mara nyingi hana nafasi mioyoni mwetu? Jamani tatizo liko wapi?
Watoto wangu hawapo hivyo,mara nyingi hata ukija kwangu utasikia baba,,,,,,,,babaa haziiishi ndani yani jinsi gani watoto wangu wanavyoonyesha mapenzi yao kwangu,ila mara nyingi ni mtazamo wa mama kuwa mdomoni zaida umekaa ki nature tu.nadhani umenisoma,kwa maelezo zaidi ni PM
 
Back
Top Bottom