Jamani wa-Tanzania hawa.....!!!!

Nyundo_tz

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2009
Posts
640
Reaction score
21
Wadau, hili swala la kampuni ya Tanzanite 1 kunyanyasa wafanyakazi wao kule migodini Arusha lilishawahi kurushwa na ITV na serikali ikaahidi kulishughulikia. Cha ajabu leo asubuhi wakati nasikiliza BBC Swahili inaonekana unyanyasaji umeongezeka maradufu. Wafanyakazi wanapekuliwa na ajabu zaidi unyanyasaji huo unafanywa hadi kwa wanawake na bado wanataka kuleta machine ya X-ray itakayotumika kuwakagua wanapotoka mgodini. Mashine hizo zinaaminika zina madhara makubwa kwa binadamu. Cha kushangaza, mkuu wa polisi mkoani Arusha alipohojiwa na BBC akadai swala hilo ni la wakubwa, halimuhusu....

JE, TUTAFIKA...????
Wa Tanzania tutanyanyaswa hivyi mpaka lini na Wazungu ili hali wakubwa wanafumbia macho swala kama hili?
 
Dah inatisha na inasikitisha sana.
Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.
 
Hivyi mpaka lini Wazungu wataendelea kubebwa ili hali ndugu zetu wananyanyasika...!!!????
 
BBC akadai swala hilo ni la wakubwa, halimuhusu....

Can somebody tell me what that is supposed to mean?
 
Tunahitaji kiongozi jasiri kama rais Hugo Chavez bila hivyo tutachezewa hadi sehemu zetu za uzazi.
 
Nakumbuka Edger Maokola-Majogo akiwa Waziri wa Nishati na Madini aliunda tume ya kuchunguza unyanyasaji Mererani ripoti yake ikaishia makabatini na huenda imeshakufungiwa vitumbua, kama hiyo haitoshi Lowassa akiwa waziri mkuu naye aliunda tume kuchunguza manyanyaso ya Mererani ripoti yake nayo ikaishi kula vumbi katika mashubaka na pengine inatumika katika kuchapisha tiketi za daladala. Naamini wadanganyika wengi hawakumbuki haya inasikitisha mno.
 
hao wakubwa anaodai ni kina nani kama na yeye si mmoja wao??
Mie nadhani yeye ni mwakilishi wa hao wakubwa ....inabidi aanze kuchukua hatua mara moja!!
 
Acheni hiyo hata ulaya kuna makampuni mengine ukitoka kazini au kwenye maduka makubwa kuna vyombo vinajua kama umesogeza kitu.zipo mashine pia ukiingia kazini zinanote muda ulioingia,sio kama Bongo uingie saa mbili saa tatu kwa baadhi ya makampuni ni sawa tu ,uwe fisadi na kukomba mapesa kibao nisawa tu.,hiyo hatutafika popote .Na nchi yetu ingeongozwa na weupe mpaka leo Bongo ingekuwa kama kwa Mandela ,ukiachilia maswala mangine ya hawa weupe.
 
Tunahitaji kiongozi jasiri kama rais Hugo Chavez bila hivyo tutachezewa hadi sehemu zetu za uzazi.

Kama wanavyowashika shika dada Zetu huko Mererani kwa kisingizio wanawakagua wasitoke na mali...
 
Hivyi mpaka lini Wazungu wataendelea kubebwa ili hali ndugu zetu wananyanyasika...!!!????

Wananchi wenzangu huu tulionao ni ukoloni mamboleo, yaani unakuwa ruled out at a background bila wewe kujijua - huu ni hatari sana bora hata ule ukoloni wenyewe enzi za bakora. Sisi wenyewe ndiyo tunauendeleza kwa kuwa na mifumo mibovu, rushwa, ufisadi na tamaa za ajabu ajabu. lazima wazungu watufanye wanavyotaka.
 
haya mpka lini jamani????

viongozi wetu mbona wabinafsi kiasi hiki jamani????? watu wanakufa kule Mara, hawa wananyanyaswa huku....

hamuwezi kuchukua hatua za haraka only because mnanufaika ninyi na familia zenu.........

Tanzania nchi ya amani.......my foot
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…