Jamani utaratibu wa kutoa posa upoje

Jamani utaratibu wa kutoa posa upoje

mwekwa ntandu

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2019
Posts
1,530
Reaction score
3,777
Ni miezi kadhaa sasa tangu mwanamke niliyekuwa ninaishi nae kwa miaka saba na kubahatika kupata watoto 3 kufikia maamuzi ya kusema kila mmoja ashike hamsini zake kutokana na migogoro mbali mbali ndani ya familia.

Nilitumia ushawishi mkubwa kumuelewesha madhara ya uamuzi huo anaochukua LAKINI ILISHINDIKANA. Nimekaa karibu miezi mitano sasa nikijua mwenzangu atajirudi lakini inaonesha amedhamiria kuendelea na maisha yake, nami kutokana na upweke na stress nikaona isiwe tabu nikafanikiwa kuwa karibu na binti mmoja mbichi mtaani kwangu nikamweleza sera zangu akanielewa ila akawasiliana na wazazi wake nao hawakuwa na kipingamizi ila walinitaka kuleta POSA na wala wao hawahitaji masuala ya sherehe wala nini ni kiasi cha kuleta posa na kuchukua mke.

Nimekuja kwenu wajuzi wa mambo mnipe utaratibu wa kutoa posa maana mimi sina uzoefu huo kwa kuwa hata mwanamke wa kwanza tuliyeachana ilikuwa ni SOGEA TUISHI na tukadumu miaka 7.

ANGALIZO: Watu wa CCM naomba msikoment huu uzi maana hamchelewi kutukana badala ya kushauri mna stress, nahitaji wana chadema na wengine wasio na mlengo wa vyama ili nipate ushauri mzuri.
 
Inategemea unaongozwa na dini ipi.

Kama huna dini manake huna muongozo,kinachokuongoza ni nafsi yako itakavyoona.

Kama mkristo waulize wanachuoni wakikristo wa karibu yako.

Kama muislamu basi tafuta mshenga(mtu) akakupelekee hiyo posa.

Posa : ni kitu chochote kile kilichoambatana na ujumbe wa kuwa "kijana wetu fulani kampenda binti yenu hivyo tumeleta ombi hili tunaomba likubaliwe"
Hapo ujumbe huu unaweza kuuwasilisha ukiambatanisha na mkungu wa ndizi,au pesa au chochote kile

Lakini uzuri zaidi hiyo posa angalia uipeleke kwa kuangalia ile tamaduni ya watu husika unakoenda kuposa.
Sio wenzio wamezoea kupewa barua yenye pesa ndo wanahesabu posa,wewe unapeleka mkungu wa ndizi,angalia na tamaduni ya ukweni kwako kutarajiwa.
 
Sahihi, ila nadhani hata wakristu kwenye kutoa posa mshenga ni lazima.
 
Nashukuru sana ndugu yangu kwa kunipa mwanga na kupata pa kuanzia,kuhusu suala la dini ni kama nimeshaliweka kando maana nina miaka kama 15 sijauona mlango wa kanisa.ila nafikiri hilo wazo la kutafuta mshenga nalifanyia kazi.SHUKRANI SANA NDUGU
 
Hyo posa peleka kwa mke wako uliyemzalisha watoto 3 bila kusahau zawadi kwa wanao uone jinsi gani wanavyofarijika na uwepo hapa duniani.
 
Tatizo hataki hata kuniona na watoto amesema analea mwenyewe kwa kuwa uwezo anao,hiyo zawadi nawapa vipi ndugu
 
Hyo posa peleka kwa mke wako uliyemzalisha watoto 3 bila kusahau zawadi kwa wanao uone jinsi gani wanavyofarijika na uwepo hapa duniani.

Kama hitaji lako ni ushauri wa kujenga, zingatia huu hapa.... vinginevyo turuhusu tuendelee kubwabwaja kile unachotaka kusikia.
 
Back
Top Bottom