Jamani uswahilini kuna mambo......! Kweli kikulacho ki nguoni mwako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani uswahilini kuna mambo......! Kweli kikulacho ki nguoni mwako

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kajukeg, Jul 28, 2010.

 1. kajukeg

  kajukeg Member

  #1
  Jul 28, 2010
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naishi na mzee mmoja ambaye miezi kadhaa iliyopita alifiwa na binti yake mdogo mwenye umri yapata miaka mitano,kifo cha mtoto huyu kiligubiKwa na utata mwingi kwani vipimo vya hospitali vilionyesha mtoto amekufa baada ya kula chakula chenye sumu,haikujulikana mapema chakula cha sumu ile mtoto alipewa na nani.

  yapata miezi minne sasa imepita,ndipo usiku wa jana kilipotokea kituko cha mwaka, familia moja ambayo ni family friend na jirani kabisa na familia iliyopata msiba pakatokea ugomvi mkubwa ulioambatana na maneno makali,pamoja na matusi makubwa baada ya mwanamke kumfumania mume wake;

  ugomvi ulikuwa hivi kwa kifupi....

  Mwanamke: toka huko malaya mkubwa wewe,mwanaume suruali,kazi kutembea na wake za watu,na nakuhakikishia lazima nikamwambie mzee (.......) jina kapuni,kwamba nimekukuta guest na mke wake.

  Mwanaume: Nenda kamwambie mchawi mkubwa wewe,muuwaji mkubwa,umemtilia sumu kwenye ndizi mtoto wa mzee (.........) jina kapuni,kwasababu ya roho mbaya uliyonayo shetani mkubwa wewe,na kesho fungasha kila kilicho chako uondoke mbwa wewe.

  Hamuwezi amini familia ile iliyofiwa na mtoto msiba ukaanza upya usiku wa jana vilio vikatawala nyumba nzima, huku baba wa mtoto akijiapiza kulipa kisasi.

  Jamani ubinadamu kazi,jihadharini na hizo family friend zenu.
   
Loading...