Kabla ya kulalamikia upweke kwanza jitazame wewe mwenyewe kwanini uwe mpweke....kwanini upo mbali na watu.....??
Kwanini watu wanakutenga na kujiweka mbali nawe....??
Je hali hiyo imezuka tu hivi karibuni au upo nayo tangu zamani..?Na kama ni hivi karibuni ni kwa sababu gani....??
Ukichunguza kwa umakini utakuta jumba la upweke tunalijenga sisi wenyewe kwa kuweka uzio baina yetu na wale wanaovutiwa nasi......uzio ambao
unafanya tujione kama tupo kwenye dunia ya peke yetu....lakini tunaweza kulibomoa jumba la upweke kwa kutokea nje ya box na kubadili mtazamo wako juu ya watu...tambua kwamba kila mtu anahitaji heshima...na hakuna mkamilifu ndani ya sayari na kukosea ni sehemu ya maisha.
Jambo la msingi na busara ni kuwa mvumilivu kwa hali zote.....saidia watu kwa kadri ya uwezo wako...cheka na kila mtu....jitokeze kwenye mijumuiko ya kijamii kama vile misiba na sherehe....jishushe...
Kumbuka dunia msongamano....