Jamani tuwe tunawasidie wenzetu ambao bado wapo gizani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani tuwe tunawasidie wenzetu ambao bado wapo gizani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PAMBANA, Sep 2, 2012.

 1. P

  PAMBANA Member

  #1
  Sep 2, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu habari za Jumapili, leo katika pitapita yangu mjini Morogoro baada ya kutoka kanisani nikakutana na kakikundi cha watu wakijadili na kusema kuwa CCM wakitoka madarakani basi watanzania wamekwisha wakijaribu kutoa mifano ya Kenya na maeneo mengine ambayo baada ya kuving'oa vyma kongwe walipita kwenye migogoro kidogo, pia walitoa mfano wa nchi ya Libya ambayo kabla ya kuingia kwenye migogoro ya kisiasa raia wake walikuwa wanaishi maisha ya raha kupata huduma zote muhimu kwa binadamu. Baada ya kuwasiliza kwa pembeni nilikugundua mambo yafuatayo kuhusu hawa jamaa:

  Kwanza inaonekana hawa jamaa ni wanazi wa CCM maana walikuwa watetea sana sera za CCM ambazo zimeshindwa kuleta mabadiliko yaliyotarajiwa kiuchumi, kijamii, kiafya n.k kwa muda wa miaka 50 tulinayo toka tupate uhuru.Tunaposema sera hizo zimeshindwa wengine wanatushangaa na kuona kwamba hatuomi ambayo yamefanywa mpaka sasa kama vile ujenzi wa barabara, shule, kilmo n.k.Haya yote ni sawa lakini hayaendani na umri tulionao ukilinganisha ua rasilimali tulizonazo, wakati wenzetu wanakimbia sisi ndo kwa tunarudi nyuma kwenye hatua ya kutambaa.Kwa mfano nchi ya Korea Kusini miaka ya 1960s na nyingine nyingi za hapo mashariki Kama Malysia, Indonesia tulikuwa na uchumi unaofanana lakini leo hatuwezi kujilinganisha nao hata kidogo maana wenzetu wana viwanda vingi wanazalisha vitu vingi sana wanatuuzia sisi pamoja na mataifa mengine.Lakini hata kiwanda cha sindano kimetushinda.Miaka hiyo mpaka 1980s tulikuwa na viwanada vya zana za kilimo, nguo na vingine lakini karibia vyote vimekufa na CCM wameshindwa kuwatumia wasomi tulionaao ili kuvifufua viwanda hivi.Sasa sijui kuna haja gani sera ambazo zimeshindwa kuinuia uchumi wa taifa hili ambalo limebarikiwa na rasilimali za kila aina.

  Pili ni watu wanaogopa mabadiliko yanayotarajiwa kutokea hapa nchini maana hakuna mabadiliko kiulaini, mabadiliko yoyote na mahali popote hapa duniani yana yana gharama zake na changamoto nyingi.Korea Kusini pamoja na mataifa mengine ya huko mashariki hawakufika hapo walipo kirahisi.Hata wenzetu Kenya pamoja na migogoro waliyoipitia kodogo mwaka 2008 baada ya uchaguzi leo uchumi wao umetulia na hatuwezi kujilinganisha na wao.Mfano mdogo tu angalia hata bidhaa nyingi tunazo tumia sisi watanzania nyingi zinatengenezwa huko Kenya kwa mfano Blue Band, maziwa ya NIDO, kiwi za viatu na nyingine nyingi tu maana nilizotaja ni mfano tu nyingine utaongezea.Wakenya wanajitapa wenyewe kuwa wapo mbele yetu mara ishirini zaidi ( they ahead of us twenty times).

  Jambo la tatu nililiona na hawa jamaa ni kuwa bado wapo gizani na ndio maana nikapa kichwa cha haka kaujumbe kwa wana JF ili tunapokutana na watu kama hawa tuwape elimu ili kuwatoa kwenye giza lililowafunga.Kuna wengine huwa wapo tayari kuingia kwenye mjadala na kukubali kuelimishwa na wengine huwa ni wabishi kwa sababu ya unazi wao kwa vyama vyao na katika hili tuweke ushabiki pembeni ili tuelimishane.Hata mimi mwanaCDM nipo tayari kuelimishwa ninapoona palipo na ukweli fulani.

  Ni hayo tu ndugu zangu.Nipo tayari kukosolewa mahali popote ambapo itathibitika kuwa nimekosea.
   
 2. m

  masluphill Senior Member

  #2
  Sep 2, 2012
  Joined: Jul 4, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kabisa ma tupoi wa chama cha mabwepande esp viongozi mara nyingi wamekuwa wakihubiri maendeleo ya nchi kwa kulinganisha leo na miaka ya kabla ya uhuru.siku utamsikia DHAIFU 'wakoloni walituachia bara2 tatu ,Leo tuna mabarabara,
  Je wakati huohuo majirani zetu walikuwa na barabara ngapi? Na leo wana ngapi?,
  Lazima ujilinganishe nyanja zote! JUZI,JANA,NA LEO LAKINI PIA ANGALIA NA MAJIRANI ZAKO.
  Kwa utaratibu huo utagundua kuwa tunasogea lakini kwa mwendo mdogo sana hasa ukizingatia majirani zetu wanakimbia wakati sisi tuna tambaa mbali na kuwa tumewazidi karibu kila kitu kwa suala la rasilimali.
  Kwa uzoefu huo mdogo wa tofauti hii na majirani zetu ni wazi kabisa kuwa Uongozi wetu na chama kinacho tuongoza wana udhaifu mkubwa sana kwa kila nyanja,
  Leo kila kukicha tunaskia orodha ya ma milioni ya pesa za wavuja jasho zilizo ibwa na mafisadi na kufichwa ulaya.
  Kwa muda mrefu watu hawa wamekuwa wakitakiwa wachukuliwe hatua ila uongozi wetu umekuwa na kigugumizi hata wakafikia hatua ya kusema wakiwashughulikia serikali itayumba,ina maana serikali inawaogopa mafisadi.sasa kama hali ndio hiyo tutafanyaje ili tuepukane na Janga hili la mafisadi na kukuza uchumi wetu?

  Nidhahiri tunahitaji serikali yenye uwezo wa kuwashughulikia mafisadi bila kuwaogopa hata kidogo,wala si kuwaomba warudishe pesa,Bali kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria na sheria ichukue mkondo wake.

  USHAURI:
  TUACHANE NA UTARATIBU WA KULLALAMIKA PASIPO KUCHUKUA HATUA,NI MUDA SASA UMEFIKA KILA MWANA NCHI MWENYE UCHUNGU NA NCHI YETU tajiri wa2 wa rasilimali duniani,Kuchukua hatua madhubuti na za ujasiri,Tuelimishane,Tushawishiane, Tujiandikishe Kisha tujitokeze kwa wingi kupiga kura tena sio kupiga tu bali kuipigia kura CDM,Maana ndio chama chenye mwelekeo wa kutuokoa na janga hili la chama cha mabwepande.
  Hao wachache ambao bado wana amini kuwa bila CCMizi haiwezekani bado ni wenzetu wala tusiwatenge bali tuwa elimishe kwa hali na mali ili mwisho wa siku tuwe kitu kimoja na TUIONDOE CCM.
   
Loading...