Jamani tuwe makini na vyakula vya njiani!!

Elia Nzwalila

Member
Jan 31, 2024
6
20
Kuna Jamaa alikuwa katika Bus, yaani yeye kila stend anaagiza chakula mara mahindi, sambusa mara karanga za kuchemsha , mara chipsi

Alipofika Kateshi akakuta nyama choma basi akaagiza nusu kilo na ndizi za kuchoma za elfu mbili! Akaomba na maziwa ya mtindi akashushia!

Baada ya kumaliza kula tu alienda kwake, yaani ile anapokelewa kwa furaha na familia yake tu, akaelelekea chumbani kwake kaingia bafuni akamuomba maji ya kuoga kwa mkewe ,,

Basi ile anapewa maji ya kuoga pale pale, akuchelewa akaoga..,, akaoga vizuri mpaka mwisho.

baada ya kuoga tu akakaa na familia , yaani ile anakaa tu sebleni akawaambia familia yake tuombe tumshukuru Mungu kwa siku nzima aliotujalia,

Basi wakasali Pamoja Sala ya Usiku na kushiriki kula tena Chakula cha usiku...

Walipo maliza kula tu, yule Jamaa akawaomba familia yake wasali pamoja kwaajili ya kwenda kulala.

Yaani Kufika Asubuhi, jamaa kaamka kaoga, kavaa vizuri akaelekea ktk shughuli zake za kila Siku.

Yaani ile anafika kazini kwake tu, alipokelewa na msaidizi wake na siku nzima akaendelea kufanya kazi zake vizuri Kama kawaida akiwa na afya njema....Yaani kwa ujumla Jamaa Yuko vizuri kiafya.

AHSANTEEEN.mnifolllow sasa
 
Back
Top Bottom