JAMANI TUCTA Ipo WAPI, MBONA KIMYA!!!!

mizambwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
4,422
1,790
Shirikisho la vyama vya wafanyakazi ndio watetezi wetu sisi wanachama. Lakini kutokana na sheria iliyopitishwa hivi karibuni kuhusiana na mafao eti mtumishi hadi atimize miaka 55 ndiipo apate mafao yake.

Vyama vya wafanyakazi vimekuwa kimya tumebaki kulalamika tu katika mitandao na mitaani kitu ambacho hakisaidii katika kuleta haki ya wafanyakazi.

Wabunge tuliowachagua kwa kupanga foleni ili wakatutetee Bungeni ndio hao wametutosa kwa kupitisha sheria kandamizi.

Vyama vya wafanyakazi ambao ndio kimblio lingine limekuwa kimya hatuelewi ni kwa kuogopa serikali au kuna kitu kimepenyezwa katikati hapa.

Tunaomba TUCTA watoe kauli tuelewe; na sisi wafanyakazi tuwe na msimamo hata ikiwezekana na sisi tuseme LIWALO na LIWE!!!!!!!!!



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Back
Top Bottom