Jamani taama ya mali! mtatuua!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani taama ya mali! mtatuua!!

Discussion in 'JF Doctor' started by Rubi, Jan 26, 2010.

 1. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Ni hatari kwa afya za wanawake


  Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Basilo Matei.  [FONT=ArialMT, sans-serif]Jeshi la Polisi mkoani Arusha limekamata shehena ya taulo za wanawake bandia maarufu kama Always zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 200.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Basilo Matei, alisema jana kuwa shehena hiyo ilikamatwa juzi nyumbani kwa mfanyabiashara maarufu mjini hapa katika eneo la Baraa, jina tunahifadhi kwa sababu hatufanikiwa kuzungumza naye. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Matei alisema shehena hiyo ina maboksi zaidi ya 10,000 na zinadhaniwa kuingizwa nchini kutoka China na kusambazwa katika maeneo ya biashara kinyemela.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Aidha, Matei alieleza kuwa polisi walifanikiwa kukamata Always hizo bandia baada ya kupata taarifa kutoka kwa kampuni Procter & Gambo Ltd ya jijini Dar es Salaam ambayo ni wakala aliyeruhusiwa kuingiza bidhaa hizo nchini.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema kampuni hiyo iligundua bidhaa hizo feki kujaa sokoni. [/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Tulipata taarifa na tukaifanyia kazi na baadaye tukaweza kukamata shehena ya bidhaa hizo zikiwa zimehifadhiwa katika gahala nyumbani kwa mtuhumiwa,” alisema Matei [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kamanda Matei alieleza kuwa pamoja na kukamatwa kwa Always hizo mfanyabiashara huyo hakupatikana nyumbani kwake na ilielezwa kuwa yupo safarini nje ya nchi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Nipashe ilitafuta wataalamu wa mambo ya afya ambao walibainisha bidhaa feki za aina hiyo kusababisha maambukizi ya magonjwa ya zinaa pamoja na fangasi ambao ni hatari kwa afya ya uzazi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Daktari Baraka Mkongo alitaja magonjwa hayo kuwa ni (UTI) ambayo wadudu hushambulia mfumo wa mkojo hatimaye kwenye viungo vya ndani vya uzazi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mkongo alieleza kuwa athari za maambukizo hayo ni mbaya kwani huweza kuambukiza haraka na hata wakati mwingine huleta mitafaruku ndani ya familia kwani humbukiza haraka wakati wa kufanya tendo la ndoa.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakati mwingine ndoa zinaweza kuvunjika kwani mathalani mke akiambukizwa halafu amwambukize mume atamtuhumu mke wake kutembea nje ya ndoa au wakati mwingine wote wawili hutuhumiana na kuleta balaa katika ndoa,” alisema Dk. Mkongo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kumekuwa na wimbi la kuingizwa nchini kwa bidhaa feki kutoka China, nyingi zikiletwa na wafanyabiashara wenye tamaa ya kupata faida ya haraka haraka.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Miongoni mwa bidhaa hizo zikiwa na thamani ya mabilioni zimekuwa zikiteketezwa nchini baada ya kumatwa nchini kufuatia operesheni zinazoendeshwa na Mamlaka za Chakula na Dawa (TDFA), Shirika la Viwango nchini (TBS) wakishirikiana Tume ya Ushindani wa Kibiashara (TFCC). [/FONT]  CHANZO: NIPASHE

  Jamani tamaa ya utajiri wa haraka na mali mtatuua! hili ni janga sijui tukimbilie wapi maana kila kukicha ni afadhali ya jana,
   
 2. M

  Msindima JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Twafa
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,152
  Trophy Points: 280
  jamani hii ni hatari.
  mtawapa ugumba wake zetu bure kwa ajili ya tamaa yenu ya vijisenti
   
 4. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tobaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 5. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  shame to tanzania
   
 6. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2010
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,213
  Trophy Points: 280
  da Tanzania kila kitu feki,itabidi tutumie matambara sasa.
   
 7. Suzzie

  Suzzie Member

  #7
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15

  Haina jinsi itabidi turudi enzi zileeee!
   
 8. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,428
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  Du! Kumbe ndo sababu ugonjwa wa 'fungus' umekuwa ni tatizo sugu kiasi hiki. Hii ni HATARI!
   
 9. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Jamani hii nchi inakotupeleka siko. Wanamama tuamke, kwa nini tusiandamane hadi huko TBS au siju TFD? wanataka kutufanyaje hawa? Wamegeuza hii nchi kuwa fake kiasi hicho? I am fed up with this country....but why? mbona hata kenya tu hapa hakuna wachina wengi na bidhaa zao feki kama hapa tz?
   
 10. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii ni hatari sasa kuna ulazima sheria ibadilike na waingizaji wafungwe maisha
   
 11. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2010
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,044
  Likes Received: 383
  Trophy Points: 180
  Hizo ambazo ni genuine zikoje nikamweleze my wife wangu???
   
 12. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Akiyamungu nikigundua mtu anacheza na Afya ya mke wangu, huku akijua...NACHUKUA SHERIA MKONONI....NTAMTOA UTUMBO KIMYAKIMYA.
   
 13. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #13
  Jan 26, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kweli hii ni hatari sana kwa afya za kina mama. Lakini hii stori naona kama imengizwa thread siyo, ilifaa kuwa habari mchanganyiko. Maana mimi nilipoona heading "Jamani tamaa ya mali...(halafu neno "mtatuua!") silioni nikajua labla kuna "dawa" ya tamaa ya mali imepatikana sasa "JF Doctor" inatuhabarisha, kumbe ni criminal issue. Sasa na wale wanaotuuzia "Tomato source fake za kutengeneza kienyeji", Maji ya kunywa fake, chakula cha juzi, kuku na nguruwe walioshwa ARV?, nao ni JF Doctor stori?. Maana hivi vyote ni kucheza na afya na uhai wa binadamu.

  Ushauri kwa MODS "Kulifanya jukwaa hili kuwa genaral zaidi nafikiri lingebadilishwa jina na kuwa "JF Health" au "Jukwaa la Afya" Inasound vizuri kwani afya ni pana zaidi ya Doctor. Ni katika kuboresha tu
   
 14. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #14
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Jibu ni moja tu, huko bandarini,TRA,TFDA na TBS wote wachumia tumbo hivyo they are all corrupt what do you expect?
   
 15. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #15
  Jan 27, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Hapo nilipo - red nakubaliana na wewe.
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  Jan 27, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  huko TBS sijui wapi wamewekana ndungu .sasa nani atamsack mwenzake?
   
 17. 2my

  2my JF-Expert Member

  #17
  Jan 30, 2010
  Joined: Jan 30, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  loh hapa inabid turudie urithi wa bibi
   
Loading...