Panya anakunywa juice?
Ndugu zangu,
Ninaomba msaada wenu kwa yeyote anayejua dawa nzuri ya kukabiliana na panya,wadogo kwa wakubwa.Panya ukiweka sumu chakula hawakili,ila ukiweka chakula kisicho na sumu unakuta sahani tupu.Panya hawa wanakunywa juisi iliyoachwa kwenye glass bila kuiangusha.Panya hawa maandazi saba nimeyaacha mezani asubuhi yake nimekuta sahani kavu.
Msaada wenu tafadhali!
panya anakula maandazi saba bila kubakiza ???
Mi nakushauri ufuge paka tu. Maana ukiwawekea sumu wakianza kufia chini ya makochi na makabati hiyo harufu si mchezo! Na bado ukiwaua hao waliopo kwa sumu wengine wapya watahamia so unakua hujasovu tatizo.
Tatizo paka wa siku hizi nao ukiwalea lea wanakua masharo baro.. ! "Yo! panya men.. njoo tupozi kwenye kochi men!" LoL
Wawekee bia kwenye glasi,asubuhi watakuwa na hangover,ni kujiokotea tu.
Nimecheka sana.... eti paka nao masharobaro