Jamani nisaidieni huu ni ugonjwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani nisaidieni huu ni ugonjwa?

Discussion in 'JF Doctor' started by KIBURUDISHO, Jul 13, 2011.

 1. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 953
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  WanaJF habari za asubuhi,ninaye mwanangu mwenye umri wa miaka mitatu anapenda sana kunywa maji. Wakati mwingine huweza kuamka usiku kati ya saa saba au saa nane akiomba maji ya kunywa au asubuhi anapoamka cha kwanza anahitaji maji ya kunywa.Huu ni ugonjwa? Au hii ni kawaida tu
   
 2. God bell

  God bell JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 581
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Mkuu ukileta swali kama hili hapa Jf utapata majibu mengi sana na mengine yatakuchanganya akili. Nakushauri umpeleke huyo mtoto hospital ukaonane na doctor majibu utapata.
   
 3. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kama anavosema alie nitangulia bora umpeleke hospitali ila mi naona ni kawaida. Watoto mara nyingi wanapenda maji na labda huyo wako amesha gundua maji ndio kitu pekee humpimii kwa hiyo kila akitaka attention toka kwako anajilazimisha kunywa maji. Uzuri wa maji haya dhuru... we mpe tu.
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  jaribu kumcheki kama ana kisukari ( type 1 diabetes). kwa hiyo kuenda hospitali ni muhimu bado. kama hana kisukari,hakikisha anakunywa maji ya kutosha mchana ili asisumbuke usiku. otherwise, mwili una kitu kinaitwa ''body clock''. ndo maana hata mtoto mchanga akiskia njaa anajua kunyonya vidole! tii kiu yake
   
 5. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mkuu nenda google kaulize watakupa majibu kibao na jinsi ya kutibu..
   
 6. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Nadhani uko sahihi kuuliza, japo JF au Google isichukue nafasi ya kwenda hospitali. Kuna vitu ambavyo ni rahisi ku google, kama side effects za dawa, lakini sio kutaka kujua waumwa nini. Hiyo ni kazi ya daktari ambayo aghalabu kasomea angalau miaka mitano na kuendelea. Si kwamba nasema huruhusiwi ku google, ila naogopa usije ukaanza kutibu dalili (kama maduka ya dawa mengi yafanyavyo hapa Tanzania) wakati kuna vitu vingi ambavyo daktari akiviunganisha pamoja hufikia kutambua tatizo ama ugonjwa.
  Mimi sio daktari bingwa wa watoto, lakini kitu cha kwanza ambacho mzazi anatakiwa kukijua je, maji anayosema anakunywa mengi ni kiasi gani? Litre 2, litre 3, litre 1? Maana waweza ukasema anakunywa maji mengi wakati ni kiasi sawa kwa umri kama huo. Hivyo kabla hatujasema anakunywa maji mengi lazima tujue kiasi anachokunywa.
  Lakini pili kunywa maji mengi kunaweza kukawa ni dalili ya kuwa na kiu kubwa (kwenye magonjwa kama Diabetes Insipidus, Diabetes Mellitus n.k) au ni tatizo la kisaikologia (kama Stress, Anxiety, n.k na pia kama dalili za mwanzo za autism). Hivyo utaona dalili ya kunywa maji mengi yenyewe haiwezi ikakupa jibu la tatizo, ila labda kutakuwa na dalili muambata ambazo zitakusaidia kujua kama kuna tatizo fulani kama vile je, mtoto anakojoa kitandani usiku, je ana hamu sana ya chakula, je anapungua uzito n.k.
  Kwa hayo yote, mwisho wa siku ukienda hospitali ukakutana na daktari na kumweleza kila kitu, hakika utasaidiwa. Kufuatana na utakavyomweleza daktari, mtoto anaweza pimwa sukari kwenye mkojo na damu na vipimo vingine kadhaa ili kujua tatizo.
  Kama mtoto wako ametoka sehemu ya baridi na kahamia sehemu ya joto pana uwezekano mkubwa asiwe na tatizo (ikiwa tumethibitisha anakunywa maji mengi zaidi ya itakiwavyo kwa umri wake), zaidi ya kuzoea mazingira ya joto. Mwone daktari wa watoto.
   
 7. Katibukata

  Katibukata Senior Member

  #7
  Jul 13, 2011
  Joined: Dec 27, 2007
  Messages: 183
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Well said! umehitimisha vizuri. Akamwone dakatari, hiyo ndiyo hatua ya kwanza.
   
 8. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 953
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Asanteni nitafanya hivyo
   
 9. g

  geophysics JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 904
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Maji ni kawaida kwa mtoto ila unaposema anakunywa mengi kiasi gani.....maana hapo ndo wataalam wataweza kukujibu vizuri..... Rafiki yangu ana mtoto ana miaka miwili na miezi minne anakuja juice karibu lita moja kwa siku na hapo ni kumbania...anaongeza wakati mwingine na maji..... Ushauri wangu ni kwenda kwa madaktari wa watoto lakini usimnyime kunywa maana maji yanalinda mwili wake usiwe dehydrated.
   
 10. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,059
  Likes Received: 6,506
  Trophy Points: 280
  no comments.
   
Loading...