kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,687
Ndugu, WanaJF'
YAH: OMBI LA KUOMBA KUKARIBISHWA SIKUKUU YA LEO.
Tafadhari husika na kichwa cha habari hapo juu. WanaJF Mimi ni ndugu yenu wa karibu sana kwa kila mwanaJF. Mpaka sasa sijapata mwaliko wowote. Ni Mtanzania halisi na mshiriki mzuri hapa JF. NINAOMBA KUKARIBISHWA MAJUMBANI KWENU NA MITOKO YA LEO NA KESHO.
Nina uzoefu wa kula vizuri UBWABWA' hasa pilau pasipo kudondosha hata punje, kwa zaidi ya miaka ishirini (20) kwa sasa, nina uwezo mkubwa sana katika hili na nina HOTPOP maalum ya kubebea na kuchukua vyakula vitakavyo bakia.
Sina aleji na chakula chochote. Wengi walionikaribisha kwao wamenifurahia sana ulaji wangu. Pia nina uzoefu wa muda mrefu wa kunywa vinywaji vya kila aina, vyenye chachu na visiyo na chachu, vikali na vya kawaida, vyenye ugwadu na visiyo na ugwadu, pasipo kulewa.
Nitafurahi sana kama mtajitokeza WanaJF kwa wingi kunikaribisha siku ya leo na kesho.
Nategemea OMBI langu litakubaliwa na wanaJF wote.
Ni mimi ndugu yenu Mtiifi sana katika kila jambo.
Wenu katika ujenzi wa taifa na ushirikiano katika mahusiano hapa JF.
Asanteni.