"Zamani nilidhani kila mzungu kashawahi kupanda ndege" -- Mr. Kamugisha, 1997.
Wazungu, kama kundi, wana utamaduni wa kutunza kumbukumbu na wana umoja; nadhani hiyo ndio tofauti kubwa sana na sisi Waafrika.
Mifano:
1. Wazungu wanaandika kwenye diary kila jambo muhimu, hata ya upuuzi. Ukifanikiwa kuinasa diary ya Mzungu, hutaamini macho yako. Hivi diary kwa lugha ya kikwetu sijui inaitwaje. Hata kwa Kiswahili sijui. Nyie kikwenu inaitwaje 😉
2. Wazungu kutokana na kutunza kumbukumbu (na kuzisoma), huanzia pale mwengine alipoishia. Hii ni kwenye mambo makubwa au hata madogo. Kwa mfano, mzungu aliyekuja TZ, siku akirudi kwao, hata ikipita miaka kadhaa, mwenzake akitaka kuja TZ, atamuuliza wapi pa kufikia, dereva teksi, shambaboy, na timu nzima ya wadau wanaofaa na wasiofaa. Kama ni taasisi, atapata nyatunyatu zote kabla hajafika TZ. Siku akiripoti ofisini tayari keshajua ofisi kinaganaga. Sisi Waafrika, siku mtu akiondoka ofisini, mbali na ile karatasi ya makabidhiano ya ilimradi, unakuta hakuna institutional memory . Taasisi inajikuta inarudia makosa yaliyofanywa miaka michache iliyopita. Duplication of Efforts tele.
3. Wazungu wana umoja: ukimchokoza mmoja, umechokoza wote. Muulize Bob Mugabe (R.I.P). Wenzake wengi walikaa mbali wakimuacha apambane na Wazungu toka hemisphere zote. Of course, wameifiksi Zimbabwe, nasikia mpaka imeomba poo. Ukiharibu kwa Mzungu mmoja aliyeko TZ, wenzie wote wa TZ watajua, na watakaokuja kutoka nje watakuja tayari na data zako walizopewa naye. Ukimuwini mmoja, umewawini wote halikadhalika. Sisi sasa... Mwarabu aliweza kutuswaga toka Kigoma hadi Bwagamoyo huku akipita kwenye jamii za Waafrika wenzetu ambao walikuwa kiroho safi, mradi siyo wao wapelekwao utumwani.
Ukitaka kununua gari used, lipi unakuwa na imani nalo zaidi: la Mzungu au la Mswahili mwenzio? Imefika mahali sisi Waswahili hatuaminiani wenyewe kuliko tunavyowaamini Wazungu.
Kujibu hoja yako: Waafrika na Wazungu tuna tofauti za tamaduni, zinazoleta tofauti za maendeleo.
By the way, suali kama hilo lilipata kuulizwa na kusababisha vitabu vizima kuandikwa: