Jamani naomba ushauri ni makelele toka nyumba ya jirani hadi usiku wa manane

Asanteni. Nitaenda kituo cha police. Maana nikienda kwa hawa wa mtaa cjui mjumbe mwisho atanitaja nitaonekana mbaya
Wala ujakosea nenda tu polisi..serikali za mitaa wanakutaja na wanasema kabisa si kwani tunatatizo ni jirani yenu hapo ndio kashtaki..inasikitisha kweli..polisi nao itabidi utoe hela ya petrol hapo ndio watakuja na wala awakutaji.
 
dawa ya moto ni moto na wewe piga kelele tu usiku kucha , jamaaani eeeeh wahamiaji haramuuuuu!!!!!, utaona kama kutakuwa na kelele tena
Umenifanya nicheke mpaka basi,Mkuu kweli unakwenda na wakati,Ushauri huu ukizingatiwa hali itakuwa shwari kabisa
 
Asanteni sana wakuu... nawashukuru sana wote mliopost mawazo yenu. Usiku mwema.
 
Kodi kwa mwezi ni laki tano tena na nusu.. na pia si uswahilini basi tu imetokea wamejibana kwa nyuma basi ni fujo tu ucku
 
Kuna kifaa sijui kinaitwaje vile!Chumba cha pili hata wafungulie sauti hadi mwisho ukikiweka chumbani kwako husikii kelele hata za kuku wa jirani.
 
sasa kama ishu ndogo kama hii unaumiza kichwa kiasi hicho mpaka unakuja kuomba ushauri hapa jf?
labda kama ulikuwa unatupa taarifa kuwa unapo kaajirani yako anauza GONGO hapo labda.
kwa hilo usiwe na shaka ngoja wenyewe wakuje ila sasa hujatoa location ya wapi unaishi.
ila kumbuka hao wauza gongo huwa wanatoa kodi /fungu kwa polisi na ukienda polisi sio kwamba haujui usishangae huyo jirani yako akaanza kukukunjia uso na kukutafutia visa kisa tu umeingia anga zake
 
Kodi kwa mwezi ni laki tano tena na nusu.. na pia si uswahilini basi tu imetokea wamejibana kwa nyuma basi ni fujo tu ucku

huna haja ya kukereka kwa mshiko huo tafuta nyumba sehemu nyingine utakuwa huna kazi ya kufanya kila siku police na kutoa fedha za mafuta kwa ajili ya kuja hapo
 
Ripoti polisi gongo ni haramu!!! Na ni kosa la jinai kupika na kuuza gongo! Utakuwa unaisaidia jamii ukiripoti polisi. Ila nadhani polisi watachukua kitu kidogo tu. Nenda serikali za mitaa ripoti. Kama mtu unastarehe usisumbue wenzio hivyo hao ni kuwaripoti kwa usumbufu kwa majirani. Wakaweke kilabu chao porini kama hawawezi kunywa hiyo gongo kistaarabu!!!
Jamani wanajamii.. ni kero ya kelele na matusi ya nguoni toka kwa walevi nyumba ya jirani wanauza pombe za kienyeji na gongo. Si mchana si ucku ni kero ya kelele na matusi sana.. yaani siku nyongine wanakesha kbs... nifanyeje jamani... naomba ushauri. Niko dar.
 
Mkuu mbona tatizo lako ni dogo!!! Nenda Polisi ukaripoti, usiwe na mashaka yoyote yale hakuna atakayejua. Ikishindikana kwa Polisi hapo mtaani kwenu basi njoo tena hapa Jf tukupe wazo lingine.

Aleyn, Mimi ninatatizo kama hilo sana sana. Ni kero sugu mahali ambapo Shangazi yangu mgonjwa anaishi. Polisi hamekuwa wanaambiwa mara nyingi sana kuhusu tatizo hilo. Kwa kweli wamekuwa wakijitahidi kuwakamata wahusika na kuwaweka ndani lakini cha ajabu wakitoka kesho yake uzi ni ule ule. Kama hapo Banana Bar ya The Big Jones ni KERO kubwa sana. Polisi wa Stakishari pia wanajua hilo na wameshiriki katika kamata kamata. Tatizo lingine hata kesi ikipelekwa mahakama ya Wilaya faini zao ni Ndogo sana Elfu Hamisini kwa hiyo hawaoni tatizo kuendelea kupiga miziki hiyo. Naomba tuambie tufanye nini?
 
Huwezi kwenda polisi hiyo ni case ya serekali za mitaa wacha ukilaza wako

Anaweza kwenda Polisi ila wazito kutatua tatizo hilo. Vilevile Polisi na Serikali ya Mtaa mara nyingi hawasaidii kwa hili la makelele, hata Diwani hasaidii kabisa kwani wenye maBaa ni wadau wao wakubwa. Tafadhali kama kuna mtu anaweza kutusaidia short-cut ya kutatua tatizo hili atusaidie.
 
Back
Top Bottom