Jirani yangu ni mganga, anatufanya tusilale usiku

Mohammed wa 5

JF-Expert Member
Jun 20, 2022
1,215
2,992
Ni mwaka na miezi 2 tokea nimeanza kuishi maeneo haya mwazoni tulikuwa tunaishi vizuri, sababu Mimi napenda maeneo yanayotulia makelele sipendagi kabisa.

Miezi 2 nyuma Jirani yangu aliuza nyumba, yake mtu alionunua Ile nyumba hatumfahamu shida imeanza wiki ya pili sasa usiku hatulali, ni makelele tu Mara ngoma zinapiga usiku majira ya saa 7 au 8 na nyimbo zinaimbwa muda huo, usiku unasikia vishindo vya mtu anakimbia anazunguka nyumba eti anakimbizana na wachawi. Usiku umelala ghafla unasikia vilio Kama watu wanalia hivi sijui ndo wateja wake ni shida.

Baada ya kuulizia Ile nyumba anaishi nani tunasikia ni Mganga wa kienyeji shughuli zake anafanyia pale kwa sasa.

Tumeongea na balozi akaongee naye kuhusu tabia yake ya kutupigia makelele usiku tunaona kimya balozi sijui anamuogopa mpaka watoto usiku wanaogopa.

Kama mganga kweli si akaishi milimani uko?

Naomba kuwasilishaa
 
759f0b20-c90f-45eb-8983-515b3b563398.jpg
 
Msanii tu huyo. Mganga kweli hana mbwembwe za kukera watu.

Chukueni njiwa mtoeni manyoa yote na nazi wekeni mlangoni kwake usiku. Fululizeni kama wiki hivi muone kama hajamwaga manyanga na kuondoka.

Huyo ni mganga njaa na hapo anakutengenezeeni mazingira ya kumuogopa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom