Jamani naomba ufafanuzi kuhusu taasisi hii! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani naomba ufafanuzi kuhusu taasisi hii!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kuku dume, Jul 18, 2012.

 1. kuku dume

  kuku dume JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  http://www.hlssf.org
   
 2. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,929
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Wewe kuku dume sasa unataka ufafanuzi wa aina gani ... juu ya nini?

  Taasisi umetupatia wewe mwenyewe alafu umetupa na link ya website yao!

  Sasa kama unataka kufahamu si ungeanza na web yao wanajieleza?!

  Kwani umepitia sehemu ya FAQ kwenye web yao?

  Anyway, baadhi ya yaliyomo ni haya:

  ====

  [h=2]MASWALI NA MAJIBU YAULIZWAYO MARA KWA MARA[/h]
  HIGHER LEARNING STUDENTS SUPPORTING FUND (HLSSF).MFUKO WA KUSAIDIA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU NCHINI.MASWALI NA MAJIBU YA MASWALA MBALIMBALI YANAYOIHUSU HLSSF.UTANGULIZI.
  HLSSF ni NGO ambayo ilisajiriwa tarehe 30/10/2008 chini ya Wizara ya maendeleo ya jamii,jinsia na watoto.Ilipata usajiri namba 00NGO/00002621.
  SWALI: Je, HLSSF inatoa huduma gani kwa ujumla?JIBU: HLSSF inatoa huduma zifuatazo kwa kifupi;
  1. Inatoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa ajili ya kuwasaidia kulipa karo,kununua chakula,kulipia gharama za malazi,kununua vitabu na kufanya utafiti pamoja na mafunzo kwa vitendo.
  2. Inawatafutia scholarship za kusoma ndani na nje ya nchi wanafunzi wote ambao wanasifa za ufaulu stahili kadiri ya masharti ya wafadhili.
  3. Inawatafutia kazi wahitimu wote wa vyuo vikuu.Hii inafanywa kwa kuwakutanisha wahitimu na waajiri kadiri ya fani zao.
  4. Inatoa fursa ya kuwasaidia wahitimu wa vyuo na vijana wengineo wanaotaka kujiajiri katika fani za kisomi zaidi.Hii itafanikiwa kwa kuanzishwa kwa HLSSF ENTREPRENEURSHIP CLUBS kwenye vyuo mbalimbali nchini ambapo wanafunzi wanachama wa HLSSF watakutanishwa pamoja na kuweza kuandaa michanganuo bora.Hii michanganuo itatafutiwa mitaji na HLSSF ili kikundi husika cha wanafunzi waweze kuanzisha na kuendesha rasmi biashara yao.
  5. Kufanya utafiti juu ya matatizo mbalimbali yanayoikumba sekta ya elimu nchini;pamoja na kutoa mapendekezo kwa serikali juu ya uboreshaji wa sera husika.
  6. Kuendesha workshops,events na mafunzo mbalimbali yanayolenga kuwapatia elimu pana zaidi wafanyabiashara na wanafunzi juu ya maswala ya ujasiriamali, uongozi wa biashara, upatikanaji na uboreshaji wa mitaji,risk management,changamoto za soko huria n.k
  7. Kutoa ushauri kwa wanafunzi wa sekondari na vyuoni juu ya namna ya kufanya uchaguzi sahihi wa michepuo ya kusoma pamoja na kozi muafaka za kusoma kulingana na changamoto za ajira za sasa.
  8. Kutoa msaada wa kufanya maombi ya vyuo kwa njia ya mtandao(TCU ONLINE APPLICATIONS) pamoja na kufanya maombi ya mkopo wa BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU (HESLB) kwa njia ya mtandao (HESLB LOANS ONLINE APPLICATIONS).

  SWALI
  : Je,Uanachama wa HLSSF unapatikanaje?

  JIBU
  : Uanachama wa HLSSF unapatikana kwa kufanya maombi ya uanachama.Maombi haya yanafanywa kwa kujaza fomu za uanachama kulingana na kundi lako husika;pia inabidi ulipe gharama ya uanachama kadiri ya kundi lako husika.Pia ambatanisha bank deposit slip ya malipo yako pamoja na fomu ya maombi iliyojazwa na kubandikwa picha na kuituma kwenye sanduku la posta la HLSSF au kuileta ofisini kwetu.
  SWALI: Uanachama wa HLSSF uko wa aina ngapi?JIBU: Uanachama wa HLSSF uko wa aina nne.Zifuatazo ni aina za uanachama:
  1. Uanachama wa mwanafunzi wa sekondari.
  2. Uanachama wa mwanafunzi wa chuo kikuu
  3. Uanachama wa mzazi/mlezi wa mtoto aliye mwanafunzi.
  4. Uanachama wa taasisi isiyo ya serikali,kampuni au chuo kikuu.
  SWALI: Ada za uanachama ziko vipi?Je,zinalipwa mara ngapi?
  JIBU
  : Ada za uanachama ni kama ifuatavyo:
  1. Ada ya uanachama wa mwanafunzi wa sekondari na mwanafunzi wa chuo ni Tsh.10,000.
  2. Ada ya uanachama wa mzazi/mlezi wa mtoto aliye mwanafunzi ni Tsh.50,000.
  3. Ada ya uanachama wa taasisi isiyo ya serikali,kampuni au chuo kikuu ni Tsh.100,000.
  ADA hizi zinalipwa mara moja tu;pale ambapo mwanachama anajiunga na HLSSF. SWALI: Kuna michango ya mwanachama au la?Kama ipo,Je ni ya aina gani?
  JIBU
  : Ndio kuna michango ya wanachama ya aina mbili.Michango hii ni kama ifuatavyo:
  1.Michango ya mwisho wa mwaka.Michango hii inategemeana na aina ya uanachama kama ifuatavyo:
  • Mwanafunzi wa sekondari atalipa Tsh.20,000.
  • Mwanafunzi wa chuo atalipa Tsh.30,000.
  • Mzazi au mlezi wa wanafunzi atalipa Tsh.80,000.
  • Taasisi ya serikali,kampuni au chuo kikuu kitalipa Tsh.200,000.
  NB: Hii ndio michango itakayo mtabulisha mwanachama husika kuwa ni “active member of HLSSF”.2.Michango ya kila mwezi .Hii ni michango itakayofanyika kila mwezi kwa kiwango kitachoafikiwa na muhusika.Hii ni michango itakayofanywa na wazazi au walezi wa wanafunzi wa sekondari au chuo kwa lengo la kuwawezesha watoto wao kulipa gharama muhimu za chuo kwa miaka ijayo.Kulingana na makubaliano HLSSF itamuongezea mwanachama kiasi cha pesa kulingana na michango yake ya kila mwezi pamoja na mda wa kuchangia pindi tu atakapo taka kupata pesa hizo kwa ajili ya kusomesha mwanae.
  ===

  Sasa Wewe kuku dume hayakutoshi hayo? ... au unataka kujua nini?!
  .
   
Loading...