Jamani namtafuta mbunge wangu nani kamwona? Je nani mwingine mwanajf anamtafuta mbunge wake?

JATELO1

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
1,230
301
Wadau nimekuwa nikimtafuta Mbunge wangu wa jimbo la Rorya ndugu LAMECK AIRO kwa muda mrefu, je kuna mtu kamwona? Katika kikao cha Bunge kilichopita nilimtafuta sana Bungeni lkn sikufanikiwa kumwona. Sijui ana mpango gani na wananchi wake ambao wana shida nyingi sana lkn yeye yupo kimya tu; hivi anajua kwamba Ukimwi unawamaliza wananchi wake? na hali mbaya ya uchumi je? Lameck hata kuchangia kwa njia ya maandishi Bungeni imekuwa tatizo? Je ni nani sasa anayewasemea wananchi wake?
 
Sie tuna mwarabu mmoja anaitwa Aziz Abood, inavyosemekana Ndo mbunge we2 wa jimbo la Morogoro Mjini...Huyu ndo sidhani ka atakuja kuchangia, manake kipindi cha kampeni hata ile kutamka "KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI" alikuwa hadi asome kwenye kalatasi..
 
Kazi ya mbunge ni kugawa pesa? kazi ya ubunge ni kuzuia Ukimwi? Kazi ya mbunge kuinua uchumi?
 
Pole sana ndugu yangu kwa kutomwona mbunge wako kwa muda mrefu hadi umeamua kujitoa humu inawezekana kura yako ulimuuzia,

Mimi mwenzako namshukuru Mungu kwa kuwa karibia kila siku namwona Mbunge wangu Mh Mchungaji Peter Msigwa akiwa anatoa mawazo, hata kwenye Mwananchi ya leo naye mchango wake umetolewa,

Labda kwa kukusaidia wew pamoja na wazalendo wenzako wa jimboni kwenu niwape nukuu moja isemayo,' Bad Leaders are elected by good Citizens who do not Vote'; George Jean Nathani . Kwa hiyo muda wa kuachana na huyo mbunge umewadia.

Poleni sana kwa kupoteza kura zenu.
 
Kuna jamaa yangu wa Shy Mjini naye alikuwa anamuulizia Mbunge wake Mhe. Masele. Atakayemwona tafadhali atusaidie. Amemtafuta maeneo yote Shy amemkosa. Mimi mbunge wangu wa Ubungo sina shida nae. Tunapiga nae story kama kawa.
 
Kwa hiyo wewe ukipiga story na mbunge wako basi inatosha? Watanzania bana
 
Kwahiyo unataka mbunge akatoe Elimu ya kujikinga na Ukimwi?.
 
Kwahiyo unataka mbunge akatoe Elimu ya kujikinga na Ukimwi?.

Mkuu hata mimi nashangaa kuna mwingine yeye akisalimiwa tu na mbunge basi, kazi ya mbunge ni kusalimia watu?
 
Kuna jamaa yangu wa Shy Mjini naye alikuwa anamuulizia Mbunge wake Mhe. Masele. Atakayemwona tafadhali atusaidie. Amemtafuta maeneo yote Shy amemkosa. Mimi mbunge wangu wa Ubungo sina shida nae. Tunapiga nae story kama kawa.

kweli we ni kiazi. Kwahiyo mmemchagua ili mpige nae stori tu.
 
Mi mbunge wangu Vicent Nyerere..Musoma Mjini anaonekana jimbon,na maendeleo yameanza kuonekana kwan halmashaur ipo chini ya CDM
 
Sie tuna mwarabu mmoja anaitwa Aziz Abood, inavyosemekana Ndo mbunge we2 wa jimbo la Morogoro Mjini...Huyu ndo sidhani ka atakuja kuchangia, manake kipindi cha kampeni hata ile kutamka "KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI" alikuwa hadi asome kwenye kalatasi..

Ndio maana Morogoro imedumaa kimaendeleo
 
Mi namtafuta mbunge wangu wa kilombero anaitwa Abdul Mteketa aka pedesheee. Bungeni simuoni ila nackia kwa macheni huwa anapatikana je nifanyaje?
 
mi mbunge wangu wa ubungo namuona kila siku mjengoni, nadhani anakaimu nafasi ya MBOWE kama mkuu wa upinzani
bungeni.
 
Mie wa kwangu Zitto Kabwe, historia imeandikwa Kigoma Kaskazini kuna lami nzuri kama Nyerere road, big up Zitto kuna changamoto ndogondogo ambazo nasi tunaendelea kumsaidia ili mambo yaende
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom