Jamani namtafuta mbunge wangu nani kamwona? Je nani mwingine mwanajf anamtafuta mbunge wake?

Kazi ya mbunge ni kugawa pesa? kazi ya ubunge ni kuzuia Ukimwi? Kazi ya mbunge kuinua uchumi?


Du!! Siamini kama huyu jamaa huwa zinamtosha, yaani hata gamba lililokufunika hakika linakucheka saaaaaana ebu zinduka acha ulofa. Kama mbuge hana jukumu katika kudhibiti maambukizi ya ukimwi hana jukumu katika kusimamia na kufuatilia michakato ya kiuchumi ya nchi yake, ebu tupe upupu wako wa masaburi unafikiri hayo ni ya nani pekee??
 
Nadhani wanaowakilishwa na cdm hakuna anaemtafuta mbunge wake 7bu wote wanajua wajibu wao, hofu mnaowakilishwa na after hela (magamba)
 
jamani mbunge wa dodoma mjini Mh David Malole na mbunge wa Bahi mh omari Baduel
 
Wangu joseph selasini, mara ya mwisho nilimsikia akiomba posho ziongezwe ili akachangie mahafali ya shauritanga na kiraeni girls.
 
Darasa la saba hana jambo la kuchangia kwenye bunge la viwango vy karne ya 21. Poleni sana wana Jimbo la Rorya, nilikuwa naangalia kampeni zake nilikuwa nacheka sana mlivyokuwa mnashabikia et PESA!maana ninyi mlimchagua mfadhili badala ya mbunge.
 
Wadau nimekuwa nikimtafuta Mbunge wangu wa jimbo la Rorya ndugu LAMECK AIRO kwa muda mrefu, je kuna mtu kamwona? Katika kikao cha Bunge kilichopita nilimtafuta sana Bungeni lkn sikufanikiwa kumwona. Sijui ana mpango gani na wananchi wake ambao wana shida nyingi sana lkn yeye yupo kimya tu; hivi anajua kwamba Ukimwi unawamaliza wananchi wake? na hali mbaya ya uchumi je? Lameck hata kuchangia kwa njia ya maandishi Bungeni imekuwa tatizo? Je ni nani sasa anayewasemea wananchi wake?
hahahaaaaaaa yuko ka hotel men,,leo alikua kanisani anatafuta siresire
[chenchi}siunajua ni mjasiriamali pia?any way wewe humjui mbunge wako?acha kabisa jimbo la rorya mbunge wetu ni mh wenje.ila tulimpa kazi sana mh wenje....pole kaka ukimtaka mbunge wako nitaarifu nkupe namba za simu za wenje na mtawasiliana koz saiz anashughulikia suala la madawati tarafa ya luoimbo,,sio matani nikweli kabisa ye anachofanya nikowasiliana na wahisani plus madiwani waelewa ili kulikwamua jimbo letu,,,siunajua nyamagana kasi inasonga mbele?
 
pole saaana kwani we naona uko gizani,,rorya mbunge wetu tuliongea na watu wa nyamagana wametusaidi mh wenje na mpaka sasa ndo anatusemea,,juzi kabla ya kuja bungeni alikua luoimbo anhamasisha harambee ya kununua madawati...lakairo hajulikani aliko inasemekana yukom kwa bizness ya sukari huko mpakani kenya siunajua sukari inalipa saizi?wenje ndo anatusimamia saizi bwana ntakupa namba za mbunge wako wenje
 
Hivi huyu bado ni mbunge? Naona kanywea baada ya kuukosa unaibu waziri.


Bado ni "mbunge mteule" maana hata kuapishwa bado. Yupo hoi kitandani zaidi ya mwaka sasa. Tatizo ni kansa ya ubongo. Inaonekana mtoa roho anamzungukia tu!
 
Mbunge wangu ni Mh. Godbless Lema. Sasahivi yupo magereza.

Haruhusiwi kutembea na miguu jimboni. Akikutwa na watu hata 10 tu anaongea nao, anakamatwa!

Hatumtafuti kabisa maana huwa yupo jimboni na tunaona akitimiza ahadi zake kidogokidogo! Huhitaji kumwona ingawa yupo. Unaona tu mambo yake unafurahi

God bless Lema!
 
Hadi akajenga four star hotel LAKAIRO kule uswahilini kirumba na wewe jitahidi uuze dagaa utatajirika

Jamaa aliua ndugu yake mpaka kapata utajiri acha upuuzi wewe! isitoshe la cairo ina mkono wa mtu!
amka mkuu
 
Bado ni "mbunge mteule" maana hata kuapishwa bado. Yupo hoi kitandani zaidi ya mwaka sasa. Tatizo ni kansa ya ubongo. Inaonekana mtoa roho anamzungukia tu!

Hivi siyo kwamba anapumua kwa mashine kweli? namuombea apone, ila nadhani atakuwa chizi!
 
Pole sana ndugu yangu kwa kutomwona mbunge wako kwa muda mrefu hadi umeamua kujitoa humu inawezekana kura yako ulimuuzia,

Mimi mwenzako namshukuru Mungu kwa kuwa karibia kila siku namwona Mbunge wangu Mh Mchungaji Peter Msigwa akiwa anatoa mawazo, hata kwenye Mwananchi ya leo naye mchango wake umetolewa,

Labda kwa kukusaidia wew pamoja na wazalendo wenzako wa jimboni kwenu niwape nukuu moja isemayo,' Bad Leaders are elected by good Citizens who do not Vote'; George Jean Nathani . Kwa hiyo muda wa kuachana na huyo mbunge umewadia.

Poleni sana kwa kupoteza kura zenu.

Humu ndani kumbe kujipigia pasi inaruhusiwa??
 
Mbunge wangu ni Mheshimiwa Spika, alikashifiwa na mnafiki fulani kuwa amewekwa na mafisadi lakini hajakanusha na hivyo katuweka njia panda wapiga kura wake kama kweli kawekwa na mafisadi au ni wivu wa kike wa yule mnafiki. Mbunge wetu alikuwa na mkwanja wa kutosha wakati wa kampeni akawanunua wapinzani wake akapita bila kupingwa, hivyo tukabahatika kuepukana na yale manguo ya kijani yenye ishara ya ufisadi. Hatuna mtu wa kupeleka shida zetu bungeni kwa vile mbunge wetu ndio anayepokea shida za wengine hivyo hawezi kujipelekea shida zake mwenyewe, itakuwa sawa na kutoa hela mfuko wa shati ukahamishia wa suruali na kusema zimeongezeka, katiba mpya ije ituokoe. Tunatarajia kumuona mbunge wetu akija kula Xmass na Mwaka Mpya, tutaserebuka naye lakini shida hatutampa yeye kwani hana kwa kusemea, yeye ni spika wa wengine.
 
Umenikumbusha kwenye kampeni zake mh. AIRO aliwahi kusema ''mimi sijasoma lakini nimeajili maprofesa ndio wananisadia kufanya kazi zangu, na mkinichangua watanisadia kupanga mipango ya kuwaletea maendeleo' na Shwaiba wake Peter Zakaria (moja ya matajiri kanda ya ziwa) ambae pia hajasoma kwenye kampaini aliwahi kumsemea 'JAMANI MGOMBEA WETU NI DARASA LA SABA LAKINI MAMBO ANAYOFANYA YANAZIDI ALIYESOMA, JAMANI MSICHAGUE MSOMI CHAGUENI ATAYELETA MAENDELEO' hakika wanarorya wamechagua mtu wa kuwaletea maendeleo.
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom