Jamani mwenzenu DSTV imenishinda

Jamani mwenzenu DSTV imenishinda

mie hilo lidicoda nishaliweka store, sabab nimekosa hata mteja wakumuuzia,,,,
DSTV ni wanyonyaji wakubwa,,,
 
tatizo sio GHARAMA ZA DSTV...

tatizo ni uwezo wako wa kifedha umekuwa mdogo!!, au haukuruhusu tena kuendelea kuwepo kwenye hiyo status!!

hii ndio reflection ya kudorora kwa uchumi!!!...sio Gharama za DSTV.

unatakiwa uwe na vyanzo vilivyo stable vya kukuwezesha kuendelea kuisha maisha yanayoendana na Gharama mbalimbali zinazotokana na mahitaji husika...

kwa msaada zaidi CHAGUA CCM, CHAGUA MAGUFULI.... maisha bora kwa kila mtanzania.........ARI MPYA, KASI MPYA NA NGUVU MPYA....... HAPA KAZI TU........


Hahahahaaa. Kweli Hapa kazi tu.
 
Najuta kupoteza hata hela yangu kununua Dstv, imenibidi kufunga Azam na fundi nikamwambia alitoe na hilo dish, nimeweka ndani kabisa yeyote atakaye kuja akihitaji nampatia,hata kwa wazi wangu nime wambia watafute fundi watupie ndani wacha ni wafungie king'amuzi resonable
January Makamba na wenzake wameshindwa kudhibiti hili kabisa.
 
Muwe mnaenda baa jamani khaa mia 5 unaangalia mechi zootee
 
Mimi ni mpenzi mkubwa wa mpira wa miguu hasa ligi mbali mbali duniani.

Nilikuwa nalipia DSTV Premium 139,000 wakapandisha mpaka 199,000, na sasa hivi wamenitumia ujumbe kuwa kuanzia kesho yaani Octoba 1, itakuwa 219,000. Nimekata tamaa kabisa kwani hiyo bei ni kubwa sana.

Nimeiangalia hiyo bei nikaona mpangaji wangu analipa 30,000 kwa mwezi, hivyo kwa bei hiyo atalipa kodi ya miezi 6 yaani 180,000 na atabaki na chenji ya umeme 39,000.

Uchunguzi wangu umegundua kuwa wengi wameacha kulipia kifurushi cha juu na kile cha kati kwasababu hata ukitoza kwa watazamaji wengine hutapata hiyo hela ya kulipia.

Wenyewe wanajitahidi kupiga simu kukumbushia malipo lakini ukweli wengi wetu tutakwama, labda wafikirie upya bei zao. Sasa hapa Azam ndio wangechangamka mapema ili tuachane na hawa Multichoice.

sis tulisha hama huko tuko zetu kwenye cable tv
 
multi choice kuna siku watajuta kwa hiki kiburi wanachokofa sasa, technology inakua kwa kasi sana inayomwezesha mtazamaji kujipatia chanell nyingi na zenye ubora wa vipindi na picha, wao badala ya kuweka bei rafiki kwa subscribers wanafanya kama vile wanatukomoa, mimi niliahamia kwenye iptv na ninaona kila ninachotaka in hd!

lakni hawaonyeshi UEFA
 
Kile cha pass wamekifikisha sh ngapi maana tulizoea tsh 22,000/= ila itabidi tusepe maana hawasikii
Hiki ni 23000 mkuu wameongeza buku, hiki ndo nimekuwa member wa kukilipia kila mwezi, cha premium nimeachana nacho life inakaba unless kama nipo mapumziko ndo nalipia
 
Najuta kupoteza hata hela yangu kununua Dstv, imenibidi kufunga Azam na fundi nikamwambia alitoe na hilo dish, nimeweka ndani kabisa yeyote atakaye kuja akihitaji nampatia,hata kwa wazi wangu nime wambia watafute fundi watupie ndani wacha ni wafungie king'amuzi resonable
January Makamba na wenzake wameshindwa kudhibiti hili kabisa.
Mie zamani lilibaki juu tu kwa ajili ya kuelekeza wageni maana nilikuwa nawaambia nyumba ya tano utaona juu kuna dish la DSTV, sasa ving'amuzi vilivyoshika kasi madish yanayofanana na hilo yakaongezeka, siku nimebaki kulipia kile cha 22,000 ila wa watu wa kanda ya ziwa hasa Mwanza na Bukoba wanafunga cable tu 15,000 na unacheck game zote muhimu kupitia zile channel za kiarabu na Ten Sports plus channel kibao nzuri
 
Siyo siri dstv gharama zake zipo juu sana hata mimi nimeacha, nina kama miezi miwili, ila kupoitia thread hii nimepata kujua kwanini wao wanapandisha gharama kuliko wenzao.
Ahsanteni wadau
 
Nunua Qsat 28G weka na dish ya nile sat peleka muelekeo wa south Africa mpango mzima!
 
naomba kujua zaidi kuhusu smart tv na iptv .Maana natumia sony bravia LCD je nawezaje kuiunganisha na IPTV msaada
Mie mchovu tu wa IT ila nilifuatilia hiyo link juu niliyokuwekea nikaweza kuinstall kodi kwenye computer yangu huku nikipata maelekezo toka kwa CHIEF MKWAWA na Watu 8 (hao ndo wataalamu ukifuatilia hiyo link plus kuwaona hao jamaa nina amini watakupa maelekezo
 
Last edited by a moderator:
Sijaelewa hapa tatizo ni nini ?? Hawarushi matangazo au yana scratch sana au vipi kwani. Inakuwaje kila mtu analalamika sana tatizo nini

Hahahhaha, JF rahaa sana aisee..Karibun Bein sport HD. Channel 20 HD zote sports tu, malipo ni 45,000 tu kwa mwezi
 
Back
Top Bottom