Jamani mwenzenu DSTV imenishinda

Jamani mwenzenu DSTV imenishinda

Huu uzi umefuta kabisa hamu yakutaka kua na hii kitu.vibanda umiza vinitarajie sana.
 
Hadi jana kilikuwa 22,000/= Ila nasikia kimefika 23,000/=
 
Mbona mnalialia, kwani mmejipangaje?

Acheni ubinafsi, nenda bar jumuika na wenzako jipatie kinywaji upendacho na kwa raha zako unacheck game!

Faida ni nyingi kuliko kujifungia ndani. Kwanza utatumia gharama kidogo, pili unaweza pata hata dili la kuongeza kipato, tatu unachangia maendeleo ya mwekezaji wa ndani, nne unawahakikishia hata wahudumu upatikanaji wa mishahara yao mwisho wa mwezi n.k n.k
Kule hawashiki remote mkuu....anyway I was joking ila sio kwamba mtu akiwa ana DSTV hakai bar ila wakati mwingine kama kuna dharula au wakati mwingine game za usiku mwingi unakuta mtu unajipendelea lakini wengi wanalialia including mie ni kutokana na kuna raha nyingne ya DSTV ya unaweza ukaangalia game zingine kwa muda mwingine japo zinakuwa ni replay
 
Mie zamani lilibaki juu tu kwa ajili ya kuelekeza wageni maana nilikuwa nawaambia nyumba ya tano utaona juu kuna dish la DSTV, sasa ving'amuzi vilivyoshika kasi madish yanayofanana na hilo yakaongezeka, siku nimebaki kulipia kile cha 22,000 ila wa watu wa kanda ya ziwa hasa Mwanza na Bukoba wanafunga cable tu 15,000 na unacheck game zote muhimu kupitia zile channel za kiarabu na Ten Sports plus channel kibao nzuri
hata zanzibar wanatumia sana cable tv nilimuuliza jamaa akasema kwa mwezi wanalipa 20 elfu na channel kama 80 na kuna channel za wamanga wanaonyesha mipira..hivi hapa Dar hamna cable tv kweli?
 
TCRA hili linawahusu.
wanahitajika kutoa bei elekezi kwa hawa vendors - kama wafanyavyo EWURA kwenye bei za petroli.
 
Mbona mitusi inamwagwa kwenye mitandao lkn hawafanyi lolote. Itakua dstv?
 
Mimi ni mpenzi mkubwa wa mpira wa miguu hasa ligi mbali mbali duniani.

Nilikuwa nalipia DSTV Premium 139,000 wakapandisha mpaka 199,000, na sasa hivi wamenitumia ujumbe kuwa kuanzia kesho yaani Octoba 1, itakuwa 219,000. Nimekata tamaa kabisa kwani hiyo bei ni kubwa sana.

Nimeiangalia hiyo bei nikaona mpangaji wangu analipa 30,000 kwa mwezi, hivyo kwa bei hiyo atalipa kodi ya miezi 6 yaani 180,000 na atabaki na chenji ya umeme 39,000.

Uchunguzi wangu umegundua kuwa wengi wameacha kulipia kifurushi cha juu na kile cha kati kwasababu hata ukitoza kwa watazamaji wengine hutapata hiyo hela ya kulipia.

Wenyewe wanajitahidi kupiga simu kukumbushia malipo lakini ukweli wengi wetu tutakwama, labda wafikirie upya bei zao. Sasa hapa Azam ndio wangechangamka mapema ili tuachane na hawa Multichoice.

Dawa yao nafikiri iko njiani azam wakichukua epl tu kwisha habari yao
 
hata zanzibar wanatumia sana cable tv nilimuuliza jamaa akasema kwa mwezi wanalipa 20 elfu na channel kama 80 na kuna channel za wamanga wanaonyesha mipira..hivi hapa Dar hamna cable tv kweli?
Dar mitaa ya katikati ya mji nadhani, Cable Dar ni kama haijazoeleka kutokana na kulikuwa na TV nyingi zinapatikana free of air kabla ya kuja ving'amuzi lakini mikoani hasa kuanzia Singida kwenda Mwanza mpaka Bukoba huko Tv ilikuwa ni issue kukamatika na wengi walikuwa wananunua madish hivyo kwa mji mkubwa kama Mwanza watu wakatumia fursa wakawa wanasambaza cable yaani hata kabla ya hizi local Tv kuanza kurusha matokeo yake ikawa ndio wamezoea mpaka sasa kutokana na cable kutokuwa na mchelemchele
 
TCRA hili linawahusu.
wanahitajika kutoa bei elekezi kwa hawa vendors - kama wafanyavyo EWURA kwenye bei za petroli.

Walishawashindwa hao yaani muda mrefu kweli walikuwa wanalipisha kwa dolla kama cha premium ilikuwa dola 78 baadae wakapandisha 80 unaweza ukaandaa bajeti yako kama shilingi imezidi kudorola siku ambayo unaenda kulipa hapo inakula kwako unajikuta kuna nyongeza buku tano kutokana na bei ya dola siku hiyo
 
Hahahahhhhaàaa kumbe tuko wengii ee. Yaan Nilipiga mahesabu kodi ya nyumba ninayolipa inazidiwa na king'amuzi. Nikasema yatosha. Kwa kuwa mi mpenzi wa La Liga nimenunua Azam. Naangalia La liga kiroho safi. EPL naenda Bar nanunua soda yangu 1000. Naangalia game. Mwaka huu watafika 300,000.

Saf mkuu ht iwe El Classico tunacheki Azam Tv
 
Kama ulipo internet connection ya simu iko vizuri unaweza kufanya live streaming ni rahisi zaidi!
 
Unalipa 219,000/= umeme wenyewe kwa kaya no way

tata Dstv
 
Umeme bado tatizo kubwa,internet conn speed na mafoleni kwa kweli Maisha bora kwa watanzania hayawezekani!
 
Khee cc ndo noma wki ya tatu umeme hakuna na dstv nsha sahau at a matumz yakee
 
Jamani wakuu naomba kuuliza kwann Clouds Tv haipo kwenye list???
 
Back
Top Bottom