mbona kuna wanaomiliki mahoteli ya kitalii hawasumbuliwikosa lake ni kumiliki mashamba ya maua kule arusha
Kwa nini kila analofanya linaonekana baya machoni mwa watanzania
Nyerere alimwambia kuwa nchi haiwezi kuongozwa na bepari kama yeye, kwani kuwa tajiri ni kosa?
Kikwete akamwambia asante kwa msaada wako lakini naomba ujiuzulu uwaziri mkuu kwa manufaa ya taifa, hivi taifa ni nani.
Kama hiyo haitoshi sote tunajua yeye na JK walivyohangaika pamoja hadi kutokea kuitwa Boyz 2 Men sasa anaambiwa hatakiwi kwenye chama wala sura yake haitakiwi kuonekana nec wakati yeye ni waziri mkuu mstaafu,sawa.
Kama vile tena haitoshi wanataka kumpokonya kadi yake ili akose hata ubunge alioutolea jasho, jamani tuna nini na mtu huyu hadi yote haya yamtokee yeye tu na si mwingine. Nisaidieni.
hawawezikumfanya chochote ...hayo ni makelele tu wa utaona subiri ..kwanza si alisema JK huyu bwana kapata ajali ya kisiasa tu
Tajiri mwizi hafai ila kutumia pesa zake kuingia madarakani sawa.Kuwa tajiri sio kosa, ila tajiri anayejipatia utajiri wake kwa njia zisizo sawa ni makosa. Ni wizi. Tajiri mwizi hafai kuwa kiongozi wa nchi, ataendelea kuwaibia hao anaowaongoza.
Msaada unaoingizia hasara kubwa taifa-richmond- ni ufisadi kwa taifa aliloapa kuliongoza.
Kwa tuhuma hizo na nyingi ni sahihi kuondolewa kwenye vyombo vya maamuzi vya chama kama NEC na CC. Nadhani hiyo ingekuwa adhabu tosha kwake.
Suala la kunyang'anywa kadi ili akose na ubunge, lipo mikononi mwake. Kwa busara yake tu anapaswa kujiuzulu kuwatumikia watu wa jimbo lake hata kama atabaki kuwa mwana CCM. Kama hakufaa kuongoza watanzania, ambao wanaMonduli ni sehemu yake, hata faa abaki kuwaongoza wana Monduli.
Nasema haya kama hizo tuhuma ni za kweli. Kama sio za kweli basi na asonge mbele na maisha kama mtanzania yeyote, tujenge taifa pamoja.
Leo amekuwa Dinosaurhe is another Dinosaur that CCM could live without
aende akalime tuu