Jamani mimi mapenzi tena basi!

Jamani mimi mapenzi tena basi!

Ngoja kwanza nitoe wasifu wangu, mimi ni kijana wa makamo nina miaka 27 kwa sasa, nina kazi nzuri inayonilipa vizuri mbali na hapo nina biashara zangu binafsi za nyumba na viwanja (real estates) zinazoniingizia si chini ya laki 5 kwa siku namshukuru mungu pesa ya kubadili mboga na mafuta ya gari haisumbui.

Jamani naombeni ushauri wenu coz nahisi kufa kufa hivi..!

Ha ha ha, at 27!

Bora ufe tu.
 
"Something is wrong somewhere" haiwezekani uwe unasalitiwa na kila mwanamke unayempata. Kuna kitu kwako hakiko sawa kwenye sekta ya mapenzi,watafute hao wanawake waliokusaliti uwaulize sababu za usaliti wao nini. Ila uende friendly,utapata jawabu.
Muongo huyu ukute hata hasimamishi au pre ejaculation za kutisha
 
Kuna rafiki yangu mmoja aliachwa na mpenzi wake akaona njia moja ya kumliwaza ni kunywa pombe mwisho wake kawa teja la nguvu. Kunywa Pombe sio kutatua tatizo lako bali angalia wapi unapo kosea, Hata timu ya mpira inaweza kuwa na wachezaji wazuri na kocha mzuri lakini ikatokea kufungwa na timu pinzani sababu ndio mchezo. Kuna kupata na kukosa kama wanawake wako unawapata kwenye social media,Club,Bar na Gym, basi tafuta njia nyengine ya kutafuta mwenza lakini kama michepuko hizo ndio sehemu zao. Bila ya kusahau unapopata mwanamke usimwambie kipato chako(kuwa una hela) jifanye mtu wa kawaida tu siku za mwanzo panda mwendokasi kumfata. Jitahidi kuwa
1 Mkweli na mwenye confidence
2 Mcheshi ukiwa na mpz wako
3 Kuwa na lugha nzuri ukiwa nae
4 Muulize nini anapenda na nini hapendi
5 Mchunguze bila ya yeye kujua kama unamchunguza nyendo zake.

Kuhusu nini cha kufanya baada ya kumfuma mpz wako na njemba nyengine huo ni uamuzi wa moyo wako, Dalili za mvua ni manyunyu leo imenyesha nje ya ndoa kesho itanyesha ndani ya ndoa. nategemea umenipata kila la kheri mkuu
Asante sana kwa busara zako, nimepata kitu kimoja kwenye ushauri wako, ki ukweli mimi sijawai kua mcheshi na sina kipaji cha ucheshi kwa wanawake zangu uenda hilo ndo tatizo.
 
Pole kijana, nakushauri kwa sasa usimwache ama kutangaza kumwacha, tens usiseme hats kwa ndugu, endelea kuwa nae ila kama rafiki bila yeye kujua nia yako, na nia iwe kusubiria had mtoto azaliwe, ili kama so wako basi utaamua kumwacha. Ila nia ya pili iwe kumpa mda ajutie dhambi, nakuhakikishia kipindi hiki had I anajifungua atajutia na kujirekebusha, kumbuka wakati huo ajui mpango wako HVO atatafuta kila hali abadilike na kukuthibitishia. Sasa iwapo yote mawili yatakuwa positive yaani mtoto wako na yeye katubu, baso waweza kumwoa mlee motto. Ila kama mtoto so wako basis hip utakuwa muda mzuri kumwacha na kushirikisha familia. TAMBUA itakuwa aibu sana ukimtangaza kwa familia na kumwacha, ikitokea mtoto no wako itakuwa ngumu kumpata au kumkaribia. Vumilia na mwombe mungu kwa hekima zaidi ! Usikate tamaa, mshukuru mungu hats kwa hili!
Kweli nimeamini humu kuna ushauri murua, asante ndugu yangu maana umenifungulia mtazamo mwingine.
 
Mtu Mwenye biashara inayomuingizia Tsh 500K kwa siku hawezi kuleta malalamiko ya kusalitiwa na mpenzi hapa JF kijana. Jitafakari halafu chukua hatua. Inawezekana tatizo lako kubwa ni Uongo na Ulaghai kwa hao mabinti. Jitathmini.
 
Daah promo n matangazo on fleek mnaotafuta mtarimbo six pack n pesa kazi kwenu
 
Asante sana kwa busara zako, nimepata kitu kimoja kwenye ushauri wako, ki ukweli mimi sijawai kua mcheshi na sina kipaji cha ucheshi kwa wanawake zangu uenda hilo ndo tatizo.
Jitahidi sana na ucheshi usiwe serious kama gaidi au kamanda Sirro😉😀. Pia kuwa muongeaji na msikilizaji hata kama hupendi anachokiongea wewe msikilize ili kumrizisha moyo wake. Sio kila tunachokifanya/tunachokiongea nao wanakipenda lakini huridhia ili kuyakuza mapenzi tu.
 
watakuja tu PM umewaweza, 500kpd na hali ngumu hii



nasema hvi watakuja tu PM
Naomba asije binti yeyote coz kwa sasa simuamini mwanamke yeyote, ninachohitaji ni ushauri tu jinsi ya kupita hiki kipindi kigumu na nisije jutia uamuzi nitakao uchukua coz mimi kinachoniumiza ni mimba aliyoibeba coz sina uhakika kama ni yangu ama si yangu, kwa sababu ya tukio la fumanizi.
 
Mtu Mwenye biashara inayomuingizia Tsh 500K kwa siku hawezi kuleta malalamiko ya kusalitiwa na mpenzi hapa JF kijana. Jitafakari halafu chukua hatua. Inawezekana tatizo lako kubwa ni Uongo na Ulaghai kwa hao mabinti. Jitathmini.
Mkuu kuwa na hela sio kila kitu kuna muheshimiwa fulani ana hela hatarii lakini mkewe alikuwa analiwa na jamaa kachoka kinomaa.
 
Daah promo n matangazo on fleek mnaotafuta mtarimbo six pack n pesa kazi kwenu
Daaaaah! ndugu yangu, mimi sihitaji mwanamke wa kunifata, coz mimi nikihitaji mwanamke namfata yeye, na siyo yeye anifate mimi coz wengi walionifata ndo walikua wa kwanza kunisaliti so, kiufupi sihitaji binti yeyote anifate private kwa hii post, me ninaomba ushauri tu coz sijui nifanye nini.
 
Jitahidi sana na ucheshi usiwe serious kama gaidi au kamanda Sirro😉😀. Pia kuwa muongeaji na msikilizaji hata kama hupendi anachokiongea wewe msikilize ili kumrizisha moyo wake. Sio kila tunachokifanya/tunachokiongea nao wanakipenda lakini huridhia ili kuyakuza mapenzi tu.
Nimekuelewa ndugu, nitalifanyia kazi hilo.
 
wambie wazazi kuwa umemfumania so ndoa hairisha akijifungua pima DNA baada ya majibu nyoa au suka. Hiyo mimba sio yako
Duuuuuuh! tayari wazazi wanajua mimba ni yangu. ila asante ndugu nitaangalia uwezekano wa kufanya ivo.
 
Habari za mwezi mtukufu wa ramadani!

Mimi ni mgeni humu jamii forums lakini nahisi nyinyi ni watu wenye upendo na ushauri mzuri basi naombeni ushauri wenu.

Sijui nina kasoro gani maana kila ninapopenda natendwa, sijui ni kwanini kwa sababu ninadhani ninavyo almost vitu vyote ambavyo mabinti au wanawake hupenda kwa mwanaume, lakini nashangaa kila mwanamke nimpendae mwisho wa siku huishia kunitenda, kama sio kuniacha basi atanisaliti.

Ngoja kwanza nitoe wasifu wangu, mimi ni kijana wa makamo nina miaka 27 kwa sasa, nina kazi nzuri inayonilipa vizuri mbali na hapo nina biashara zangu binafsi za nyumba na viwanja (real estates) zinazoniingizia si chini ya laki 5 kwa siku namshukuru mungu pesa ya kubadili mboga na mafuta ya gari haisumbui. Pia nimebahatika kupata nafasi ya kuhudhuria gym kila siku tano za wiki hivyo mwili wangu unaonekana vyema na pia sura yangu si nzuri wala si mbaya nadhani nipo kwenye kundi la watu wa kawaida ki mtazamo wa sura. Ukija katika upande wa uanaume ki ukweli namshukuru mungu kanijalia mtarimbo wa maana na show napiga ya uhakika siyo kwamba najisifia ila huo ndo ukweli halisi, kiufupi bao la kwanza hua hata sipumziki naunganisha, (hapo kama nimeenda kavu na binti ninae muamini kiafya).Na kila binti niliyewai kushiriki nae tendo la ndoa hudhihirisha dhahiri ufundi wangu katika shughuli hiyo.

Lakini cha ajabu nimekua mtu wa nuksi kila binti ninaeamua kua nae katika uhusiano mwisho wa siku huishia kuniacha au kunisaliti (Kunicheat) najiuliza why? coz ninampa kila anachohitaji kuanzia mapenzi mpaka basic needs n.k.

kilichofanya niandike waraka huu ni binti niliyempata mwaka jana mwezi november ambae alikua tofauti na wengi walionisaliti, yeye alionekana innocent sana kuanzia sura mpaka matendo basi nikasema asante mungu baada ya kusalitiwa na wanawake kama kumi hatimae umenipa binti wa ndoto zangu. Yani akaichukua akili yangu akanifanya nimuamini kupita maelezo, na wiki mbili zilizopita nimetoka kumtolea mahari baada ya kupata ujauzito.

Lakini navyoandika huu ujumbe kwa sasa ni hivi binti huyo nimemfumania live akiwa na tauro tu na njemba jingine kwenye nyumba jirani hapa mtaani kwetu kwa msaada wa wasamaria wema, ki ukweli niliishiwa nguvu na mpaka sasa navoandika sijui nifanye nini maana hata wazazi wa pande zote mbili zijawaeleza kilichotokea na binti analia mda wote anaomba nimsamahe lakini moyo wangu umekua mgumu kumsamehe roho inaniuma sana na nimeanza kupata mashaka uenda mimba siyo yangu.

Sasa hapa nilipo nimechanganykiwa nimenunua mapombe makali ndiyo nakunya 24 hours sijui nifanye nini naumia sana na binti huyu ki ukweli nampenda sana, ndipo nilipomshirikisha rafiki yangu mmoja ndo akanielekeza nije huku jamii forums uenda nikapata njia.

Jamani naombeni ushauri wenu coz nahisi kufa kufa hivi..!

Utakuwa na kibamia wewe
Yaani kila demu anagongwa nje
 
Mtu Mwenye biashara inayomuingizia Tsh 500K kwa siku hawezi kuleta malalamiko ya kusalitiwa na mpenzi hapa JF kijana. Jitafakari halafu chukua hatua. Inawezekana tatizo lako kubwa ni Uongo na Ulaghai kwa hao mabinti. Jitathmini.
Natamani uwe katika situation niliyopo kwa sasa ndo utaujua ukweli, ila hata hivyo nashukuru kwa mtazamo wako ndugu.
 
Back
Top Bottom