Jamani mbona michango ya huyu mwanasiasa imekosa wachangiaji?

Dik

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
1,204
416
Najiuliza sana sana sana sipati majibu. Ni dhahiri mwanasiasa Zitho Z Kabwe alikuwa akipost chochote kinachohusiana na siasa wachangiaji walikuwa wengi tofauti na ilivyo sasa. Kuna post imewekwa hapa kuonesha mchango wake kwa bajeti inayojadiliwa sasa lakini siamini response iliyopo. Jamani ni kwa nini? Hata wale watetezi wake kutoka ccm hawaonekani kuchangia na kumpongeza kama ilivyo ada yao. Natoa rai tuendelee kuwa nae na tuendelee kumuunga mkono pale anapotoa hoja zenye maslahi kwa taifa. Au mnasemaje wadau?
 
Zitto alitoka bungeni UKAWA walivyosusa. Lakini hakuonekana kwenye mkutano hata mmoja wa ukawa. Misimamo ya Zitto kwenye muundo wa serikali hapo clear. The same applies to ACT. Wana mbwembwe nyingi lakini sera na misimamo yao kwenye katiba mpya haijulikani. Huu ni unafiq wa wazi kabisa. Zitto na ACT yake wameonyesha kiwango cha juu kabisa cha unafiq, undumilakuwili, na uzabizabina.
Mwisho wa Zitto umewadia
 
ni dhahiri hawawezi kuwa na msimamo tofauti na mfadhili wao kwani lengo lao wote ni moja.
 
Hakyanani usiombe ukachukiwa na wale waliokupenda, hebu jaribu kufuatilia Thread za mdada wa PM7 zipo hapa ndani. Yaani nimakombora tu yanapishana utafikiri tuko Bengazi ni shida sana

Kwa upande wa kamanda wangu Zitto kinacho mgharimu ni UMIMI umemtawala mno hata akiwa na jambo ambalo linahitaji umoja ktk kulishughulikia yeye anataka kuliwakilisha peke yake ili kununua sifa kwa Umma hiyo haifai ndio maana wenzake humzilia baadhi ya hoja azimalizr mwenyewe

Ukiondoa mapungufu hayo jamaa bado yuko vizuri anahitaji kutuliza kichwa ili ashughulikie baadhi ya mambo ikiwemo na mgogoro na viongozi wenzake ndani ya chama, Kikubwa alenge kupata amani na wenzie hata kama hatarudi au kurudishwa kundini basi wawe tayari kushirikiana kwa mambo yahusuyo Taifa ili kuimarisha nguvu ya upinzani hasa kwa wakati kama huu tunaojiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu hapo mwakani

BACK TANGANYIKA
 
kinyesi.
Najiuliza sana sana sana sipati majibu. Ni dhahiri mwanasiasa Zitho Z Kabwe alikuwa akipost chochote kinachohusiana na siasa wachangiaji walikuwa wengi tofauti na ilivyo sasa. Kuna post imewekwa hapa kuonesha mchango wake kwa bajeti inayojadiliwa sasa lakini siamini response iliyopo. Jamani ni kwa nini? Hata wale watetezi wake kutoka ccm hawaonekani kuchangia na kumpongeza kama ilivyo ada yao. Natoa rai tuendelee kuwa nae na tuendelee kumuunga mkono pale anapotoa hoja zenye maslahi kwa taifa. Au mnasemaje wadau?
 
Hakuna aliyeamini, kwa kumuona Yuda iskarioti akijinyonga baada ya usaliti wake.... Zzk alikuwa na fursa zote za kujenga hoja na kupendwa/ kukubalika na jamii, lakin yeye akadhan yote hayo "ANA HAKI NAYO" huku akiwapuuza waTz na eti kutaka kuua Taasisi iliyobeba mustakabari wao, CHADEMA. Sasa kakwama na ndo kaisha hivyo
 
Back
Top Bottom