Jamani likaka langu limelogwa

Hapo ni sawa na ni vizuri zaidi. Kuna wamama ambao wanaona wako huru kuongea na watoto wao zaidi; na kuna wale ambao wako close na wakwe zao na wanaweza kuwaambia shida zao. Pale inapokuja kuwa mama mkwe anamwomba mwanae mimi sioni shida as long as ndani mna maelewano mume anayemthamini mkewe anachofanya ni kumueleza tu mama ana shida unaonaje tukimsaidia kiasi kadhaa? Na hiyo ni siri ya ndani si vema ukweni wajue kuwa mtoto wao hawezi toa ela mpaka mkewe aaprove. Kuna njia nyingi za kuepuka misuguano. Kubwa ni la kutokubali hata siku moja kuuziwa kesi.

Nimekuelewa mamii nadhani niko tofauti kutokana na experience yangu na mie kuwa they are my friends kwa kweli kiasi kwamba hata kama anataka kumbom mwanaye huniinfia mie tunapanga mashambulizi. We are so close kiasi kwamba hakuna kitakachotokea kwao nisikijue, so najaribu tu kufikiria Mama anashida ashindwe kunieleza/nishindwe kuijua hadi amlilie mwanae.......... so Naomba nikukubalie mpendwa.
 
ninakaka yangu wa pekee ktk familia ya watu 5.ameoa mwanamke wa kioldmoshi.jamani dada huyo hafai.kwa uchoyo,mdomo na ubinafsi.kuna siku kaka yangu alitoa elfu 50 kumpa mama yangu imsaidie amefanyiwa oparation .mwanamke akachapa lapa kwao.yani hataki msaada wowote uende kwa mama yangu.ameshatusababisha ndugu wote tugombane na kaka yetu.ili aweze kufaidi peke yake kwa kumtawala.juzi mama yangu aliomba pesa ya kununua jiko kwa kaka.mkewe akatuma msg kwa mama.kwamba mumewe anabanwa sana na ujenzi kama hana mahali pengine pa kupata hela akavunje mahali aibe.ikabidi ndugu tuingilie kati kumuuliza wifi yetu kulikoni jamani anatutukania mama yetu aliyetulea kwa shida toka afariki baba yetu miaka 23 iliyopita.cha ajabu kaka alisaport alichokifanya na kukisema mkewe.yaani tumebaki midomo wazi. Na mshangao juu.jamani huyu kaka kalogwa au ni upoyoyo wake mwenyewe?

...dahhh,....kuna dalili ndoa hii ilikosa baraka za huyo mama na nyie kina dada tangu mwanzo.
Tatizo ni huko Old Moshi au huyo mwanamke?...kwa experience yangu ndogo ya mambo haya, nahisi
mambo yamewafika kooni huyo kaka yenu na mkewe wanavyoingiliwa kwenye ndoa yao. [Japo sio busara,] wamejionea liwalo na liwe.
 

...dahhh,....kuna dalili ndoa hii ilikosa baraka za huyo mama na nyie kina dada tangu mwanzo.
Tatizo ni huko Old Moshi au huyo mwanamke?...kwa experience yangu ndogo ya mambo haya, nahisi
mambo yamewafika kooni huyo kaka yenu na mkewe wanavyoingiliwa kwenye ndoa yao. [Japo sio busara,] wamejionea liwalo na liwe.

Aksante Mbu.......kuna kitu cha ziada hapa wifi hataki kutueleza ukweli. Haiwezekani tu hivi hivi (sijui labda)

Ingawa mke alivyofanya si sawa (soma posts za nyumba kubwa zinaelezea vizuri zaidi)
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
<br />hata cc wote tuna familia zetu tena tumeolewa wote tunatunza familia ukweni na nyumbani pia but kwa mwenzetu wa kiume sasa.utata ndo uko hapo.mbishi kama nyama ya goti.yani tumemchoka na kumpotezea
<br />
Ndo maana nkasema tayari ana familia, na nzuri zaidi kumbe na nyie mnazo za kwenu basi jengeni familia acheni mambo mengine!
 
Mimi sitetei mawifi wala mama mkwe. Inawezekana mama mkwe anaomba sana pesa kiasi kwamba inaleta shida kwa familia ya huyo jamaa. Kosa nililoliona ni mke kutokuwa na busara. Hivi kweli mumeo aombwe ela afu akwambie wapigie simu waambia hatuna ela tunajenga; kama unajipenda unaweza kufanya hivyo??? Kam si kiere ere ni nini? Kwa nini unakubali kuuziwa kesi? Kama walimuomba yeye mwache awajibu mwenyewe afterall ni ndugu zake. Sasa matokeo yake wanamwona yeye ni mbaya kitu ambacho naona ameijtakia mwenyewe kujiongezea maadui duniani.

Kupunguza ugomvi na wakwe ni kuepuka kutumiwa kuwa bad news breaker!
 
Nyumba kubwa wajua mie hii mada inanipa picha tofauti kabisa! Nafikiri mleta mada ndo ameniinfluence

Yaani naiona kama ni mojawapo ya zile familia zenye kuwekeana nyimbo za mipasho, khanga za mafumbo na vicheko vya halo haloooo utajiju' vile ambapo mke hata huo uwezo wa kutambua hii ni kesi nauziwa hana anachokiwaza yeye ni .... Eheee ngoja niwakomeshe....
 
Pole sasha but nadhani na nyie pia mna matatizo, how comes mama amuombe mwanae kitu pasipo kupitia kwa mkewe?! Inaonyesha matatizo yako kwenye uhusiano mzima na wifi yenu tangu mwanzo!!

MJ1 kwa wengi hili la mama kupitia kwa mke halikubaliki kabisa, sijui labda ni kwa mila za wengine, lakini mama anapokuwa na tatizo anatakiwa aende moja kwa moja kwa mwanae na kumueleza tatizo, lakini labda kuna mila nyingine hili haliruhusiwi.
 
Hapo sasa itakuwa kazi. Maana inategemea busara za pande zote. Ukikuta mstaarabu hata upige taarabu anaweka pamba sikioni. Ukute na yeye taarabu anaijua basi inakuwa ni mipasho kwenda mbele. Kazi kweli kweli.

Nyumba kubwa wajua mie hii mada inanipa picha tofauti kabisa! Nafikiri mleta mada ndo ameniinfluence

Yaani naiona kama ni mojawapo ya zile familia zenye kuwekeana nyimbo za mipasho, khanga za mafumbo na vicheko vya halo haloooo utajiju' vile ambapo mke hata huo uwezo wa kutambua hii ni kesi nauziwa hana anachokiwaza yeye ni .... Eheee ngoja niwakomeshe....
 
Sasa kumbe hata wewe hujui kama kalogwa?

Nnachoweza kusema ni kwamba huyo dada anachofanya sio kizuri na wala sio sahihi hata kidogo.Ajaribu kua na heshima..au anadhani huyo mumewe alishushwa toka mawinguni!

Kabisa Lizzy!, huyu dada hana adabu kabisa hata kama hana uhusiano mzuri na mama mkwe lakini majibu yake kwa kweli waume wengi hawawezi kuyakubali maana yanaweza kuzua varangati la kufa mtu ndani ya nyumba na huyo mke kujutia majibu yake yaliyojaa ufedhuli wa hali ya juu. Yaani hamsini elfu ndio isimamishe ujenzi wa nyumba!!!! Duh! Kazi kweli kweli!!!
 
Afu unajua nini BaK; mimi nakuwa more conmfortable mama mkwe wangu akimwomba mwanae kuliko mimi, ingawa sometimes ananiomba vitu vidogo vidogo kama nimnunulie kitenge and the like. Naona ni bora amwambie mwanae kwa kuwa they can talk more openely kuliko mimi. Mimi akiniomba hata milioni kwa kweli siwezi kumnyima niko tayari nikope; unaona. Lakini angemuomba mwanae wangezungumza vizuri na kumwambia mama naomba labda nipe mda mwezi huu nina majukumu; wanaelewana wenyewe.

Yani mama mkwe akiniomba mimi naona kabisa ana take advantage ya the fact kuwa siwezi sema no!

Same to my family. Yani siku nikisikia sijuhi mama/ baba/ ndugu wamemuomba mume wangu pesa lazima niwaseme; si unajua mkwe anaweza kujipinda hata kama hana kulinda heshima. Familia yangu inatakiwa iniombe mimi na yake imuombe yeye. Pesa zinatokaje ni majadiliano yetu na ni siri yetu sina haja ya kutamba kuwa mme wangu apeleki pesa kwao mpaka nimruhusu nakuwa nimemshushia heshima. Huko nje lazima mme ajulikane ndiye final say; ya ndani ni siri yetu.
MJ1 kwa wengi hili la mama kupitia kwa mke halikubaliki kabisa, sijuil labda ni kwa mila za wengine, lakini mama anapokuwa na tatizo anatakiwa aende moja kwa moja kwa mwanae na kumueleza tatizo, lakini labda kuna mila nyingine hili haliruhusiwi.
 
Sometimes mama akiniambia nisioe watu wa maeneo flani hua nachukulia poa,...
ila wazazi (hasa wamama ) wanajua sana wanawake wenzao walivo (huyo anaetaka kuwa mkeo),....

tuwasikilize,hapa nimejifunza kitu,....
 
MJ1 kwa wengi hili la mama kupitia kwa mke halikubaliki kabisa, sijui labda ni kwa mila za wengine, lakini mama anapokuwa na tatizo anatakiwa aende moja kwa moja kwa mwanae na kumueleza tatizo, lakini labda kuna mila nyingine hili haliruhusiwi.

Aksante BaK wewe na nyumba kubwa mmeniongezea maji kwenye kisima changu cha elimu kusema ukweli nilikuwia naiangalia ishu hii kupitia kwenye kioo changu............kumbe ni ile ya .kioo kioo niambie nani mzuri!!

Sasa hii ya mama kuomba msaada moja kwa moja kwa mwanae, inaapply na kwa mke pia? Yaani mie Mwj1 nimeolewa afu mama ana shida ataniomba mie? au ataniomba niongee na Mr iili amsaidie? sina ujuzi juu ya hili wapendwa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
kabisa lizzy!, huyu dada hana adabu kabisa hata kama hana uhusiano mzuri na mama mkwe lakini majibu yake kwa kweli waume wengi hawawezi kuyakubali maana yanaweza kuzua varangati la kufa mtu ndani ya nyumba na huyo mke kujutia majibu yake yaliyojaa ufedhuli wa hali ya juu. Yaani hamsini elfu ndio isimamishe ujenzi wa nyumba!!!! Duh! Kazi kweli kweli!!!

mkuu bubu ataka kusema
hapo ndippo unapoambiwa ni muhimu kuomba mungu mtu sahihi kwenye maisha yako wengine wanapata kasheshe tangu kwenye urafiki lakini wanajipa moyo kwamba atabadilika kwenye ndoa nani kakwambia..tatizo lilipo sikuhizi hata ma spiritual husband/wife yanavaa miili ya kibinadamu wewe unajua unaoa mwanammke mzuri unakuja kujuta ...ni muhimu sana nasema tena na sitoacha kusema wacha niendeeleaa kusema nikiwa na pumzi hii ya mungu sitaki kuona ndoa yako ikiaribika ama kuachana sababu ya upumbavu ama kutokuwa na ufahamu..jirekebishe anza kumuomba mungu sasa akupe mke ama mume sahihi kutoka kwa mungu......,baadhi ya wanawake wamekuwa na demons hasa wanapovishwa pete niliwahi kuleta mada kadhaa za ndoa labda kukumbusha tu kufanya maombi kabla ya ndoa kunasaidia yafuatayo

1.kupata mke/mume sahihi
huyu ni mwenzako na mnatakiwa mpendane kuliko wazazi waliokuzaa sas basi kama ni mapenzi ya mungu hata upande wa wazazi wakiwa na shida lazima unakuwa wa kwanza kukaa chini na kuwasaidia..m nawambia ukifanya mchezo unafunga ndoa na majini pasipo kujua

2.visasi
unajua kabla ya kuoana lazima umwombe mungu akusamehe wewe na mtarajiwa wako akuondolee visasi vyote kwnye ukoo wenu wapo wanandoa wengi wanateseka sababu si walivishana pete pale azania ,st joseph la hasha ni visasi vya ukoo vinawafwata..ukisoma ayubu 38:11 utaona anasema utafika mpaka lakini hutopita..kuna malango yako kila ukoo labda wewe lango la ukoo wenu ni magonjwa unaoa mke mzima wewe mzima mkisahingia kwenye ndoa unaanza ooh kisukari cha gafla ooh nanii yangu imekwisha nguvu unabaki kimya shauri yako kuna watu wanaitumia bila wewe kujua kemea visasi

ukisoma hapo juu unaweza fika mpaka kwenye ndoa lakini hutomudu kwenyendoa unaweza kuvalishwa pete lakini kuitunza poete kwenye kidole ikawa swala lingine...ukiangalia kuna familia awana hata mawazo ya kuoana ukiangalia tangu wazazi wao walichukuana wakawekana ndani wakazaliana na watoto yaani sis nao tukaza nje na watoto wao wanakuja kuzaa nje so swala la ndoa kwao linakuwa hadithiya osama..ukipata neema ya kumuoa huyo ndugu moto wake unaitaji nguvuza rohomtakatifu mashetan yatamlilia mpaka mwisho ama kwa kutumia wakwe ama yeye na mwenzie

huyo ajalogwa kajilogwa mwenyewe na dawa ya mganga ni kujiagua mwenyewe how
1.apigwe prayer aondoe laana za ukoo wenu ukoo wa huyo mwanamke..
2.akumbuke wazazi wake sio mpoaka wapate shida wengine wakwe zetu wako kwenye payroll..m wakwe zangu wana bill za mlo mwisho wa mwezi na nakuambia nilikuwa natuma na basi kila mwisho wa mwezi wakaomba wawe wanakuja wanasali kesho yake unashangaa unashika dola ujui zimetokea wapi...mwambie soln ya kujitoa ni yeye mwenyewe

jumapili njema
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Aksante BaK wewe na nyumba kubwa mmeniongezea maji kwenye kisima changu cha elimu kusema ukweli nilikuwia naiangalia ishu hii kupitia kwenye kioo changu............kumbe ni ile ya .kioo kioo niambie nani mzuri!!

Sasa hii ya mama kuomba msaada moja kwa moja kwa mwanae, inaapply na kwa mke pia? Yaani mie Mwj1 nimeolewa afu mama ana shida ataniomba mie? au ataniomba niongee na Mr iili amsaidie? sina ujuzi juu ya hili wapendwa

MJ1 kama ujuavyo mila zetu katika makabila yetu nchini zinatofautiana sana. Kwa wengi hili la mama kwenda kumuomba msaada binti yake moja kwa moja halina tatizo kabisa lakini kwa wengine haliruhusiwi kabisa. Juzi nilikuwa nazungumza na marafiki zangu sasa katika mazungumzo tukawa tunaongelea mke kwenda kutembea kwao na kufikia kwa Wazazi wake katika mazungumzo hayo nikagundua katika baadhi ya makabila hili haliruhusiwi kabisa na linaweza kuzua mtafaruku mkubwa wa kulipishana faini na kutoa sababu kulikoni hadi binti akafikia kwa wazazi wake badala ya kwa upande wa mumewe. Kwa hiyo inategemea sana na mila za wahusika.
 
Sijuhi kama haya mambo yana mila mi sijuhi mila hata moja kwenye hili ila nazungumzia logic tu. Mama yako kama ana shida inabidi akuombe wewe hata kama huna kazi; kumuomba mumeo si njema sana maana kuna kumfanya atoe kwa sababu ya aibu ya ukwe; same kwa upande wa pili. Mimi mama mkwe akiniomba pesa kwa kweli kwangu inakuwa ni challenge na lazima nitampa tu ili asinichukie; lakini mama yangu ntampa kwa kuwa ninazo niko free kumwambia uwezo wangu.
Aksante BaK wewe na nyumba kubwa mmeniongezea maji kwenye kisima changu cha elimu kusema ukweli nilikuwia naiangalia ishu hii kupitia kwenye kioo changu............kumbe ni ile ya .kioo kioo niambie nani mzuri!!

Sasa hii ya mama kuomba msaada moja kwa moja kwa mwanae, inaapply na kwa mke pia? Yaani mie Mwj1 nimeolewa afu mama ana shida ataniomba mie? au ataniomba niongee na Mr iili amsaidie? sina ujuzi juu ya hili wapendwa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Duh huyu mke angeolewa na mume kama wangu sasa hivi angekuwa milembe, ukiwa mchoyo mwanakme unafunga hata baraka kwa family na kwa mume kwa ujumla, coz jinsi mnavyoweza kutoa na kusaidia wasiojiweza na wazazi kwa ujumla na ndivo Mungu anavyozidi kuwabariki, mie kuna mwanamke namjua ni mchoyo hadi wageni wakiingia wakati anatenga chakula mezani ananuna ile mbaya, all in all mdada nyie wengine vipi? labda mngejaribu kusaidia japo kupunguza makali sababu mshajua tena wifi yenu ndio yuko hivo na hakuna mtakaloweza kubadilisha, but msichoke kumkumbusha kaka yenu mlipotokea
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Acha hizo ww masikini akipata bana!!!
50 elfu unaona cio ishu acha utoto.
sasa weee dada buku 50 tu inakutoa roho mpaka unatangaza humu?? vitu vidogo tu hivyo,,au wee ndo umelogwa?? kwanza umeolewa kweli wewe? labda tuanzie hapo
 
Back
Top Bottom