shikwashikwa
Senior Member
- Jun 5, 2015
- 188
- 46
Mimi ni mpangaji katika nyumba ya wapangaji wawili, mnaita Apatment mpangaji mwenzangu ameoa lakini shughuri zake ni za kusafiri safiri ni mtu poa tu tunaishi kama tunajuana miaka 10 iliyopita itoshe kusema ni washkaji tangu kahamia hapa,wiki mbili zilizopita shemeji mke wa mpangaji alinitaka nimsindikize akapate moja moto moja baridi nikaona poa tu hakuna mbaya tukatoka mtoko wetu ukatufikisha moja ya bar maarufu ilikuwa poa kwangu na kwake japo kulikuwa na story nyingi za kunidadisi kuhusu mahusiano yangu (maana sina desturi ya kumpeleka demu home kwangu).
Nikamdanganya yupo nje ya nchi akaleta za unawezaje kuvumilia nikawa makini kwenye kujibu maana kilaji nacho kilikuwa kikianza kukolea, nikamjibu nampenda sana mpenzi wangu mpaka kumsaliti naisi naua akacheka na kunipa hongera. Leo amenitumia mesege eti niende kwake nimpe kampani kwani alipotoka kazini kwake kapitia super market kanunua bia za kutosha na kaona sio busara mke wa mtu kunywea bar. Napata hofu japo yupo mwenyewe ndio lakini mazingira aah.
Hebu niambieni jamani japo koo liko na kiu lakini hapo hakuna ka mtego hapo