Jamani iacheni iitwe njaa kwa kweli

Darucha

Senior Member
Dec 28, 2020
107
250
Asikuambie mtu jamani njaa ni hatari Sana sikia tu kwa wenzako. Omba isikukute Mara ya Kwanza nilikuwa nashangaa Sana kusikia mwizi kaingia kwenye nyumba ya mtu kapakua wali na maharage kwenye sufuria kajilia halafu kasepa na hajaiba chochote zaidi ya wali

Njaa sometimes inafanya akili iruke kwa muda na unaweza kujikuta unafanya vitu ambavyo akili yako ikija kutulia unaanza kuwaza hivi nilianzaje.

Juna jamaa amewahi kupost humu akiwahukumu watu walikuwa wanaenda Kula chakula Cha bure katika jiji la Dar es Salaam akajaribu kusema eti watu wasipende chakula Cha bure vyengine ni vya mizimu na vimenuwiwa na Mambo ya kishirikina.

Nilijaribu kumfikiria Yule jamaa nikasema huyu jamaa hajawahi kupigwa na njaa yenye roho mbaya huyu.

Njaa inaweza kumfanya mtu akaange mchanga ale(nafikiri mnakumbuka ya Madagascar watu Kula mchanga kisa njaa),njaa inaweza kumfanya mtu anywe supu ya ndala,njaa inaweza kumfanya mtu aingie kwenye shamba la mchawi na kuvuna mahindi huku Moyoni mwake akisema liwale na liwe na njaa pia inaweza kumfanya mtu akaange manyasi ya ng'ombe na ale ili mradi alidanganye tumbo lake tu ili maisha yaendelee.na yote hayo yanatokea baada akili kuruka kidogo.

Amini nawaambieni Bora upigwe na kitu kizito kichwani Ila Sio njaa kwa kweli. Ushuhuda wangu kuhusu njaa nimewahi Kula muwa maganda yake nikayaweka kwenye ndoo baada ya njaa kunipiga kisawasawa nikaanza kuyarudia Yale maganda nikiendelea kuukombeleza utamu wa mwisho😁😁😁😁😁naaaam team mzee mtei
 

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
7,654
2,000
mi nakumbuka kuna siku ubao ulinipiga nikaokota pipi kijiti kuna mtu inaelekea ilianguka bahati mbaya kwenye michanga akaacha, aisee niliila na zile sukari zilinisaidia sana.
 

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
7,654
2,000
mi nakumbuka kuna siku ubao ulinipiga nikaokota pipi kijiti kuna mtu inaelekea ilianguka bahati mbaya kwenye michanga akaacha, aisee niliila na zile sukari zilinisaidia sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom