Jamani huu si uchawi saidia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani huu si uchawi saidia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mbelekwambe, Jun 17, 2013.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. m

  mbelekwambe Member

  #1
  Jun 17, 2013
  Joined: Jun 15, 2013
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nifanyaje,

  Nyumba ninayokaa, hali imefikia napigwa na kutishwa usiku wa manane, nimefikia nashindwa kulala maana hali inanitisha. Mara ya kwanza nikilala nilikuwa napata usingizi wa kulazimishwa baada ya hapo nahisi kukualiwa na kitu kizito ajabu najipigapiga kujishtua na inakuwa ngumu mwishowe ndiyo nafanikia , hali iliyofikia sasa hata kama sijasinzia nikijifunika net na shuka, ninapigwa kwa mshindo mdogo kama mtu ananishitua aidha mguuni au kichwani nikijifunua kuangalia sioni lolote, muda mwingine hata kama nimejiegesha tu kitandani nakuta ubaridi wa ajabu unaanza vidole vya miguu mpaka kiunoni na kurudi ikifuatiwa na hali ya uzito wa kama kukaliwa vibaya kuanzia miguuni, nimekuwa nalazimika kutolala kwa siku tatu mfululizo. hali hii ilikuwa inanitokea japo kwa interval hapa nyuma kidogo sasa imezini. Nimeondoka pale (pwani) nipo dar sasa hali hii hainitokei kabisa. Natakiwa kwenda kule kwa kuwa ni kazini, hali ngumu.

  Nisaidieni namkamata vipi huyu, nataka kumkamata. nimepima malaria sina minyoo sina what is this
   
 2. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2013
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,435
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Ulipataje kazi huko uliko.
   
 3. Kazitunayo

  Kazitunayo JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2013
  Joined: Mar 30, 2013
  Messages: 2,789
  Likes Received: 1,482
  Trophy Points: 280
  Muamin Bwana wa majeshi atakuponya
   
 4. Izz

  Izz JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2013
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Weka hapa mazingira ya kuipata hiyo kazi.

  Pili tueleze mahusiano yako kazini na wafanyakazi wenzio, na hata majirani wanaoishi kuzunguka eneo lako la kazi.

  Tatu mienendo yako ya kimapenzi toka ulipofika huko pwani.

  Naomba tuanzie hapo kabla ya kuendelea mbele!
   
 5. m

  mwana wa mama Senior Member

  #5
  Jun 17, 2013
  Joined: May 2, 2013
  Messages: 146
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nakushauri ufanye toba ya kweli shika amri na maagizo yote ya mwenyezi Mungu na usali/omba kwa bidii hakuna nguvu inashinda nguvu ya mwenyezi Mungu.
   
 6. z

  zamlock JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2013
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,850
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Ni pm nikusaidie
   
 7. m

  mbelekwambe Member

  #7
  Jun 18, 2013
  Joined: Jun 15, 2013
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nework haiko vizuri huku kwetu, najibu kwa ujumla tafadhalini:nieajiiliwa na taasisi moja baada ya kufaulu usaili
  nna mahusiano mazuri na majirani,sijaamua kuwa na rafiki kwa ajili ya mahusiano ya kimapenzi ..hivyo.. sina kabisa.. ila naongea sana na watu wengi wanawake kwa wanaume.
  Nafasi za utata:
  Ninapoishi, kuna muda nilijadiliana na mwenye nyumba juu ya umeme kwa kuwa sikuwa naridhika sana na kiasi cha kulipa, tulichukua muda kidogo kuridhiana hali hii ilinitokea ingawa ni kwa kiasi kidogo. sijawahi kunotice kama tumetofautiana na huyu bwana ila mtu yeyote anaweza tambua hali iliyyopo na tofauti. kuna siku kijana niliyekuwa nakaa naye aliripoti kwamba mwenye nyumba amesema tunawasha friji kwa siri ndani kitu ambacho kilikuwa si sahihi kabisa kwa kuwa yalikuwa ni makubaliano yetu na ndivyo nilivyofanya.. sasa katika hali kama hiyo kwa kuwa hakunambia moja kwa moja yawezekana tunakuwa tumetofautiana (pengine niko biased).
  Ofisi yetu ni ya nayo ina matatizo kias tofauti huwa zinatokea kama mnavyofaham ofisi zilivyo.
  Net work inasumbua. asante kwa ushauri na mawazo.
   
 8. m

  mbelekwambe Member

  #8
  Jun 18, 2013
  Joined: Jun 15, 2013
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu yangu naambiwa siwezi kuku-pm- naona wananijibu natakiwa kuwa nimetoa post /topic kuanzia tano.
   
 9. ndendi

  ndendi JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2013
  Joined: Nov 29, 2012
  Messages: 629
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  piga maombi ya ukweli,anza kwa kumkaribisha roho mtakatifu ili akuongoze katika maombi yako.
   
 10. Izz

  Izz JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2013
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Pole sana mkuu!

  Ebu niambie, umesema unaongea sana na wanaume na wanawake.

  Mazingira ya kuongea sana na wanawake yakoje? Na je miongoni mwao ni wake za watu?

  Umesema hujaamua kuingia kwenye mahusiano, sasa uoni kama baadhi ya hao wanawake wanaweza wakawa wanakutaka na wewe ukaonesha interest kwa wengine ambao bado "hujavunja ukimya" na hivyo kuwakera wale wanaokupenda kwa kuwapa kisogo.
  Unaweza pia ukawa kero kwa baadhi ya wanaume wa hao wanawake unaoongea nao sana, na wao wakaamua kukufunza adabu kua mke wa mtu ni sumu, unaweza kojoa dagaa au uzi!

  Fanya hima uzungumze na mwenye nyumba yako kuhusu tofauti za kulipia umeme mlizowahi kuhitilafiana. Mwambie mlitofautiana lugha na hukuwa na maana nyingine yoyote ya kumkera.

  Mwambie kama ulimkera unachukua nafasi hiyo kumtaka radhi kwani wewe ni sawa na mwanawe ambae akikosa anamkanya na maisha yanaendelea. Binadamu tumeumbwa tofauti, wengine kitu kidogo kinaweza kikawa kikubwa.

  Hiyo pwani ni wapi? Ungeweka hapa ingesaidia pia kukufahamisha baadhi ya vitu.

  Yatakwisha mkuu, kila lenye mwanzo halikosi kua na mwisho, pole sana!
   
 11. ram

  ram JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2013
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 5,988
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Huko unakoishi kuna wanga, wewe binafsi mrudie Mungu uwe unasali kabla hujalala lakini pia tafuta mtumishi wa Mungu aje afanye maombi hapo unapoishi, kwa imani maruweruwe yataisha, maana imani inaweza kuhamisha milima
   
 12. morphine

  morphine JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2013
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 2,551
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Huyu jamaa sijamuelewa kabisa post yake misamehe kwa kweli.

  Anaongelea kazi mix na nyumba anayoishi majirani zaje mix na gharama za umeme wa kuchangia...dah pole yangu.
   
 13. a

  assuredly4 JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2013
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 1,214
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hao ni mapepo, unachotakiwa ukaombewe na watu waliookoka na utubu dhambi zako na kuokoka. ukiokoka unapewa uwezo na mamlaka dhidi ya shetani, mapepo na nguvu zote za kishirikina. fanya hima, usichelewe, kwani huwezi kujua lengo lao ni nini kwako, kwani kazi za shetani ni kuchinja, kuharibu na kuua lakini kazi ya Yesu ni kutuletea uzima na uzima tele yohana 10.10, mathayo 1.21, ufunuo 21.8, luka 19.10, warumi 3.23, luka 1.77, mithali 28.13, zaburi 103.3

  nakutakia mafanikio
   
 14. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #14
  Jun 18, 2013
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kuna watu humu huwa ni mtomaso, wanaweza kukwambia "weka picha ndiyo tuamini".

  Pole ndugu huwenda 'kamati ya ufundi' ya hapo mtaani kwenu inakutest. Ukienda kwa 'sangoma' utakuwa umeweka beacon hivyo watakuandama mpaka wakukomoe. Ili kuwakomesha, wewe uwe mtu wa maombi na uzikemee nguvu za ibirisi na mawakala wake, naye Roho Mtakatifu atakulinda HAWATAKUWEZA KAMWE!
   
 15. awp

  awp JF-Expert Member

  #15
  Jun 18, 2013
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,714
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Maeneo ya pwani watu wengi ni washirikina na hawafanyi kazi, jitahidi sana kuomba kulingana imani yako
   
 16. L

  Lakisipesa Member

  #16
  Jun 18, 2013
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani watanzania hebu tuache uvivu wa kufikiri na kumsingizia shetani kwa kila kitu. Kama kuna dhambi ya kumsingizia shetani nadhani waafrika tunaongoza. Mbona kila kitu siku hizi watu walishafanyia utafiti na majibu ya utafiti yanapatikana bureeee kwenye Internet?. Hizi ndio sababu zinatufanya tusiendelee kwa mawazo ya kama haya, utamaliza pesa zako kwa mganga au Muda wako kwa wanamaombi sijui tena wakuchote pesa a.k.a sadaka hadi uwemaskini.

  kinachokusibu wewe kinaitwa sleeping paralysis....... Just type kny google "sleeping paralysis" kuna maelezo lukuki kwanini tatzo linatokea na njia za kukabiliana nalo.


  angalia wenzako kwenye hii clip halafu google kama nilivyokueleza usome kwenye wikipedia

  https://www.google.de/url?sa=t&rct=j&q=sleeping%20paralysis&source=web&cd=4&ved=0CDYQtwIwAw&url=http%3A%2F%2Fwww.youtube.com%2Fwatch%3Fv%3D8Hky0kj2u1o&ei=507AUaHIC4WgtAbEvoCoBg&usg=AFQjCNGNmIrM0QmDwFusFlHQtoNHV9GIoA&bvm=bv.47883778,d.Yms  QUOTE=mbelekwambe;6604036]Nifanyaje,

  Nyumba ninayokaa, hali imefikia napigwa na kutishwa usiku wa manane, nimefikia nashindwa kulala maana hali inanitisha. Mara ya kwanza nikilala nilikuwa napata usingizi wa kulazimishwa baada ya hapo nahisi kukualiwa na kitu kizito ajabu najipigapiga kujishtua na inakuwa ngumu mwishowe ndiyo nafanikia , hali iliyofikia sasa hata kama sijasinzia nikijifunika net na shuka, ninapigwa kwa mshindo mdogo kama mtu ananishitua aidha mguuni au kichwani nikijifunua kuangalia sioni lolote, muda mwingine hata kama nimejiegesha tu kitandani nakuta ubaridi wa ajabu unaanza vidole vya miguu mpaka kiunoni na kurudi ikifuatiwa na hali ya uzito wa kama kukaliwa vibaya kuanzia miguuni, nimekuwa nalazimika kutolala kwa siku tatu mfululizo. hali hii ilikuwa inanitokea japo kwa interval hapa nyuma kidogo sasa imezini. Nimeondoka pale (pwani) nipo dar sasa hali hii hainitokei kabisa. Natakiwa kwenda kule kwa kuwa ni kazini, hali ngumu.

  Nisaidieni namkamata vipi huyu, nataka kumkamata. nimepima malaria sina minyoo sina what is this[/QUOTE]
   
 17. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #17
  Jun 18, 2013
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160

  Apply the blood of Jesus before you sleep. It is imperative.
   
 18. Zinedine

  Zinedine JF-Expert Member

  #18
  Jun 18, 2013
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,189
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pole, si peke yako Mbaraka Mwinshehe naye yalimkuta hayo na akafanya hivi:
  moro jazz - mtaa wa saba
   
 19. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #19
  Jun 18, 2013
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  FAHAMU UWEZO WA DAMU YA YESU KRISTO
  Ukweli ni kwamba katika damu ya Yesu Kristo kunapatikana zaidi ya mambo manne nitakayokushirikisha humu; lakini kwa sasa naona nianze na haya manne:-

  1. Uwezo wa Damu ya Yesu Kristo katika kuondoa dhambi. Imeandikwa katika kitabu cha 1Yohana 1:9 kuwa; "Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata ATUONDOLEE dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote".
  2. Uwezo wa Damu ya Yesu Kristo katika kupatanisha. Imeandikwa katika kitabu cha Waefeso 2:13-16 kuwa; "Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. AKAWAPATANISHA wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba"
  3. Uzima wa Milele katika Damu ya Yesu Kristo. Imeandikwa katika kitabu cha Yohana 6:53-54 kuwa; "Basi Yesu akawaambia Amini, amini, nawaambieni, msipoula mwili wake mwana wa Adamu nakuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao UZIMA WA MILELE….."
  4. Uwezo wa Damu ya Yesu Kristo katika kutulinda. Imeandikwa katika kitabu cha ufunuo wa Yohana 12:11a kuwa; "Nao wakamshinda (shetani) kwa damu ya mwana-Kondoo…." Mtihani mkubwa sana kwetu sisi wakristo ni kuyaweka katika matendo yale tunayofahamu katika Biblia. Nakushauri kwa Jina la Yesu Kristo kuwa uwe mtendaji wa neno, na usiwe msomaji tu. Ni maombi yangu kwa Bwana ya kuwa Roho wa ufahamu wa Bwana atakuwa juu yako unaposoma na ketenda neno lake.
  Imeletwa kwenu na
  Max Shimba A Bondservant Of Jesus Christ
   
 20. kashesho

  kashesho JF-Expert Member

  #20
  Jun 18, 2013
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 4,515
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  dawa ni kusali tu hakuna zaidi ya hapo
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...