JAMANI: Hivi Zitto Zuberi mwana wa Kabwe yuko wapi?

JAMANI: Hivi Zitto Zuberi mwana wa Kabwe yuko wapi?

Status
Not open for further replies.
Zitto kashapotezwa kwenye ramani ya siasa, kapoteza kabisa umakini, amebaki kuongea taarabu majukwani na kwenye twiter yake, kwa sasa anatumbua mabiloni ya walipa kodi, yaliyoibiwa pale widharani, mabiloni hayo ndiyo fedha alizopewa Zitto na wasaliti wenzie kuanzishia chama cha ACT, kwa kifupi Zitto na genge lake, wameishanunuliwa na ccm kutugawa watanzania tuotafuta mabadiliko kupitia CHADEMA, ndio maana unamuona kimya, kapotezwa mbaya, anaona aibu hata kuongea bungeni, na wale wajumbe wanaochangia na kuzungumzia wabunge mahakama, ndio wanzidi kumnyong'onyeza kabisa, alijiona yuko peke yake , kumbe chama kinawaleta vijana wengine machachari, kitu ambacho yeye hapendi sababu ni mbinafsi.
 
Zitto si mtu wa kuropoka hovyo siyo kama lisu ambao huongea hata ubwabwa ngoja kazi ya kutunga katiba ianze utamuona motto wake.
 
Moja ya sifa kuu za wabunge wa CDM ni umaarufu, na umaarufu wao huupata kwakuwa huongea sana bungeni na kwa kiasi kikubwa hoja zao huwakosha sana wananchi wa nchi hii.

Mmoja wa watu niliozoea kuwaona wakipambana ili kuweka mambo sawa ni huyu jamaa wa Kigoma akiitwa kwa jina la Zitto. Ninachoshangaa ni kuwa simsikii tena tangu bunge la katiba lianze. Simsikii akiongea wala simuoni akimulikwa na makamera ili hata tumuone tu kama yupo.

Hivi huyu mtu yupo hayupo? Kama hayupo yuko wapi? Na kama yupo mbona kalowa hivyo? Anakuwa kama Augustino Mrema?

Mkuu,nikusahihishe jambo kidogo kwa faida ya watazamaji.Bungeni hawaongei bali kuna suala zima la kujenga hoja hii ni kwa watu makini kama Zitto.Mjadala wa katiba ni mrefu na kuna vipengele vingi vya msingi vinapaswa kuvielewa na kuvijadili kwa kina Zitto si mtu wa kukurupuka kama wabunge wengine wanaopenda media attention.
 
Sidhani kama amekwisha, bali ni muda haujatosha kuwapa fursa wabunge wote.. Utamsikia tu..
 
Kuna watu wasipolitaja taja jina la ZZT, hujisikia kuwashwa hadi wamtaje tuu roho zao zitulie!.

Kuna wajinga wajinga fulani wasiojua wanadhani haya mabishano yanayoendelea kwenye bunge maalum ni vikao vya bunge maalum vimeanza!. No way!, vikao vya bunge maalum kujadili katiba havijaanza!, hiki kinachoendelea ni "semina tuu!"
"men of integrity!" wamejituliza kimya tuu, hawana sababu ya kupigishana kelele kwenye semina, warsha na makongamano!, wao wataibuka kwenye real thing na hoja zenye mashiko!. Jee mmeishamsikia Prof. Abdalah Safari?. Kila siku yupo namuona ni mwanasheria aliyebobea na yet amejinyamazia tuu!.
Kuna watu wana kimbembelembele tuu kuongea sana, ila wanamwaga pumba tuu!, na kuna watu kwa kutoongea huko ndiko busara zao zilikolalia!.
Pasco.

Ni wenye kufikiria kwa kutumia kichwa cha juu tu watakuelewa hapo.

Wenye kutazama na kuviona vitu kwa uhalisia wake (really in black n white ) wanaweza kuona hilo.

wenye ujasili wa kusema kweli wa nafsi na si unafiki watakubaliana na wewe.

Lkn ukweli ni kwamba ZZK ni Potent Figure anywhere you can dump.
Huwez kuchanganya mchanga na dhahabu ukajisahaulisha maana itakuumbua tu kwa mng'aro wake.
 
Zitto ni kijana shupavu sana, na ni mhimili wa siasa za Tanzania, hatutegemei kumuona akiropoka ropoka hovyo kwenye bunge la katiba. Katika CHADEMA yote hakuna mwenye akili nyingi kama Zitto.
 
1237039_558673150836333_73024561_n.jpg
 
Zitto ni kijana shupavu sana, na ni mhimili wa siasa za Tanzania, hatutegemei kumuona akiropoka ropoka hovyo kwenye bunge la katiba. Katika CHADEMA yote hakuna mwenye akili nyingi kama Zitto.

Katika nchi hii zito akuzidi akili wewe na wazazi wako tu
 
tupo watanzania almost mil 45..tungekuwa na watanzania japo milion 2. Wenye akili kama ya pasco sasaivi tusingekuwa tunaandaa katiba, tungekuwa tunawaza kwenda sayari nyingine..ila aina ya watz tulio wengi ni kama Sugu, josephine mshumbusi, ole sendeka, poul makonda na le mutuz. Pasco nafurahia sana uwezo wako wa kujenga hoja hata pale unapokuwa unajadili nisivyovipenda, huwa najikuta napenda uwasilishaji wako. Mungu awajalie vijana wako nao wawe majiniaz.

mkuu ni hakika kabisa unachokisema. Huyu jamaa yuko vizuri sana.
 
Zitto si mtu wa kuropoka hovyo siyo kama lisu ambao huongea hata ubwabwa ngoja kazi ya kutunga katiba ianze utamuona motto wake.

kwani wewe ni chama gani na zitto ni chama gani, tukiwaambia watu zitto anatumiwa na ccm hubisha, huu ni uthibitisho tosha, huwezi kuwa Chadema ukatetewa na ccm, na hata ACT ni zitto na genge lake, wamedhamiwa na ccm kuihujumu CHADEMA, yale mabilioni ya fedha yanayoibiwa ndio wanayotumia kina zitto, hawa nao ni mafisadi, sababu wanatumia kodi zetu isivyo, tena kwa uizi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom