Jamani hebu oneni haya,hivi huku si kuhalalisha utoro mashuleni kwa kutumia sheria,hivi Watanzania tukoje?

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
15,859
20,713
Picha

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amempa siku 14 Kamishna wa Elimu na wataalamu wake kumpa mrejesho wa maagizo aliyotoa Julai mwaka huu, kuhusu kurekebisha Waraka wa Elimu unaompa nafasi mwanafunzi kuomba ruhusa ya kutohudhuria masomo kwa siku 90, ili kuzuia utoro kwao.
Profesa Ndalichako alisema hayo katika mahafali ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Bogwe wilayani Kasulu mkoani Kigoma, akieleza kuwa Waraka wa Elimu kumpa siku 90 mwanafunzi kutoonekana shule bila kuhudhuria shuleni, ndiyo chanzo kikubwa cha utoro mkubwa kwa wanafunzi nchini.

“Nimempa maagizo Kamishna wa Elimu nchini akae na wataalamu wake waufanyie mapitio waraka huo na kuurekebisha, maagizo nimempa tangu Julai hadi leo sijapata mrejesho wowote. Na sasa nampa siku 14 kuhakikisha kazi hiyo imefanyika na kinyume chake kamishna atafute maelezo ya kuridhisha kwa nini nisimuadhibu,” alisema.
Alisema wakati waraka unatoa siku 90 kwa wanafunzi, inashangaza kuona waalimu wanapewa siku tano wasipoonekana shule wanakuwa wamejifukuzisha kazi.

Dr Ndalichako aliendelea kusema, jambo hilo si sawa kwani halina uwiano kiuhalisia. Aidha, aliwataka wanafunzi nchini na hasa wanafunzi wa kidato cha nne wanaotarajia kufanya mitihani hivi karibuni kujibidiisha kwenye masomo ili wafaulu.
Alisema serikali inatumia fedha nyingi kwenye uwekezaji wa elimu na kwa sasa kupitia Mpango wa Lipa kwa Matokeo (EP4R), hadi Septemba mwaka huu serikali imetumia Sh bilioni 308 kutekeleza mpango huo. Katika hilo, alisema jumla ya madarasa 2,898 yamejengwa, mabweni 535, nyumbani za walimu 66, matundu 6,629 ya vyoo huku shule kongwe za sekondari 62 kati ya 88 kwa thamani ya zaidi ya Sh bilioni 300 zimekarabatiwa.

Hongera sana Dr.Ndalichako,futa kabisa waraka huo kwa kuwa una nia ovu kabisa ya kuharibu elimu yetu.Mambo kama haya yanatuhakikishia kwamba kuna nia ovu ya kuharibu elimu yetu kwa makusudi na watumishi wa Wizara ya Elimu wakishirikiana na nchi za magharibi,tena kwa malipo makubwa.Mambo haya yako documented!
 
Kati ya sheria inatakiwa kufanyiwa amendment basi ni hii maana wanafunzi wanaitumia vibaya. Afadhali waziri kaliona hilo.
 
Kuna mwanafunzi mamia kwa maelfu wanamaliza na hii sheria hawahifahamu.


Hata mimi leo ndio nimehisikia baada ya kupita kote huko.

Watafute chanzo cha tatizo ila si hii sheria!
 
Kisheria hicho kipo tangu zamani, kinawapa ugumu walimu kumfukuza mwanafunzi hata akiwa mtoro maana kinataka ili mwanafunzi afukuzwe shule inabidi asihudhurie takriban siku tisini.
 
Tena siku 90 mfululizo, asipohudhuria siku 89 akaja kuhudhuria siku ya 90, kaishaharibu hesabu. Anaanza kuhesabiwa upya.

Kuna jamaa wakati tunasoma alikuwa haonekeno shule hata miezi miwili, ila akija anapiga kipindi bila bugdha. Nikawa nashangaa kimya kimya...
 
Back
Top Bottom