Elections 2010 Jamani hata Dodoma mnakosa watu

...siku hizi ccm wamewazowesha watu tabia mbaya sana...kiasi imefikia watu hawaendi tena kwenye mikutano ya ccm kwa bashasha na kujituma kama enzi za nyuma ..... siku hizi wanataka wakienda wapewe pesa...za "usafiri"....na sijui hiyo tabia ataiponya nani......
Ni tofauti kabisa na mikutano ya vyama vya upinzani ambapo watu waanaenda bila kutaka chochote..na hata wakifika wanachangia senti zao.....nitamchangaa sana mtu ambaye ataweza kulinganisha umati wa ccm na wapinzani...umati wa mikutano wa ccm watu wapo pale kikazi tu!!!.........kwa ujira wa tzs 5,000 na fulana....nadhani karibu watanzania watakuwa wajanja kuweza kuchukua hizo pesa na kura wasiwape.....sema wapiga kura hasa kinamama wana nidhamu ya ahadi kiasi akishakula pesa za balozi wake na vitenge vya WAMA...anaamini ccm ikishindwa kwenye mtaa wao basi ....anatishiwa kuwa atadaiwa....
 

kwa taarifa tu watu tayari wana taarifa ya karatasi kiyonga za kuchakachullia kura za hapa na zanzibar zinazokuja toka nje ...na wanangoja tu kuwaumbua..watu wamejipanga..tunajuwa kuwa moja ya matumizi makubwa kwenye gharama za ccm ni kuchapisha hizi karaatasi milioni kadhaa na kuzichanganya na za NEC......
 
Mchungaji nakusoma mara kibao ukiiweka hii photo.
Mie simooooooo
wenyewe watasema umewatukana matusi ya nguoni. LOLz.

BTW sura zao zinaongea kuliko maneno yao. Wanadumisha udugu wa kudumaza wengine

KUKOMAA KWA DEMOKRASIA NDO MAANAKE.....NAONA PICHA HIO HAPO JUU MWA TAFSIRI VINGINE......
 
Ukweli lazima tukubali zamani CCM ilikuwa haifanyi hivi ilikuwa inaisanifu CUF kuwa inasomba wanaCUF sasa zamu yao yaani chama kubwa kongwe inatia aibu nafikiri 2015 itakuwa imechoka sana badala ya kutumia maroli itatumia mikokoteni.

ahaaaaaaaaaaaaaaa zamu yao sio
 

duh mwaka huu jamaa wataumbuka wakifanya mambo ya ajabu maana watu wamechoshwa wanatoa siri zao ,ni noma
 
Hivi sheria si inakataza malori kubeba abiria hasa wakati wa kampeni? Tendwa, Lewis na Said mko wapi? Hii sio foul kweli?!
 
KUKOMAA KWA DEMOKRASIA NDO MAANAKE.....NAONA PICHA HIO HAPO JUU MWA TAFSIRI VINGINE......

Ahsante mdau kwa kuweka hii. Hawa jamaa wa Chadema hawaelewi maana ya kukomaa kifikra. The picture of Kikwete with Maalim na Lipumba ni jambo la kujisifia kwamba wanasiasa wetu wamekomaa kimawazo na kupevuka. Siasa sio personal beefs wakuu. Iliwachukua vifo vya watu, fujo, na Koffi Anan kuwaweka Raila Odinga na Mwai Kibaki kwenye meza moja. Ndio mnataka twende huko jameni?
 
Iringa, malori huwa yanakwenda sana minadani ndo maana Mbega alikuwa kama vile anaongea na wanakamati kwenye kikao cha harusi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…