jamani, eti mtu ambaye hana CPA anaweza kufundisha CPA class review

Kikomelo

Senior Member
Sep 12, 2011
106
57
Kuna mkoa mmoja nimeenda nikakuta kuna watu wanafundisha watu wanaotafuta CPA lakini hao walimu wenyewe hawana CPA, inakubalika hii? Au kama mtu amesoma finance anaijua vyema anaweza kufundisha? au kama mtu ana postgraduate ya taxation anaweza kuwa anafundisha somo la kodi hata kama hana CPA?

wadau mi sielewi, naomba kufaamishwa!
 
Wajinga ndio waliwao! kama anawafundisha na wanaelewa hakuna shida....endeleaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Nimebahatika kusoma kozi kadhaa ndani na nje ya nchi na katika tembea tembea yangu nimekutana na waalimu kadhaa wataalamu wa fani wanazofundisha lakini hawana vyeti vinavyowatambulisha kuwa ni wataalamu wa fani zao.

Tatizo sio kuwa na CPA, cha kujiuliza hapa ni jee anajua anachokifundisha (whether ana CPA au la)? Hebu jiulize, mtu wa kwanza kutunukiwa PhD (au bachelor/masters degree for that matter) alifundishwa na nani?
 
Certified Public Accountant= past papers za uhasibu.
Hakuna kipya ambacho chuo kizuri cha finance kilichompika mwanafunzivambacho CPA reviews wanacho zaidivya kusolve maswali
 
Kuna mkoa mmoja nimeenda nikakuta kuna watu wanafundisha watu wanaotafuta CPA lakini hao walimu wenyewe hawana CPA, inakubalika hii? Au kama mtu amesoma finance anaijua vyema anaweza kufundisha? au kama mtu ana postgraduate ya taxation anaweza kuwa anafundisha somo la kodi hata kama hana CPA?

wadau mi sielewi, naomba kufaamishwa!

Haiwezekani kabisa kitu kama hiyo, na hiyo review ni ya kijinga kabisa. Kama anaweza kufundisha si afanye mitihani hiyo apate hiyo CPA? Hoja si kufundisha hoja ni vigezo vya kufundisha watu huo.
 
Ninavyoelewa hakuna requirement ya kuwa CPA ili ufundishe CPA kwa hiyo sio tatizo.
 
Haiwezekani kabisa kitu kama hiyo, na hiyo review ni ya kijinga kabisa. Kama anaweza kufundisha si afanye mitihani hiyo apate hiyo CPA? Hoja si kufundisha hoja ni vigezo vya kufundisha watu huo.

Inasikitisha sana kuona kuwa wengi hatujui elimu fulani inapatikanaje.

Ili upate cheti cha CPA ni lazima usome masomo kadhaa. Kila somo linatakiwa lifundishwe na mtaalamu wa somo hilo mfano: mtaalamu wa Quantitative Techniques (QT) si lazima ajue Financial Accounting, Auditing au Financial Management. Mtaalamu wa Taxation sio lazima awe mtaalamu QT.

Ili upate CPA, lazima ufaulu masomo hayo hapo juu. Mara baada ya kufaulu na kupata CPA, wengi hupata kazi za uhasibu wala hawaendi kuwa waalimu na hata wakienda kufundisha watakimbilia yale ya kihasibu sio QT na IT. Je haya yatafundishwa na nani kama tunataka wawe na CPA?

La muhimu kila somo lifundishwe na mwalimu anayelijua vizuri. Mleta mada jiangalie uwezo wako
 
Kufundisha CPA sio lazima uwe na CPA mfano kuna mwalim anaitwa Hanzuruni ni mwalim mzuri wa management Accounting ila hana CPA na kila alipo fanya MA anaongoza masomo mengne anadakwa. Kuna Mwingne anaitwa Swallo nae ni mzur wa taxation na alifaulu vizur mtihan wa bod wa taxation ila cpa hana. Kikubwa ni je mwalimu ni mzuri katika ilo somo. Kuna watu wana CPA ila akikufundisha utakaa chini ulie.
 
hebu acha kubaishwa ni ni hivi sifa za kufundisha cpa ni hizi
1.uwe na cpa
2.uwe na masters au degreee
wanaofundisha cpa wakati wao hawana ni kuwafelisha wanafunzi ndo maana cpa inakuwa ngumu kutokana na walimu vilaza kama
hawa ndo maana matokeo ya cpa yanakuwa mabaya
 
Haiwezekani kabisa kitu kama hiyo, na hiyo review ni ya kijinga kabisa. Kama anaweza kufundisha si afanye mitihani hiyo apate hiyo CPA? Hoja si kufundisha hoja ni vigezo vya kufundisha watu huo.

Punguza jaziba "tunataka Scientic argument si tu uwezo wa kubishana"
 
hebu acha kubaishwa ni ni hivi sifa za kufundisha cpa ni hizi
1.uwe na cpa
2.uwe na masters au degreee
wanaofundisha cpa wakati wao hawana ni kuwafelisha wanafunzi ndo maana cpa inakuwa ngumu kutokana na walimu vilaza kama
hawa ndo maana matokeo ya cpa yanakuwa mabaya

Haimaanishi CPA holders ni competent kwa kila eneo, Mfano huyu bwana anazungumzia somo kama Taxation SPECIALIST wake ama mwalimu wa somo kama hili Lazima atakuwa na degree ya Tax na Masters ya tax nk. sioni uhusiano na CPA kama sifa ya kufundisha TAX kama somo, ingawa haizuiliwi kwa holder wa CPA kufundisha tax, vivyo hivyo kwa masomo mengine kama QM, Financial mgt, enterprenuership, management, marketing, mangement accounting, ukiachana na somo kama Auditing & assuarance, financial reporting, lakini siyo somo kama contemporaly issues.
 
Sio lazima mwalimu awe na CPA
CPA ni professional recognition and acknowledgement of accounting field. Ila accounting knowledge and skills zinapatikana kutoka kwa scholars.
Added advantage utakayopata kutoka kwa mwalimu aliyefanya CPA na kufaulu ni exams experience ambayo watu ndio wanaipenda. Badala ya kuelewa lengo la CPA tunakomalia kuchunguza maswali yanatungwaje ili tufaulu (Exams oriented Vs knowledge oriented). Kwani wahadhiri wote wa sheria wamepita school of law au ni ma-advocates? Ila products zao ni nzuri.
Mtu anaweza akawa na CPA halafu kufundisha akawa cheche kwa kuwa alifaulu kwa kukukariri bila kuelewa maana halisi ya majibu yake kwenye hiyo mitihani.
 
Inasikitisha sana kuona kuwa wengi hatujui elimu fulani inapatikanaje.

Ili upate cheti cha CPA ni lazima usome masomo kadhaa. Kila somo linatakiwa lifundishwe na mtaalamu wa somo hilo mfano: mtaalamu wa Quantitative Techniques (QT) si lazima ajue Financial Accounting, Auditing au Financial Management. Mtaalamu wa Taxation sio lazima awe mtaalamu QT.

Ili upate CPA, lazima ufaulu masomo hayo hapo juu. Mara baada ya kufaulu na kupata CPA, wengi hupata kazi za uhasibu wala hawaendi kuwa waalimu na hata wakienda kufundisha watakimbilia yale ya kihasibu sio QT na IT. Je haya yatafundishwa na nani kama tunataka wawe na CPA?

La muhimu kila somo lifundishwe na mwalimu anayelijua vizuri. Mleta mada jiangalie uwezo wako
Uko sawa kabisa . ssi wakati tunasoma DSA mwaka 1980 tulikuwa tunafundishwa na baadhi ya waalimu wazuru lakini walikuwa hawajamaliza CPA zao wakati huo kulikuwa na Part I na II na waliowawafundisha walifauru sana na mmoja alikuwa akiendelea na kuresit somo alilokuwa hajalimalizia. Kwa mitihani ya CPA ni kupata uelewa jaribu past papers na baadae ujipime kwenye mitihani ya NBAA. NBAA hawana waalimu na wala hawakatazi kama Mtu ambaye hana full CPA asifiundishe masomo yaliyo kwenye syllabus yao.
 
Back
Top Bottom