Jamani eeh msaada ndugu zangu

alumn

JF-Expert Member
Jul 15, 2018
2,366
3,109
Naandika hapa kwa maumivu makali na hali sasa imekua tata si kama awali naombeni ufumbuzi

Ni Leo mchana nimebahatika kununua dawa ya kuharisha kwa yelo subai (Maasai) ili niharishe na kusafisha tumbo, akanipatia dawa na kuniambia ni funga kazi kua nitumie then nikiona nimechoka ninywe maji ya baridi hali itakata

Sasa wadau niko chooni masaa mawili na nusu naharisha tu majimaji na nimekunywa hayo maji ya baridi hali bado haikati

Msaada ndugu zangu ni nini nitumie kingine niondokane na hii dhahama
 
Umekipata ulichokuwa unakitaka.. Nini tatizo

Hao jamaa siku hizi wahuni wengi
 
Asanteni ndugu zangu. Nimefanikiwa ila nimekiona cha mtema kuni
Hongera usirudie tena;kuna jamaa mmoja alikunywa alovera ili kujikinga na malaria,matokeo yake aliendesha hadi damu...ikabidi ajiwaishe hospitali.Hii inamaanisha dawa nyingi za kienyeji hazina kipimo maalumu kilichokubalika kimataifa kwa matumizi,matokeo mtu anazidisha dozi na kuleta tatizo.
 
hahaha..daah pole mkuu..kuna dada mmoja alileta uzi humu kuwa mume wake kanunua vimbegu kwa jmaa ili asafishe tumbo kilichotokea almanusura mume wake akate Moto maana aliendesha V8 mpaka Wese likakata V8 ikakosa nguvu ilibaki kidogo litumbukie mtaroni kwa Panic ya dereva...

Na kuna siku nilikua nipo kwenye usafir ustadhi mmoja akawa anauza hiyo dawa ni vimbegu fulani vyeusi akatoa angalizo ukinunua usitafune ndani ya basi maana shugul yake si ya kitoto inatakiwa uwe home siku hiyo na hutoki kwenda mahali. Daah niliogopa hadi leo sijawahi katumia.
 
Asee mkuu ni kweli ni balaa ni kimbegu kidogo tu lakini kaz yake haimithiliki, nimeamka bado naendesha mimi nilijua hali hyo imeisha. Sasa naenda tu hospital, ni vizuri pia maana mwili pamoja nauchovu ila nimetoa uchafu but all in all sirudii
 
Write your reply...chukua Cocacola mimina kwenye kikombe tia chumvi kijiko kimoja na nusu cha chai halafu kunywa,haitachukua mda litafunga
 
Back
Top Bottom