Jamani CCM hapa mnajenga ama mnafanya nini ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani CCM hapa mnajenga ama mnafanya nini ?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lunyungu, Jul 13, 2009.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Date::7/13/2009Mamia wakataliwa kuandikishwa katika daftari la wapiga kura Pemba[​IMG]Na Salim Said, Pemba

  ZOEZI la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Jimbo la Magogoni wilayani Micheweni, Pemba limeingia dosari katika siku yake ya kwanza baada ya mamia ya wananchi kutimuliwa na maofisa usalama katika baadhi ya vituo vya uandikishaji na kushindwa kujiandikisha.

  Wananchi hao kutoka vituo vya Kinyasini, Finya na Wingwi Mapofu waliofika katika vituo hivyo na kupanga foleni mapema jana asubuhi, walijikuta wakitimuliwa vituoni na maafisa hao kwa kuwa hawana vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi (Zan ID).

  Maafisa hao waliwaambia wananchi hao kwamba hawapaswi kuonekana katika vituo hivyo kwa sababu hawana Zan ID.

  Wakizungumza na waandishi wa habari, baadhi ya wananchi walilalamika kuwa maofisa wa usalama waliokuwa wamekaa karibu na maeneo ya vituo vya uandikishaji, waliwataka waondoke mara moja vituoni hapo.

  Katika kituo cha Wingwi Mapofu, kulikuwa na maofisa wa usalama waliokuwa wamekaa katika baraza la jengo la kituo hicho wakitoa maelekezo kwa watendaji wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).

  Mwenyekiti wa halmshauri ya wilaya ya Micheweni, Abdallah Ali Said alithibitisha kupokea malalamiko hayo katika siku ya kwanza ya zoezi hilo kwenye Jimbo la Magogoni kisiwani hapa.

  “Ukifika pale kituoni unaambiwa uondoke na maafisa usalama kwa sababu huna Zan ID, hii ni haki kweli," alihoji mtu aliyejitambulisha kwa jina la Khatib Hassan, 27.

  "Mimi nina cheti cha kuzaliwa, kipande cha kupigia cha uchaguzi mkuu wa 2005 na uchaguzi mdogo wa mwaka 2003.”

  Hassan alilalamika kuwa alipokwenda kwa Sheha ambaye anapaswa kutoa fomu za kuombea Zan ID, aliambiwa aende wilayani na alipofika huko aliambiwa anatakiwa kurudi kwa sheha.

  "Ukienda kwa sheha anakwambia nenda wilayani na ukienda wilayani unaambiwa nenda kwa sheha. Wametufanya kama mpira wa kona; sheha apiga chenga, wilaya inafunga goli. Wanatunyima haki zetu hivi hivi,” alilalamika Hassan.

  Naye Mbarouk Rubea, 48, alisema ana sifa zote za kuandikishwa kuwa mpigakura kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar, lakini hadi sasa anahangaishwa hajapata kitambulisho na hatimaye amenyimwa kujiandikisha katika daftari hilo.

  Akiwa amesawajika na mtoto mgongoni, Rehema Khamis, 32, alisema ameanza kukata tamaa ya kupiga kura katika uchaguzi ujao kwa sababu hajapatiwa kitambulisho licha ya kuwa ameshalipa Sh 500 za Zan ID.

  "Hivi sasa nakaribia kulia maana nimeacha kwenda kuvuna mpunga wangu nikaamua kuja huku, lakini nahangaishwa na mtoto mgongoni. Nanyimwa haki yangu na maofisa wa usalama wanatufukuza hapa,” alisema Rehema.

  Hata hivyo, maofisa wa usalama waliokuwa vituoni hapo walikataa kuzungumza na waandishi wa habari na kuwapiga marufuku watendaji wa tume kufanya hivyo.

  Sheha wa shehia ya Mjananza, Hamad Said, ambaye pia ni wakala wa ZEC, alikatazwa na watu walioonekana kuwa ni maafisa wa usalama kuzungumza na waandishi wa habari waliofika kituoni hapo.

  Baada ya kuitwa na waandishi kituoni hapo, sheha huyo alitoka na kusalimiana nao, lakini ghafla aliitwa ndani na kuagizwa asizungumze na waandishi.

  ”Nimekatazwa na wale pale nisiongee na ninyi,” alisema Said huku akielekeza kidole kwa maofisa hao na kurejea ndani ya kituo hicho.

  Katika vituo hivyo kulikuwa na ulinzi mkali wa dola uliojumuisha polisi, askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), askari wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanibar (SMZ) na usalama wa taifa.

  Wananchi wengi kisiwani Pemba hawana Zan ID, hususan wale ambao ndio kwanza wametimiza miaka 18 na wale waliokuwa nje ya Zanzibar. Katika vituo vitatu ambavyo waandishi walitembelea, waligundua mamia ya wananchi walinyimwa haki hiyo kwa kukosa Zan ID.
  Tuma maoni kwa Mhariri
   
Loading...