Jamal Khashoggi mwanahabari mwanamageuzi

Jamal Khashoggi mwanahabari mwanamageuzi

mawazomgala

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2014
Posts
342
Reaction score
212
nz-saudi-201018.jpg

JAMAL KHASHOGGI MWANAHABARI MWANAMAGEUZI

Hatimaye nchi ya Saudi Arabia yatoa taarifa kukubali juu ya kifo cha Mwandishi maarufu mwenye raia wa Saudi Arabia,katika ubalozi wa Saudi nchini Uturuki juma lililopita, taarifa hii imetoka baada ya taarifa mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwa nyakati tofauti na viongozi mbalimbali wa nchi ya Saudi juu ya kupotea kwa mwandishi huyo maarufu katika nchi za Kiarabu.
Taarifa hii imekuja baada ya serikali ya Saudi kuitisha uchunguzi maalumu ili kujua kwa undani nini kimetokea juu ya sakata la mwandishi huyo mwenye umri wa miaka 59, ndani ya ubalozi wa Saudi Arabia katika nchi ya Uturuki, Katika taarifa yake iliyotoka ijumaa jioni ya tarehe 19, oktoba 2018 inadai Jamal khashoggi alifikwa na umauti akiwa ndani ya ubalozi huo na kilichopelekea umauti ni mapigano yaliyosababishwa na mabishano makali kati yake na watu wanaotuhumiwa kusababisha kifo chake tarehe 2,oktoba,2018, ingawa mpaka sasa serikali ya Saudi haijaweka wazi majina ya watu wanaotuhumiwa kuhusika na kifo cha mwandishi Jamal.
Hii ni taarifa ya mwisho kutolewa na serikali ya Saudi Arabia mpaka sasa, ambapo taarifa za awali zilieleza kuwa Bwana Khashoggi aliondoka ndani ya Ubalozi huo akiwa salama.

JAMAL KHASHOGGI NI NANI?
Jamal Khashoggi ni mwandishi maarufu aliyekua akiangazia taarifa kubwa katika mashirika mbalimbali nchi Saudia.
Mwandishi Jamal kashoggi alizaliwa katika mji wa Medina, tarehe 13, oktoba, 1958. Babu yake Muhammad Khashoggi, ambaye alikua na asili ya Uturuki, alioa mwanamke mwenye asili ya Saudi Arabia na alikua daktari binafsi wa Mfalme Abdulaziz Al Saud, muasisi wa Ufalme wa Saudi Arabia.
Jamal alipata elimu yake ya msingi na sekondari nchini Saudi Arabia na kufanikiwa kupata shahada ya usimamizi wa Biashara kutoka chuo cha Indiana (Indiana State University) kilichopo nchini Marekani mwaka 1982.
Jamal Khashoggi alianza kazi nchini Saudi Arabia kama meneja wa duka la vitabu lilifahamika kama Tihama kuanzia mwaka 1983 mpaka 1984. Baadae alifanya kazi kama mwandishi wa gazeti linalofahamika kama Saudi Gazzete na meneja msaidizi wa gazeti la kila siku la Okaz. Aliendelea na kazi za uandishi kwa magazeti mbalimbali nchini Saudi Arabia kuanzia mwaka 1987 hadi mwaka 1990, ikiwemo magazeti ya Al Muslimoon, Asharq Al-Awsat na gazeti la Al Majalla.
Mwaka 1991 khasoggi akawa mhariri mkuu na Kaimu mhariri mkuu wa gazeti la Al madina, nafasi aliyoitumikia mpaka mwaka 1999.
Akiwa katika kazi zake ndani ya tasnia ya habari kuanzia mwaka 1991 hadi mwaka 1999, khashoggi amepata kuwa mwandishi wa habari katika mataifa mbalimbali ikiwemo Kuwait, Afghanistan, Algeria, Sudan, na Mashariki ya kati. Pia yako madai kuwa amewahi kufanya kazi na taasisi ya kishushushu ya nchini Saudi Arabia (SAIA).
Khashoggi alichaguliwa katika nafasi ya naibu mhariri mkuu wa gazeti la Arab News lenye makao mjini Riyadh Saud Arabia, Jamal alishika nafasi kuanzia Mwaka 1999 hadi mwaka 2003.
Baadae Khashoggi alipata nafasi ya mhariri mkuu wa gazeti la kila siku nchini Saudia limnalofahamika kama Al Watan, nafasi aliyodama kwa kipindi sio chini ya miezi miwili, ambapo alifukuzwa katika nafasi hiyo mwezi wa tano mwaka wa 2003 na Wizara ya habari ya nchi ya Saudi Arabia, kwa kosa la kuruhusu mwandishi wa Makala kwenye gazeti hilo kumkosoa mwanazuoni wa Kiislam aliyefahamika kwa jina la Ibn Taymiyyah (1263-1328), ambaye anaheshimika kama baba muasisi wa moja ya mafundisho ya Wahhabi yaliyoanzishwa na mwanazuoni Muhammad ibn Abd al-Wahhab.

MAHUSIANO YAKE NA OSAMA BIN LADEN
Katika miaka ya 1990 Mwandishi jamal Khashoggi alipokuwa akifanya kazi katika gazeti la Al-Madina aliandika kwa undani kuhusu wanamgambo wa kiislamu waliokwenda kupigana katika vita ya kupinga uvamizi wa Usovieti katika nchi ya Afghanistan.
Khashoggi alifanya mahojiano na raia wa Saudia waliojitolea kupigana vita hivyo nchini Afghanistan.
Inataarifiwa kuwa mnamo mwaka 1995 familia ya Osama bin Laden ilimuomba Mwandishi Jamal Khashoggi ambaye anaarifiwa kumfahamu tangu ujana wake nchini Saudi Arabia, wakiamini anaweza kumshawishi Osama kuachana na matumizi ya ghasia katika kuziondoa tawala mbalimbali za kiarabu, na aweze kuomba msamaha kwa watawala wa Saudia ili aweze kuishi maisha ya kawaida.
Osama Bin Laden kwa wakati huo hakua bado mtu anayefahamika sana katika mataifa mbalimbali ya magharibi kama kiongozi wa kundi la al-Qaeda.
Khashoggi alimtembelea Osama Bin laden katika mapango kwenye milima ya Tora Bora, na pia aliwahi kumfanyia mahojiano Osama nchini Sudan pia mnamo mwaka 1995.
Kwa mujibu wa jarida la The Looming Tower Katika ziara hiyo ya kumtembelea Osama nchini Sudan, Khashoggi alimshawishi Osama kuachana na matumizi ya mbinu za ghasia lakini ushawishi wa Khashoggi haukufanikiwa na Osama akaendelea na mapambano dhidi ya Marekani, kitu kilichopelekea khashoggi kuondoka nchini Sudan siku iliyofuatia.
Mwaka 2011 Khashoggi alipofanyiwa mahojiano na gazeti la Ujerumani, Der Spiegel kuhusu uhusiano wake na Osama bin Laden, alikiri kwamba alikua akiikubali mitazamo ya Osama katika siku za nyuma kuhusu matumizi ya mbinu zisizo za kidemokrasia kama kutumia mbinu za ghasia kuziondosha tawala fisadi katika mataifa ya kiarabu.

Pichani: jamal Khashoggi (aliyebeba roketi) akiwa na vijana wa kiarabu waliokuwa wakipigana vita pamoja na Osama Bin Laden nchini Afghanistan. (picha kwa hisani ya Mwandishi Patrick poole)
Kwa mujibu wa jarida la Global News, mwaka 2002 Jamal Khashoggi aliandika Makala katika gazeti la The Daily Star la nchini Lebanon akieleza kwanini alimuunga mkono Osama Bin Laden kwenye suala la vita dhidi ya uvamizi wa Soviel lakini kutokubaliana naye juu ya vitendo vya kigaidi vya kimataifa.
Mahusiano yake na vikundi vya Al qaida yamemletea matatizo mara nyingi hadi kufikia kuhusishwa na ufadhili wa vikundi vya kiislam vyenye msimamo mkali.

MAGEUZI
Khashoggi alihamia Marekani juni mwaka 2017, baada ya kuwepo kile alichokiita tishio dhidi ya maisha yake huku akimshutumu kiongozi wa kudumu wa Saudi Arabia, Mwanamfalme Mohammed bin Salman, kwa kulenga upinzani, na alianza kuandikia shirika la habari la The Washington Post kuanzia mwezi septemba 2017. Katika Makala zake amekua mkosoaji wa sera za serikali ya Kifalme ya Saudia ikiwemo mgogoro wa Saudi na Lebanon, mgogoro wa kidiplomasia kati ya Saudi na Canada, Khashoggi amekua muungaji mkono wa baadhi ya sera za mageuzi za mwana mfalme wa Saudi ikiwemo kuruhusu wanawake kuendesha magari, lakini mara nyingi amekuwa mkosoaji mkubwa wa mwana mfalme huyo ikiwemo kitendo cha kukamatwa kwa mama Loujain Al-Hathloul ambaye alikuwa mtu wa tatu katika orodha ya wanawake 100 mashuhuri katika nchi za kiarabu. Pamoja na ukamataji wa wana harakati mbalimbali wanaopigania haki za binadamu nchini Saudia.

KIFO
Serikali ya Saudi Arabia imekiri kuwa mwandishi jamal Khashoggi amefariki ndani ya ubalozi wake mjini Instanbul Uturuki huku ikieleza sababu ya kifo chake kuwa ni mabishano kati yake na watuhumiwa kitu kilichopelekea mapigano yaliyosababisha kifo chake.
Taarifa za kupotea kwa mwandishi Jamal Khashoggi zilianza kusambaa tarehe 2 oktoba baada ya mchumba wa mwandishi huyo kutoa ripoti kwa maafisa wa usalama kuhusu Khashoggi kupotelea ndani ya ubalozi wa Saudi huku akimsubiri nje ya ubalozi huo kwa muda mrefu bila mafanikio.
Hadi sasa timu ya uchunguzi ya nchi ya uturuki inayofanya uchunguzi wa tukio hilo limeelekeza tuhuma moja kwa moja juu ya ushiriki wa maafisa wa nchi ya Saudi Arabia kwenye mauaji ya mwandishi huyo huku wakieleza kuwa aliuawa kwa kupigwa na kisha mwili wake kukatwa vipande na kuharibiwa.
Mauaji ya Jamal Khashoggi yameibua mjadala mkubwa katika jumuiya za kimataifa huku viongozi wan nchi mbalimbali wakiahirisha safari mbalimbali za kidiplomasia nchini Saudi Arabia.
***********************END**********************
 
Asante kwa TAARIFA mzuri. Ku.be jamaaa alifanikiwa kuwa maarufu. Habari za Oszama nakumbuka tulizipata kabla y smartphone
 
Kulikuwepo na mipango ya siri ama mbinu za kumchafua jina lake ili kuweza ku downplay umuhimu wa kufuatilia mauwaji yake.

Ninaamini kila jambo hutokea kwasababu maalumu. Kuuwawa kwa Kashoggi, fukuto lake halitaisha mapema kama wengi wanavyodhania. Na Saudi Arabia wali miscalculate kama walivyofanya watunga movie wetu. Imebuma.
 
Pichani: jamal Khashoggi (aliyebeba roketi) akiwa na vijana wa kiarabu waliokuwa wakipigana vita pamoja na Osama Bin Laden nchini Afghanistan. (picha kwa hisani ya Mwandishi Patrick poole)
Kwa mujibu wa jarida la Global News, mwaka 2002 Jamal Khashoggi aliandika Makala katika gazeti la The Daily Star la nchini Lebanon akieleza kwanini alimuunga mkono Osama Bin Laden kwenye suala la vita dhidi ya uvamizi wa Soviel lakini kutokubaliana naye juu ya vitendo vya kigaidi vya kimataifa.
Mahusiano yake na vikundi vya Al qaida yamemletea matatizo mara nyingi hadi kufikia kuhusishwa na ufadhili wa vikundi vya kiislam vyenye msimamo mkali.
Propaganda za wasaudi!Wamelikoroga na walinywe! Hovyo sana pia na wale wanaowasapoti kwasababu tu ya maslahi ya pesa. Magaidi wote kasoro mmoja wa sept 11 2001, walitokea Saudia, lakini Iraki na Afghanistan ndo zikashambuliwa. Wapi na wapi?
 
Back
Top Bottom