Jamaa yuko Rumande kwa kosa gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamaa yuko Rumande kwa kosa gani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkulima, Sep 2, 2009.

 1. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2009
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Mbona jamaa kasema ukweli mtupu? Anafanya nini rumande?

   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,382
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  Alitoa maoni yake kama raia,alichokosea ni kuingia maeneo ya ikulu hiyo ni kama kutangaza vita na jamhuri.Angesemea mahali pengine kama vyombo vya habari............aliamua kuifanya ikulu kwa babu yake sasa mwache asote kidogo ajue ikulu ni mahali patakatifu...
   
 3. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  bora wamweke huko apumzike ameacha kuongelea matatizo ya kwao huko aje aongelee ya kwetu
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Huyo keli raia wa Iraq au ni Mtanzania mwenye asili a Iraq.

  Vp raia wa Iraq asifie Azimio la Arusha na Fikra za Nyerere badala ya kusifia Fikra za Saddam?
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa sio raia wa Iraq ni mtanzania wa kabila la Iraqw toka kule Arusha.Waandishi wetu ni vigumu kufuatilia masuala ya kihabari wanakurupuka kuuza habari kwa kugeuza iwe ni mtu wa Iraq.
   
 6. m

  mzanganyika JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 257
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kilichokashifiwa ni kipi?

  Kwani si kweli kwamba Azimio la Zanzibar liliuwa Azimio la Arusha?

  Kwani kuna dhambi gani kuuwa sera iliyoshindwa na kujaribu nyingine?
   
 7. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2009
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Anney Anne sio raia wa Iraq bali ni Mwiraqw wa Endabash, Wilaya ya Karatu. Kesi yake ilipotajwa ilielezwa kuwa ni mkazi wa Mtaa wa Kilombero, Manispaa ya Arusha. Mwandishi alipotosha alipooandika ni raia wa Iraq.
   
 8. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2009
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Mkulima, kama unafuatilia magazeti madai ya kosa la Anney haya hapa:

  Mlemavu kortini kwa kumkashifu Kikwete  na Datus Bornface
  MLEMAVU wa miguu, Anney Anney (50), mkazi wa Arusha Kilombelo, jana alipandishwa katika Mahakama ya Wilaya Ilala, jijini Dar es Salaam, akituhumiwa kumkashifu Rais Jakaya Kitwete.

  Mwendesha Mashitaka, Mrakibu wa Polisi Niama Mwanga, alidai mbele ya Hakimu Samwel Maweda kuwa, mtuhumiwa alitenda kosa hilo Julai 23, mwaka huu, eneo la Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Alidai kuwa, siku ya tukio akiwa kwenye maeneo hayo ya Ikulu, mtuhumiwa alitoa ujumbe kupitia bango aliloliandaa ambao ungehatarisha uvunjifu wa amani kwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Mwanga alidai kuwa, mtuhumiwa alitoa ujumbe wenye maneno ‘Jakaya Kikwete, Ikulu ya Dar es Salaam, Nyerere alilinda ardhi yetu pia utu na uzalendo’.

  Alidai kwamba, maneno mengine ni ‘Mwinyi aliua Azimio la Arusha, Mkapa aliuza mashirika yetu na nyumba za umma, wewe (Kitwete), unauza ardhi yetu kwa Wazungu na Waarabu pamoja na utu na utaifa wetu’.

  Aliendelea kudai kuwa, ujumbe huo pia ulisomeka kama, ‘Udumu ujamaa na kujitegemea, lidumu Azimio la Arusha, zidumu fikra za Mwalimu Nyerere’.

  Mtuhumiwa alikana shitaka hilo na kurudishwa rumande kwa kushindwa kukidhi mahitaji ya dhamana kwani alitakiwa kuwa na wadhamini wawili.

  Kesi hiyo ya aina yake, imeahirishwa hadi Agosti 10 na upelelezi bado haujakamilika.

  Wakati huo huo, mfanyakazi wa ndani, Idd Hassan (19), mkazi wa Buguruni, jijini Dar es Salaam, jana alipandishwa kizimbani, akituhumiwa kwa kosa la kubaka mtoto mwenye umri wa miaka miwili (jina limeahifadhiwa).

  Mwendesha Mashitaka, Inspekta wa Polisi Hamis Mhellya, alidai mbele ya Hakimu wa Wilaya, Afumwisye Kibona kwamba mtuhumiwa alitenda kosa hilo Julai 20, mwaka huu, eneo la Buguruni Malapa.
   
 9. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hiyo siasa tu. Jamaa katoa mawazo yake hivyo sioni ulazima wa kumweka rumande. Rumande zetu zinaweka mpaka wezi wa kuku. Si shangai hata hili nalo. Je angewakashifu ingekuwaje?
   
 10. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Wanaotakiwa kwenda rumande ni wakina Rostam Aziz na genge lake na sio huyu mlemavu wa Mungu!! Hivi hapa nchini haKuna wanasheria wa haki za binadamu ambao wangejitokeza kumuwekea dhamana huyu mpambanaji anaeipenda nchi yake kiasi cha kwenda na kusema maneno ya kweli ambayo yanaowahusu na kuwagusa wanaita uchochezi? Wazungu wanamsemo; YOUR TERRORIST IS MY FREEDOM FIGHTER. HUYU JAMAA NI MPAMBANAJI NA WALA SI MCHOCHEZI KUNA UMUHIMU WA KUMPIGANIA ATOKE HUKO SELO.
   
 11. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #11
  Sep 5, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  jamaa yuko sahihi kabisa nimependa maoni yake .kwani uongo!?
   
 12. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #12
  Sep 5, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sijaona tatizo alilofanya huyo jamaa mpaka atiwe ndani. Alichoongea ni ukweli mtupu na ametumia haki yake kikatiba kama mtanzania kudumisha demokrasia. Niko tayari kumchangia pesa ya dhamana kama inatakiwa.
   
Loading...