Jamaa watatu

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
3,068
Reaction score
277
Jamaa watatu walishinda pesa,walipozigawa wakaamua kila mmoja wao atoe kiasi flani kama sadaka.

Jamaa wa kwanza Wafula akasema:"Mimi nitachora duara,nisimame katikati nirushe pesa juu...zitakazoingia ndani ya duara ni zangu,zitakazobaki nje nitatoa sadaka.

Jamaa wa pili Mutua akasema:"Mimi nitachora mistari miwili,nisimame katikati alafu nirushe pesa juu...zitakazoingia kati ya mistari ni zangu...zitakazokuwa nje nitatoa sadaka.

Jamaa wa tatu Njoroge akasema:"Mimi sitachora kitu! Nitarusha pesa juu...zitakazobaki juu itakuwa nishatoa sadaka,zitakazoanguka chini ni zangu."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…