Jamaa ni mwongo sana na Kila anachomwambia mzazi ni uongo

ahoma

Member
Dec 28, 2021
29
42
Habari za majukumu Wana JF.

Nina jambo linanisumbua naombeni ushauri. Ninaye ndugu yangu mtu mzima na wajukuu anao.

Kila kitu atakacho mwambia mzazi anasikilizwa sana, huyo jamaa ni mwongo sana na Kila anachomwambia mzazi ni uongo na kutuchonganisha wengine Kwa mzazi, sasa mzazi anampenda kiasi Cha kutuona watoto wake wengine wote ni wabaya kwake, pia Kwa sababu mzazi anamwamini sana yeye.

Mzazi anataka na sisi wote tumkubali la sivyo mzazi anakuchukia Hadi kukulaani.

Tulikaa kikao na kumweleza mzazi ukweli wa huyo mtoto wake anayemwamini na kumpenda mno ila mzazi sasa ana hasira na watoto wake wengine 7.

Je hapo tunafanyaje jamani?
 
Back
Top Bottom