Jamaa na paka wake

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,228
Jamaa mmoja alikuwa na mke wake ambaye anampenda sana paka, Jamaa hakumpenda yule paka na kila siku ilikuwa ugomvi.

Siku moja aliamua kumchukua yule paka na kwenda naye umbali wa kilometer 1 na kumtupa huko muda anarudi kwake ile anafika tu akashangaa paka naye anaingia ndani, siku ya pili akaenda naye umbali wa kilometer 5 na kumtupa,ile tu anarudi kamkuta paka ndani akasema kimoyo moyo ngoja kesho utanikoma,
kesho yake akaenda nae umbali wa kilometer 50 akazunguka sanaaa akakata kushoto kulia kulia kushoto kumchanganya paka kisha akamtupa
Muda anarudi nyumbani akampigia simu mke wake.
Mume: helo mke wangu vp huyo paka yupo hapo
Mke: Ndio mume wangu paka yupo hapa tena ametulia
Mume: MPE SIM ANIELEKEZE NJIA YA KURUDI NYUMBANI !!!
 
Hata kama ni copy and paste bado yanchekesha.It means jamaa alichanganya njia huko porini ili paka apotee lakini mwishowe kapotea yeye!
 
Back
Top Bottom