Jamaa kacheza vikoba hewa mwaka mzima kupitia mke wake

Nacheka kama mazuri lol
Boya kabisa duu
Aisee hawa viumbe muwape ushirikiano chumbani tu, ila mengine tufanye siri zetu tu hata kama ni nyumba unampa ufunguo tu
Kama ni pesa weka mbali kabisa, aone tu zinamfikia ila asijue zinahifadhiwa sehemu gani.
 
Ingekua mm simple tu hamna kuingia nae ligi, kumpiga wala kumfokea ila sitakaa nimshirikishe tena mambo yanayohusu hela, assets au mambo yote ya msingi nayoyafanya
 
Miaka nyuma kidogo nilienda kujiendeleza kimasomo nilivyorudi nilipitia kipindi kigumu sana kwan nilikua na madeni Benki nilichukua Hela ya kusomea pia loan board wakaongeza makato maradufu bila kujali ⅓ , afu ndio nimeoa na mtoto mdogo. Wife akaja kunambia ana mchezo wa laki Kila mwezi, akapita kipindi flan akasema kapewa ni zamu tukanunua sofa, Siku nyingine akapewa tukanunua tv " 32. Baadaye sana maisha yalivyokaa Sawa, wife ndo akanambia hakuwa na mchezo na mtu yeyote alikua anazitunza zikifika za kununua kitu flan ndio anajifanya imekua zamu yake kupewa na alifanya hivyo Kwan alijua nisingekubali kutunza Hela Katika hali ile
Hii ndio nafanya mimi aiseez mme wangu anajua anacheza mchezo wa laki3 kila mwezi na anajua tunapokea mwaezi wa sita kila mwaka. Kumbe naweka sijamsanua.. ni mwaka wanne huu ikifika mwezi wa sita tarehe 30 naachia mabunda baaasi maisha yanaenda
 
Kama ni wazo lenu wawili ndani ya nyumba mume na mke kwanini mfikie hatua ya kuwaza kuwekeza akiba kwenye vikundi mitaani?

Kwanini msikubaliane kwa kauli moja kwamba kila siku tuweke sehemu fulani 10K kwa ajili ya kufanya jambo fulani na iwe sehemu ambayo muda wote wewe mume una access ya kuifikia?
Wengi wanatafuta social capital.
 
Back
Top Bottom