Nucky Thompson
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 1,817
- 4,061
Jamaa mmoja amekuwa mkali zaidi ya pilipili baada ya mpenzi wake aliyekua nae kwenye mahusiano muda ambao sio mrefu sana kuendekeza tabia ya kumpiga vizinga, jamaa anasema alishampa huyo dada 200,000 na alifanya nae mapenzi mara 1 tu lakini bado dada anamletea bili za ajabu ajabu kama kodi n.k
Ndipo jamaa akamtolea uvivu na kumwambia kuna wasichana wanafanya kazi wanahenyeka vibaya kwa mwezi mzima wanalipwa 50,000 hadi 100,000 ila yeye amepewa 200,000 bila kufanya kazi yeyote na bado anaendelea kudai apewe nyingine, wakati kwenye mapenzi wana enjoy wote!
Alimuita mwanamke huyo ni mjinga sana na asiye na huruma na hafai kuwa mke kwa kuwa kuna matatizo mengi ya kushughulikia yeye anajiangalia tu mwenyewe..sijui walipigana kibuti au ilikuaje.....